H1N1
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 4,217
- 1,579
Unarejea kuuliza kwa kuwa umekarii jibu la "sijui" lakini Mimi nafahamu kuwa uwezo wote na ujuzi wote unahusisha kuumba ulimwengu wa aina yoyote. Kama uwezo wote kwako ni kuumba ulimwengu wa aina Fulani.Siwezi kuacha kuuliza swali ambalo hujalitatua.
Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote kaumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
Hujalitatua hili swali, na siachi kukuuliza mpaka ulitatue au kukubali kwamba hujui utatuzi wake.
Huo ni uwezo wote kwa "time and space " na sio kwa Moral God.
Waona aibu kwa kuwa udhaifu wa swali lako umewekwa peupe wenye fikra wote wanauona hivyo ili kulinda udhaifu wako umekomaa ati huoni majibu kwenye majibu unayopewa.
Ulidhani kuamini Mungu hayupo ni kwa wenye akili kumbe ni kwa wenye uwezo mkubwa wa kukariri huku hekima ikitumika kiduchu.