MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Hili lipo kwa Watanzania wengi, wametelekeza lugha zao za asili kiasi cha kutia huruma. Unakuta hata vijijini wanasalimiana kwa kilugha halafu inaishia hapo, mengine yote wanakimbilia Kiswahili, hawana uwezo wa kuendeleza mazungumzo kwa lugha yao ya asili zaidi ya salamu.
Ni hatari sana maana hata ukiangalia uandish wao kwenye hicho Kiswahili ni tabu tupu, sasa mtu anaishia kuwa kama mtumwa, Kiswahili hakijui kwa ufasaha, lugha yake ya asili pia haijui zaidi ya salamu, Kingereza ndio kiliwakataa kata kata.
Japo kuna wale hujaribu, hususan wale ambao wamepata fursa ya kutengamana na watu wa kutokea kwenye nchi majirani, waliopo maeneo ya mipakani, hao bado hawajatelekeza lugha zao. Haswa Wahaya, Wasukuma, Wachagga, Wamaasai, Wameru, Wakurya n.k. Hawa hawajamezwa kabisa.
Uwezo wa kuongea lugha kadhaa ni jambo huniletea fahari sana, nikiwa kijijini huwa naongea lugha yangu ya asili bila kuchakachua hata neno moja, nikiingia mjini kwenye maofisini naachia Kingereza na Kiswahili hadi raha, na pia nimejifunza lugha kadhaa za Kiafrika. Huwa nahakikisha wanangu wanaongea lugha zetu za asili, sio kuishi mjini kama watumwa huku wakiachia milegezo.