H1N1
JF-Expert Member
- May 29, 2009
- 4,217
- 1,579
Nakukumbusha tena, nje ya kuwepo kwa Mungu hakuna Mabaya.Hapana.
Wapi nimesema ulimwwngu siupendi?
Mini tatizo langu si kwamba ulimwengu siupendi.
Tatizo langu mungu wenu anajichanganya.
Huku tunaambiwa ana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.
Logically mu gu wa hivyo yuko consistent na ulimwengu ambao hauruhusu mabaya.
Sasa inekuwaje mungu huyo akaumba ulimwengu ambao unaruhusu mabaya?
Ningeambuwa myngu hatujali, ningejua lbda hakutuina muhimu akatuacha tuteseke na mabaya.
Ningeambuwa mungu hana ywezo wote, ningejua labda alitaka kuumba ulimwengu ambao hauna mabaya, lakini hakuwa na uwezo.
Lakini huyu mungu naambiwa ana uwezo wote, ujuzi wite na uoendo wote.
Kwa nini kaumba ulimwengu ambao ubaya unawezekana wakati alikuwa na kika sababu ya kuumba ulimwengu ambao ubaya hauwezekani?
Sinajibuwa swali hili.
Ukizungumzia mabaya una maana kuna mema pia, hivyo unauwa unazungumzia uwepo wa sheria ya kimaadili ambayo aweza kuitumia kutambua mabaya dhidi ya mema.
Ukitambua uwepo wa sheria ya kimaadili ya kuambua wema dhidi ya ubaya unatambua uwepo wa mweka sheria husika ambaye ndiye Mimi na wengine tunamwita Mungu.
Sasa wewe ambaye ni matokeo ya ajali ulimweguni apohhoji kuhusu mema na mabaya unatumia sheria gani kutambua na kutofautisha?
Lakini pia Wakristo tuna maelezo ya ziada kwa kuwa ndani ya uyaonayo mabaya limo tumaini kwa kuwa kuna ahadi katika maisha yajayo ! Sasa wewe ambaye kwa maisha ni kula them kufa na kuoza lete maswali yenye mashiko kwa imani yako.
Hili swali limekuwa gumu sana kwa miaka mingi kwa kuwa waliotakiwa kujibu walikuwa wanasahau kumtambua muuliza swali.
Swali linajibiwa kwa namna bili kutegemea namna unavyoelewa na kumwelewa muuliza swali ; swali la aina hii inatakiwa kumjibu muuliza swali na sio swali lenyewe kwa kuwa swali liko nje ya msimamo wa (world view) ya muuliza swali