The so called 'GOD' from religions

The so called 'GOD' from religions

Hujaelewa swali.

Sijataka mungu afanye chochote.

Nimeuliza swali.

Mungu mnasema nature yake ni uzuri.

Ana uwezo wote, ujuzi wote, uoendo wote.

Kaumba ulimwengu. Kwa nini kaumba ulimwengu ambao ubaya (kinyume na nature yake ya uzuri) unawezekqna wakati alikuwa na kila sababu, ujuzi, uwezo na uoendo wa juumba ulimwengu ambao ubaya hauwezekani?

Hujajibu hili swali.
Teh,Mkuu ungekausha tu

Hawa theists wa kibongo ni wagumu wa kuelewa

Utakesha,maana mtu anajibu swali asiloulizwa!
 
Ha ha ha Kiranga bwana ha ha unarudia kulekule kusema neno VITABU VYENU .mimi shida yangu useme sababu zako ambazo usifanye reference za "uongo wa vitabu vyetu ". Sijui umeelewa swali langu?? Yan kwa mfano nataka useme huamini kama yupo kwa kuwa "nimejaribu kumuomba nionane naye hakutokea".huo mfano ni kukusaidia ujibu swali langu.
Sababu yangu ni logical inconsistence which turns into a contradiction.

Mungu wenu anajipinga.

Tunaambiwa ana upendo wote, uuzi wote na uwezo wote.

Halafu hapo hapo kaumba ulimwengu wenye kuwezekana kuwepo ubaya, wakati aliweza kuumba ulimwengu ambao ubaya hauwezekani.

Kwa nini?

Ina mana aliweza kuumba ulimwengu ambao ubaya hauwezekani lakini hakutaka tu?

Kama hakutaka tu, lakini uwezo alikuwa nao, hakutubania kwa namna inayomfanya asiwe na upendo wote?

Ni kweli ana upendo wote?

Kama alipenda kuumba ulimwengu ambao ubaya hauwezekani, lakini hakuweza tu, ni kweli ana uwezo wote?

Huyu mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na uoendo wote yupo kweli au ni hadithi tu?
 
Nimekuambia chochote kina hasi na chanya,kwa maana ya chochote,sikukuambia k urudi nyuma.Kurudi nyuma sio chochote,ungejuwa chochote usingesema kurudi nyuma.
Umesema chochote kina hasi na chanya.

Kama muda kwenda mbele ni chanya, basi kurudi nyuma ni hasi.

Unaweza kurudi nyuma katika muda?

Kama huwezi, ni kweli kwamba chochote kina hasi na chanya?
 
Wewe contradiction ya the problem of evil hata hujaielewa, unaita kariri.

Unaweza kurudia hiyo contradiction kwa maneno yako kama kweli umeielewa?
Wewe ndiye huna uwezo wa kuelewa. Unayoita "Evils " ni sahihi Tu kama ni MTU anayeamini Mungu. Waamini Mungu ndiyo ambao huamini ya kwamba binadam anayothamani ambayo inatakiwa kulindwa na binadam mwenzake. Na matendo ambayo ni kinyume na mtazamo wa wenye kuamini juu ya thamani ya binadam ndiyo huitwa "Evil" na pia matendo ambayo ni kinyume na maamrisho ya "Moral God " pia huonwa kwamba ni Evils.

Sasa wewe ambaye binadam ni matokeo ya ajali za kwenye ulimwengu habari ya Good and Evils umeitoa wapi kama sio umrkaririshwa na Atheist waliokuwa wavivu wa kufikiri ?
Unasema kuna Evils ukimaanisha kuwepo kwa Moral law unayotumia kutambua hayo mema na mabaya, ukiamini kuwepo kwa hiyo Moral law una maana kuwepo kwa Moral law giver, na huyo moral law giver ndiye Mungu .

Sababu ya msingi ni kuwa katika habari za Mungu ndipo thamani ya binadam hupatikana nje ya hapo binadam ni kiumbe sawa na viumbe wengine hana thamani yoyote ya ziada katika yeye ndiyo sababu Atheist ndiyo mawakili wa ushoga na utoaji mimba kwa kuwa wao hakuna jambo ambalo ni baya kwa kila binadam isipokuwa ubaya hutegemea MTU mmoja mmoja na mtazamo wake.

Tafuta hoja nyingine kupinga uwepo wa Mungu ili ufundishwe. Futa uliyokaririshwa Kiranga
 
Kwa nini unafikiri ni lazima mungu awepo ili evil iwepo?

Mungu wako ni evil?
 
Kwa nini unafikiri ni lazima mungu awepo ili evil iwepo?

Mungu wako ni evil?
Ficha uvivu wako wa kufikiri. Sijaandika Mungu ni Evil. Nimeandika ni kwa kupitia kuwepo kwa Mungu ambaye alimuumba mwanadam na kumpa uwezo wa kujua Jema na baya ndipo waweza kuleta na kuzungumzia habari za Good and evils
Kwa ninyi Chip incarnate sijui habari ya evils and good imekujaje wakati ninyi ni matokeo ya kiajali Tu kwenye "time and space "

Moral God ndiye aliyeweka kanuni za kutambua mema na mabaya (good and evils ) Nje ya Moral God hakuna evils
Kama hutaki kuelewa subiri time and space ije ku format kichwa chako labda utaja kuelewa
 
Hujajibu swali langu.

Unaleta circular argument.

Swali langu ni kwa nini mungu kaumba ulimwengu ambao ubaya unawezekana. Wewe hujibu swali nililokuuliza, inaniambia bila mungu hakuna evil.

That is a total evasion of the question.

Mungu wako mnasema anajua yote, anaweza yote na ana upendo wote.

For the sake of argument, let's take that as a given. In order to examine matters further.

Kwa nini huyu mungu kaumba ulimwengu ambao ubaya unawezekana wakati alikuwa na uwezo, upendo, ujuzi na sababu zote za kuumba ilimwengu ambao mabaya hayawezekani?

Hujajibu hili swali.
 
Hujaelewa swali.

Sijataka mungu afanye chochote.

Nimeuliza swali.

Mungu mnasema nature yake ni uzuri.

Ana uwezo wote, ujuzi wote, upendo wote.

Kaumba ulimwengu. Kwa nini kaumba ulimwengu ambao ubaya (kinyume na nature yake ya uzuri) unawezekqna wakati alikuwa na kila sababu, ujuzi, uwezo na uoendo wa juumba ulimwengu ambao ubaya hauwezekani?

Hujajibu hili swali.
Mungu anafanya atakavyo sivyo utakavyo wewe,kama wewe unavyofanya utakavyo,sivyo nitakavyo mimi.
 
Teh,Mkuu ungekausha tu

Hawa theists wa kibongo ni wagumu wa kuelewa

Utakesha,maana mtu anajibu swali asiloulizwa!

Unajua kuna kitu huwa sikielewi....nacho ni kama hawa watu wanaoamini katika mungu wanajua hata wanachokifanya.

Kwa nini nasema hivyo?

Kwa sababu, kama wangekuwa wanasema 'wanaamini' tu katika uwepo wa mungu, wangemaliza kabisa hii mijadala isiyo na kikomo.

Lakini pale wanaposhindwa hata kujua wanachokifanya na kuanza kuchanganya imani na uhalisia, hapo ndo wanapokosea.

Kusema mungu yupo na naamini mungu yupo ni vitu viwili tofauti kabisa.

Mtu akisema anaamini kuwa mungu yupo utamkataliaje?

Scratchin' my head!
 
Mungu anafanya atakavyo sivyo utakavyo wewe,kama wewe unavyofanya utakavyo,sivyo nitakavyo mimi.
Wapi nimesema mungu afanye ninavyotaka mimi?

Kusema kwamba idea ya mungu inatakiwa kuwa na logical consistency ndiyo kusema mungu afanye ninavyotaka mimi?

Huyo mungu wenu hawezi hata kufanya atakavyo yeye, maana hayupo, na idea yake iko self contradictory, atafanyaje ninavyotaka mini?

Ukisema mungu anafanya atakavyo, bila kunieleza kwa nini anafanya hivyo, unakuwa unakubali kwamba unamuamini mungu usiyemuelewa.

Ukimuamini mungu usiyemuelewa, unaweza kumuamini mungu ambaye hayupo.

Mungu wako hayupo. Angekuwepo dunia isingekuwa na ubaya.

Dunia kuwa na ubaya ni pingamizi linalokingamana na wazo zima la mungu wako kuwapo.

Unaamini kitu ambacho hata hukielewi.

Kwa sababu huwezi hata kuelezea kwa nini mungu kaumba ulimwengu unaoruhusu mabaya kuwepo wakati alikuwa na uwezo, ujuzi, upendo na sababu zote za kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani.

Unaamini tu. Huelewi unachoamini.
 
Kiranga said:
Kwa sababu huwezi hata kuelezea kwa nini mungu kaumba ulimwengu unaoruhusu mabaya kuwepo wakati alikuwa na uwezo, ujuzi, upendo na sababu zote za kuumba ulimwengu ambao mabaya hayapo
Chief,mbona swali lako linamuwekea Mungu mipaka?

Mungu si robot anayetufanyia kazi zote sisi,hata na yeye ana uhuru wa kuchagua

Mantiki ya msingi ya swali lako nafikiri ni hii

1.Mungu mwenye upendo wote,asingeruhusu mabaya yatokee

2.Mungu mwenye ujuzi wote,angefahamu namna ya kuyazui

3.Mungu mweye nguvu zote,asingeshindwa kuyazuia

4.Mabaya yapo,kwahiyo Mungu mwenye ujuzi,upendo,na nguvu zote hayupo

Nakubaliana na hizo zote,kasoro ya 1 na ya 4

Hiyo ya kwanza ilitakiwa kuwa hivi

1.Mungu mwenye upendo wote,asingeruhusu mabaya yatokee unless awe na sababu nzuri ya kuyaruhusu

Mfano mzuri ni wa mtoto mchanga anayechomwa sindano[chanjo]

Maumivu atakayoyapa wakati sindano inaingia,yataonekana kama kitu kibaya kwake

Lakini lengo la kuchomwa sindano lilikuwa ni zuri tu

Kumkinga na magonjwa!
 
Kutokujuwa wewe kama Mungu yupo,sio sababu ya wewe,utake wanaomjuwa Mungu kuwa Yupo,
nao pia wawe,kama wewe usiyejuwa kama Yupo.Hata wewe ndani ya mwili wako zipo alama mwengine hana,kwa hiyo huyo mwingine kutoziona alama kwenye mwili wako,sio sababu yakufanya alama hizo,ziwe hazipo,na wakati zipo.
 
Tuseme 'Amen' kaka magagafu

Lakini,wana hoja zenye mashiko,ukiwa dhaifu wanakupoteza!
Hoja za kutokuwako Mungu,hazina mashiko,huko kusema Mungu hayupo,ndio uthibitisho wa kuwa Mungu yupo.
Ni sawa na kusema Fulani hana akili,ni pale akili zinajulikana,zipo,lakini kwa fulani hazipo.Kwa hiyo kwa wanaosema Mungu hayupo,ni hayupo kwao kwa kutomjuwa kama yupo,lakini kwa wanamjuwa Mungu,wanajuwa yupo.
 
Lakini kaka,

Mbona hata sisi,tunapinga uwepo wa miungu mingine

Mfano kama wewe ni mkristo au muislam utapinga uwepo wa zeus au mars[Miungu ya kigiriki na kiroma]

Ukiulizwa,kwanini unapinga uwepo wao,utajibuje?

Mimi nafikiri,cha msingi ni kupambana nao kwa hoja na mantiki kaka yangu!
 
Chief,mbona swali lako linamuwekea Mungu mipaka?

Mungu si robot anayetufanyia kazi zote sisi,hata na yeye ana uhuru wa kuchagua

Mantiki ya msingi ya swali lako nafikiri ni hii

1.Mungu mwenye upendo wote,asingeruhusu mabaya yatokee

2.Mungu mwenye ujuzi wote,angefahamu namna ya kuyazui

3.Mungu mweye nguvu zote,asingeshindwa kuyazuia

4.Mabaya yapo,kwahiyo Mungu mwenye ujuzi,upendo,na nguvu zote hayupo

Nakubaliana na hizo zote,kasoro ya 1 na ya 4

Hiyo ya kwanza ilitakiwa kuwa hivi

1.Mungu mwenye upendo wote,asingeruhusu mabaya yatokee unless awe na sababu nzuri ya kuyaruhusu

Mfano mzuri ni wa mtoto mchanga anayechomwa sindano[chanjo]

Maumivu atakayoyapa wakati sindano inaingia,yataonekana kama kitu kibaya kwake

Lakini lengo la kuchomwa sindano lilikuwa ni zuri tu

Kumkinga na magonjwa!
Tukiendelea na mfano wako.

Mungu anashindwa kumkinga mtoto na magonjwa bila sindano?

Na kama anaweza kumkinga mtoto na maginjwa bila sindano, asimkinge mtoto na magonjwa bila sindano, aruhusu sindano inuumize mtoto, myoto alie kwa maumivu ya sindano, mungu huyo ana upendo wote?
 
Kutokujuwa wewe kama Mungu yupo,sio sababu ya wewe,utake wanaomjuwa Mungu kuwa Yupo,
nao pia wawe,kama wewe usiyejuwa kama Yupo.Hata wewe ndani ya mwili wako zipo alama mwengine hana,kwa hiyo huyo mwingine kutoziona alama kwenye mwili wako,sio sababu yakufanya alama hizo,ziwe hazipo,na wakati zipo.
Nani anataka wanaomjuwa mungu wawe kama yeye asiyemjua mungu?
 
Hoja za kutokuwako Mungu,hazina mashiko,huko kusema Mungu hayupo,ndio uthibitisho wa kuwa Mungu yupo.
Ni sawa na kusema Fulani hana akili,ni pale akili zinajulikana,zipo,lakini kwa fulani hazipo.Kwa hiyo kwa wanaosema Mungu hayupo,ni hayupo kwao kwa kutomjuwa kama yupo,lakini kwa wanamjuwa Mungu,wanajuwa yupo.
Ukisema kusema mungu hayupo ni uthibitisho kwamba mungu yupo, basi kusema mungu yupo ni uthibitisho kwamba mungu hayupo.

Na kwa sababu hapa kuna watu wanesema mungu yupo, na wengine wamesema kwamba mungu hayupo, waliosema mungu yupo wamethibitisha mungu hayupo na waliosema mungu hayupo wamethibitisha mungu yupo.

Hivyo tumethobitisha mungu yupo na hayupo.

Unaona habari uliyotuletea ilivyojaa kichaa??
 
Back
Top Bottom