Ukisema Mungu hayupo,ndio uthibitisho wa kuwepo Mungu.Huwezi kusema hayupo,ila ni baada ya kuwepo,kama asingekuwako,usingesema hayupo,kwasababu hayupo.Utasemaje hayupo ikiwa hayupo?Ila utasema hayupo kwa kuwepo Yupo.
Ndo maana
Kiranga kakwambia,"You have crazy way of thinking"
Mimi naweza kutunga jina hapa hapa,
Tuseme,
Mzee pxkqz
Halafu nikaja kukwambia wewe,huyu
mzee pxkqz ndiye aliyekuwa mwalimu wa Alexander mkuu
Na huyu Mzee pxkqz,alikuwa anaishi Afrika
Lakini ukweli ni kuwa,hili jina nimelitunga hapa hapa
Mtu mwenye akili timamu,atahoji
Alexander mkuu,hakuishi Afrika,iweje awe na mwalimu kutoka Afrika?
Baada ya kufikiria kwa kina,akahitimisha kwa kusema
mzee pxkqz hayupo
Ina maana baada ya yeye kusema hivyo,atakuwa amethibitisha uwepo wa
Mzee pxqz?
Na Mungu yupo hivyo hivyo,ni jina tu lililopewa sifa zinazojipinga.