sokoMchizi
Member
- Oct 15, 2022
- 50
- 210
Duh , Dunia Ina mambo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante kipenzi
-Kwanini ulimwachia vitu vyote hivyo?MWANZO WA MAISHA MENGINE
Baada ya kuja na dada yake pale kukawa na kikao mwenyewe akaniomba aniambie kila kitu,me nikamwambia aniambie tu ukweli
Akaniambia ni kweli alikuwa anadate na yule mzee na walianza nae kitambo alikuwa kama sugar dady wake na alikuwa anasafiri nae sana kwasbabu huyo mzee nature ya kazi yake ni kusafiri sana alikuwa anampa hela na nini vitu vingi hapo kati kati alikuwa anamsaidia sana.
Hapo tulikuwa wawili dada mtu alitupisha nikamuuliza swali nikamwambia niambie ukweli kuhusu mtoto na naomba usinidanganye ili nirudishe imani kwako na kwa ufupi tu nimeshachukua sample ya nywele nataka kupeleka kupima DNA(hii nilimdanganya),so naomba ukweli niupate kwako nisiende kuupata sehem nyingine
Nikaona mtu akapiga magoti huku analia akanii jina langu kiukweli huyu mtoto ni wa flani akamtaja yule mzee
Nikamuuliza what happened ilikuaje hadi ukapata mimba ya yule mzee
Akaniambia yule mzee ni mtu mwenye mke na watoto wakubwa tu na mimi niliona kwenye picha ya yule mkwe wa yule mzee facebook
Akasema baada ya kudate nae akiwa side chick akaja kukutana na mimi badae yule mzee aligundua kuwa anadate na mimi kwa sababu alikuwa ratiba zake zikawa hazieleweki kama zamani kumbe kipindi hicho yupo na mimi
Yule mzee anasema akamuuliza kuhusu kupata mtu mwingine akasema ndio anaye mtu mwingine akulizwa kama ananipenda akasema ni kweli ananipenda
Yule mzee akampa option kuwa kama akiniona nafaa basi aendelee na mimi,basi kumbe kipindi hicho huku mapenzi yamenoga kwangu story niyingi company nzur na akasema kwangu akaona kuna feature kule ye alikuwa kama side chick tu
so akamwambia mzee , mzee akawa mbishi kumwachia aende mara amtishie kuwa atanifata aniambie kuhusu uhusiano wao sasa sijui alikuwa anaona angeharibiwa kotekote sasa dada akawa anatumanage wote kwa pamoja.
Akaniambia kipindi flani nilisafiri kama miezi 2 hv hatukuonana nikiwa narud dar yeye anakuwa amesafiri kumbe dada alikuwa ameshakata shauri la kuachana na mzee ili aje kwangu kwa hiyo alikuwa kama amempa mzee mara ya mwisho kama ndio ya kuagana na mzee alikuwa hawez kuwithdraw since wako pamoja ndio mana kama unakumbuka kule mwanzon aliniuliza ninawezaje kumbe mzee ilikuwa hivyo na anhisi hicho kipindi ndio alipata ujauzito coz alichanganya siku zake na mzee kama alimfanyia kusudi kwasababu alivyomwambia mzee akamwambia atalea.
Me baada ya kurudi tulionana almost after miezi miwili kwa hiyo huyo mtoto sio wa kwangu ila naomba sana nimsamhehe yeye alishaachana nae.
Nikamuuliza mbona anakupigia kila siku kama umeachana nae?akasema anamsumbua kujuli hali mtoto
Nikamuuliza mbona kuna transactions anakutumia naona unazipokea akawa hana jibu ansisitiza nimsamehe.
tukarud nyumbani nikamwambia naomba nitafakari na naomba usije ukawapigia simu nyumbani kwetu kuwalilia kwa sasa kwani wamesikitishwa sana ka hili (nilimwambia hivyo ili asipige simu home kwani alikuwa amekubaliuka sana asilete complications zingine ila kiukweli hapo home sikusema chochote)
Basi nikaondoka nikaenda nikaenda kwa mshkaji wangu mmoja usiku ule nikamzuga gheto kuna wageni kesho nikaamkia job nikarud tena kwa mshakji,yeye alikuwa anapiga simu sipokei namtumia tu sms niko salama.
Baada ya kutafakari sana nikaona siwez kuishi kwenye uhusiano ni bora nikae pembeni basi siku ya tatu nikarudi nyumbani nikamsalimia nikambeba mtoto nikamwangia sana kwa huruma malaika yule hana hata hatia na alikuwa maeshanizoe kama baba yake coz kila jion nikirud lazima nicheze sana ndio alale, nikasema wacha niwapishe wawe na maisha yenye amani nikalala nyumbani,
Kipindi hicho pale tulipokuwa tunakaa ilikuwa kama miez miwili hv kodi kuisha kulivyokucha nikaenda bank tulikuwa na saving zetu kidogo nikampigia mwenye nyumba nikamwomba nimwekee kodi mana miez michache iajyo naweza nisiwe vzur alikubali nikmwekea kodi ya miezi 6 na kiasi kilichobaki kidogo nilichukua.
nilivyotoka bank nikarud mtaa flani nikamwomba dalali anitafutie chumba kimoja,kufika jion akawa amekipata nikaenda nikalipia mwenye nyumba akaniambia hata kesho niende kuhamia.
Nikatoka hapo jioni nikaarud nyumbani mud huo mi nalala sebuleni
Kesho yake nikaenda mwenge nikanunua godoro na ndoo moja na kopo la kujimwagilia,nikanunua na pasi ya philips nakumbuka,nikaenda kwenye chumba kipya nikanunua taa nikanunua na net na kamba nikfunga tok =a kwenye dari
Jioni nikarud home pale nikamwita nikamwambia mimi nimekusamehe ila siwezi kuendelea na wewe tena na pia hili pia sijawaambia watu maana ni aibu yetu sote naomba iwe hivi me naomba niondoke hapa nyumbani nakuachia kila kitu vitu vya ndani hadi gari naomba nikuachie kwasababu tulilinunuan sababu ya huyu mtoto me nitaenda kuanza upya basi nikaingia nikachukua vyeti vyangu,mashrt na trousers za kuvaa ofisini na viatu vyangu na slipers nikaweka kwenye bag dogo niakondoka
hakuamini akawa anaivuta huku analia me niakondoka zangu nikaenda kwenda kuanza upya kwenye kagheto changu.
Na huo ndio ukawa mwisho wa uhusiano wetu,alinitafuta sana badae akawa hadi anakuja kunisuburia ofisini akaja kuona nimeamua hivyo basi na yeye akaamua aanze maisha yake
Hatukuwasiliana kwa muda kidogo kuna muda hapo kati kati tuliwasiliana kidogo na yule mtoto anaendelea vzur sasa hv kakuwa mkubwa huwa namwona kweye status akimpost na kwa upande wangu nashkuru naendelea vizur
Ahsanteni
Mwisho.
Nitake radhi kuniita Gily baby zuchu😀
Nimebahatika kukisoma kisa Cha jamaa. Aliyopitia sio madogo
Nitake radhi kuniita Gily baby zuchu😀
shukrani sana ngoja nipite nayo kwa spidi kali 😁
Nimebahatika kukisoma kisa Cha jamaa. Aliyopitia sio madogo
Hakuna haja ya kuomba radhi mkuu, imeeleweka hiyo. Gily baby zu 😅😅😆😆
Keyboard niliyotumia mwanzo haina neno 'na'
Uzuri jamaa haitaji ushauri, amejaribu kushare nasi life experience yake.Swadakta mkuu
Uzuri jamaa haitaji ushauri, amejaribu kushare nasi life experience yake.
Ila kiatu chake ni kikubwa, sio rahisi kukivaa
Ni kweli usemalo, ila kwenye maisha progress ni muhimu sana. Hakuna anayependa kuanza upya, tena baada ya jitihada kubwa sana alizofanya.Wachuchu wapo wengi mkuu, jambo rahisi sana hilo...
Ingekuwa issue kama angeungwa gridi, lakini hili la mtu mmoja kutoa kitumbua chake kwa mwengine...nawe unatafuta kitumbua kipya maisha yanaanza kivingine
ila mwishowe ikabidi aachie vyote.