Nketi,
Umerejea lakini naona umekuja na kejeli.
Mie kujibu kejeli kwangu ni muhali.
Ila kwa faida ya ukumbi nitakuwekea kwa muhtasari habari za
Idd Faiz Mafongo.
Mafongo alikuwa mwekahazina wa Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika na wakati
huo huo alikuwa mwekahazina wa TANU.
Mafongo alihudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Arnatougo Hall Agosti 1954.
Mafongo ndiye likabidhiwa jukumu la fedha kwa ajili ya safari ya Nyerere ya kwanza
UNO 1955.
Mafongo ndiye liyemjulisha Nyerere kwa Sheikh Mohamed Ramiya wa Bagamoyo.
Yapo mengi.
Labda Nketi nikukumbushe kitu kidogo.
Mkwawa, Kinjiketile, Selemani Mamba, Ali Songea Mbano, Abdallah Mchiama, Abushiiri bin
Salim na mashujaa wengine walionyanyua silaha dhidi ya Wajerumani wote hao walikuwa
Waislam kama unavyoona hao hapo chini waliokuwa na Nyerere katika kupigania uhuru wa
Tanganyika.
Na huu si uzushi.
Kushoto Kwenda Kulia:
Idd Faiz Mafongo, Sheikh Mohamed Ramiya, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro
na Haruna Taratibu. Picha imepigwa Dodoma Railway Station wakiwa katika harakati za kufikisha ujumbe
wa TANU kwa wananchi.