Ngoja nikupe mfano rahisi kutoka Ujerumani.
Huwezi kwenda Ujerumani ukakuta hata alama ya barabarani imeandikwa Kiingereza. Lugha ya kufundishia kuanzia chekechea mpaka PhD ni Kijerumani (isipokuwa kwa masomo ambayo wameweka wazi yatafundishwa kwa lugha nyingine), lugha ya mahakama, sheria, serikali, bunge ni kijerumani.
Kwa ufupi ni nchi moja tu Huko Ulaya ambayo wanaongea Kiingereza kama lugha yao kuu, nayo ni Uingereza.
Kutokana na muingiliano mkubwa ulaya wajerumani inawalazimu wajifunze lugha zaidi ya moja ili waweze kuwasiliana katika mambo ya biashara n.k, hivyo kiingereza kinaongewa pale tu kinapohitajika.
Huwezi kwenda kwenye mgahawa pale Stuttgart halafu muhudumu akakuuliza unahitaji nini kwa Kiingereza, hilo sahau. Maeneo mengine kama huongei Kijerumani haupewi huduma.
Na hivyo hivyo kwa nchi zote zilizoendelea, iwe Japan, Urusi, Uswidi au Uholanzi.
Sisi huku Afrika na akili zetu za kitumwa tunadhani kuongea sana lugha ya kigeni ni kustaarabika, na ndio maana wamefanikiwa kututawala kifikra.