The Torch on Kilimanjaro: kitabu cha watoto kuhusu Historia ya Baba wa Taifa

The Torch on Kilimanjaro: kitabu cha watoto kuhusu Historia ya Baba wa Taifa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
"THE TORCH ON KILIMANJARO" KITABU CHA WATOTO KUHUSU HISTORIA YA BABA WA TAIFA

1630435638847.png


Miujiza ya Mwenyezi Mungu haiishi.

Maofisa kutoka CCM Dodoma walikuwa wamemaliza mazungumzo na mimi kuhusu mengi katika historia ya Mwalimu Nyerere, TANU na mambo mengi yaliyotokea wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kabla ya kuagana wakataka waikague Maktaba ina nini.

Ghafla nasikia mtu anasoma kitabu kwa sauti.

Natupa jicho naona kitabu kinachosomwa ni "The Torch on Kilimanjaro."

Naangalia saa yangu naona ni muda mchache sana umebakia katika nukta adhana itatoka.

Naam haukupita muda adhana ikapigwa.

Msomaji anasoma kipande cha safari ya Julius Nyerere UNO mwaka wa 1955.

Kwangu mimi ni kama vile naisikia historia hii kwa mara ya kwanza.

Kitabu kimeandikwa kwa staili ya kusomwa na watoto wa shule za msingi.

Wahariri wa Oxford University Press, Nairobi (OUP) walini-"couch," namna ya kuwaandikia watoto wadogo hadithi katika matukio ya kweli ya historia ya uhuru ili wajifunze historia ya nchi yao.

Binti anakisoma kitabu kwa fasaha na sauti iliyojaa furaha.

Namwangalia namuona kama vile mwalimu amesimama mbele ya darasa anawasomea wanafunzi wake historia ya safari ya kudai uhuru ya TANU na Julius Nyerere.

"Allahu Akbar, Allahu Akbar," adhana inatoka.

Msomaji anaendelea kusoma...
Nimenyamaza kimya naijibu adhana kimoyomoyo.

Msomaji anaendelea kusoma.
Adhana imemalizika nawaomba wageni wangu tuagane.

"Mzee Mohamed unatufukuza..."

Kwa masikitiko nawajibu, "Wanangu historia hii ni ndefu mje tena kuna mengi ya kuzungumza kati yetu."

Wananijibu kuwa wao wako Dodoma.

Kitabu kinawekwa chini lakini namuona vidole vyake bado vinafungua kurasa.

Najua ni picha anazoangalia kitabuni ndiyo zilizokamata akili yake.

Vitabu vya watoto vina picha nyingi za maudhui iliyoandikwa na hizi picha ndizo zinazowasaidia wanafunzi kuelewa na watoto kupenda vitabu.

Nimeagana na maofisa watafiti wa historia kutoka CCM Dodoma bado wakiwa na hamu ya kutaka kujua kitabu kina nini katika historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Kitabu hiki kinasomwa kote Afrika ya Mashariki na Kati katika shule za msingi ila nchini petu Tanzania.
OUP wanashangazwa na hili.

Huniuliza kulikoni?
Nawajibu sina jibu.

Hivi sasa OUP wanakwenda toleo la tatu.
 
Back
Top Bottom