The so called 'GOD' from religions

You are the one who should tell us the creator of your created god
Non of God believers claimed that God was created !
myself l believe da presence of God. But your brain must think who create god
 
Kiranga ,Jimena na wapinga Mungu wengine ni vyema basi mkatupa sababu zenu za kutokuwepo Mungu nje ya hv vitabu vya quran na biblia kwa kuwa hamviamini.hizi kauli za upendo,uwezo na ujuaji alionao Mungu ni maneno mlosikia sisi waabudu Mungu tukisema au nyie wenyewe mumesoma kwenye vitabu vya iman ambavyo tayari hamviamini.sasa kwa kutusaidia mungetoa sababu zingine nje ya vitabu.sijui nimeeleweka??
 
Kama radi kupiga ni matokeo ya mchakato usio na mpango hata wakimbizi kufa ni matokeo yaaiyopamgwa sasa wewe ubaya wa vifo vya radi unahusikaje na Mungu.?
Uliza kuhusu Mungu kwa yanayomhusu kadri ya world view yake. Lakini kutumia world view yako kuuliza maswali kuhusu world view nyingine usiyoikubali ni ujuha.
Pasipo Mungu hakuna Jema wala baya kuna kutii muziki na mihemko ya DNA
 
Uwezo wako mdogo wa kutafakari ndiyo unaona kujipinga kwa Mungu. Ni tatizo lako binafsi sio la Miungu
 
Ukisema Duara yenye pembe tatu IPO?Ndio pembe tatu ipo na duara IPO,mpaka ukauliza duara na ukauliza pembe tatu,ni vitu viwili tofauti,ambavyo vipo.

Ukiuliza bachelor aliyeoa,ndio ubachelor upo na kuoa kupo,alianza kuwa bachelor ndio akaoa.Bikra aliyezaa, pia yupo, alianza ubikra ndio akazaa.Kwa hiyo ubikra upo na uzazi upo.Vyote ulivyovitaja vipo.

Kumbuka huwezi kusema hakuna bila kuwapo,kama hakukuwapo basi huwezi sema hakukuwapo,ila kukikuwapo ndio utasema hakukukuwapo.
Unaposema Mungu hayupo, ndio kuthibitisha kuwa yupo.Kama angekuwa hayupo,usingesema hayupo,ni baada ya kujuwa yupo,ndio ukasema hayupo kwako,lakini kwa wengine yupo.
 
H1N1 said:
Kama radi kupiga ni matokeo ya mchakato usio na mpango hata wakimbizi kufa ni matokeo yaaiyopamgwa sasa wewe ubaya wa vifo vya radi unahusikaje na Mungu.?
We ukapimwe akili!

Matetemeko ya Ardhi yanayoua watu kila mwaka,Njaa,Tsunami na magonjwa bado Mungu hausiki

Kwahiyo yeye anafurahia kuona watu wakifa kama hivyo?
Uliza kuhusu Mungu kwa yanayomhusu kadri ya world view yake. Lakini kutumia world view yako kuuliza maswali kuhusu world view nyingine usiyoikubali ni ujuha.
Pasipo Mungu hakuna Jema wala baya kuna kutii muziki na mihemko ya DNA
Hata ya ham ya kukujibu sina

Maana kichwani mwako hakuna kitu.

Talk to the hand!
 
Aliyezaliwa kipofu wa macho,hajawahi kuona jua,atasema hakuna jua,kusema kwake hakuna jua,ni baada ya kusikia kuna jua,lakini halioni,kwa kutoliona kipofu jua na kusema hakuna jua,sio sababu ya wanaliona jua kwao pia iwe hakuna jua.

Na ni vilevile,kwa mwenye upofu wa moyo,asiyemuona Mungu kwa moyo,iwe sawa kwa wanaomuona Mungu kwa moyo,ikiwa wewe humuoni Mungu kwa moyo,sio sababu yakufanya wanamuona kwa moyo,nao iwe kwao kama wewe usimuona kwa moyo,Mungu,wakati wao wanamuona kwa Moyo.

Ni baada ya wewe kusikia wanaomuona kwa Moyo kama Mungu yupo,ndio wewe,kwa vile humuoni kwa moyo, ndio ukasema hayupo. Kwa hiyo kusema Mungu hayupo,ndio kuthibitisha kuwa yupo.
 
Hujathibitisha kwamba mungu yupo.

Unaleta hadithi ndefu zinazojikanganya.

Thibitisha kwamba mungu yupo kwanza.
 
Unaweza kuwa kipofu, ukamshika tembo mkia, ukaambiwa huyo ni tembo, ukapewa kamba, ukaishila ukaona ni kama mkia wa tembo, ukasema kamba na tembo vina umbo sawa.

Kama binadamu ana tatizo la upofu, suluhisho ni kutafuta kuona/ kujua.

Kutafuta kujua hakuji kwa kuamini tu.

Kunakuja kwa uchunguzi.

Mpaka sasa hakuna uchunguzi uliothibitisha kuwapo kwa mungu.

Wote wanaosema mungu yupo, wanasema hivyo kwa imani potofu ambazo tushazipangua hapa.

Unaweza kuthibitisha mungu yupo?
 
Hujathibitisha kwamba mungu yupo.

Unaleta hadithi ndefu zinazojikanganya.

Thibitisha kwamba mungu yupo kwanza.
Huko kusema Mingu hayupo,ndio uthibitisho wa kuwa Mungu yupo.
Huwanza kuwapo, ndio ikaja kutokuwapo.

Na unaposikia hakipo,ni kuwa kipo,lakini hakipo machoni mwako au moyoni mwako,lakini kwa wengine kipo. Na hata ukisikia fulani ampenda Fulani,sio lazima wewe umpende huyo fulani,ndio ujuwe kama Fulani ampenda Fulani. Anayejuwa Fulani ampenda Fulani,ni yule anayeziona hizo athari za huyo anayempenda na anaypendwa.

Na hivyo hivyo,kutokuona kwako athari za Mungu, sio sababu kwa wanaona nao wao kama wewe usiyeona hizo athari za kuwepo Mungu.
Kwa kusema Mungu hayupo,ndio uthibitisho tosha wa kuwa Mungu yupo.
 
Sitaki kukupa sababu nje ya vitabu vyenu.

Kwa maama mtasema si sababu za kweli.

Sababu za kitokuwepo mungu zipo katika vitabu vyenu.

Vitabu vinasema mungu wenu anajua yote, ana nguvu zote, ana upendo wote. Sawa?

Sasa basi, kama mungu ana ujuzi wote, ana upendo wote na ana uwezo wote, turudi nyuma alipokuwa anauumba ilimwengu.

Aliweza kuumba ulimwengu wa aina yoyote. Hakuna kikichomzuia.

Aliweza kuumba ulimwengu ambao manaya hayawezekani kufanyika. Yanawezekama mazuri tu.

Lakini hakuumba ulimwengu huo.

Kwa nini hakuumba ulimwengu huo na yeye alikuwa na uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote?

Kazini kwangu softwareengineer akiwa na uwezo wa kutengeneza software isiyo crash, halafu akatengeneza software inayocrash, anafukuzwa kazi kwa uzembe.

Na huyu hana uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Kwa nini mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote tunamuwekea standards za chini zaidi ya software engineer?

Kwa nini mungu kaamua kuumba ulimwengu ambao mabaya yanawezekana wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani?
 
Onvioisly either the concept of consecutive application escaoes you or you are jusf being funnily evasive.
 
Kama kusema mungu hayupo kunathibitisha kwamba mungu yupo, basi kusema mungu yupo kunathibitisha kwamba mungu hayupo

Na hapa tumesema mungu yupo na hayupo.

Kwa hiyo mungu hayupo na yupo.

You have a crazy way of thinking.
 
Hoja kama hizi ndiyo tunazoziita non sequitur

Duara lipo,pembetatu ipo,Lakini pembetatu duara haipo

Bachelor yupo na kuoa kupo,lakini bachelor aliyeoa hayupo

Bikra yupo,kuzaa kupo
Lakini bikra aliyezaa hayupo

Ukishaa zaa,sio bikra tena

Kwani nikisema 'mzee Panknqzk' hayupo?hapo nitakuwa nimethibitisha yupo

Unajua 'mzee Panknqzk' ni nani?
 
Huyo jamaa kashindwa kujibu hoja kajitia uchizi tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…