The Voices From Within: "Mahakamani Watashindwa Tena!" Sababu ni Mawakili! Jee Tanzania Tuna Mawakili wa Calibre ya Murtaza Lakha?Jitokezeni Kusaidia!

Eti hawakutendewa haki!
Kwa hiyo wewe ni mahakama inayoamua mwenye haki?
Kazi ya mahakama ni kuhukumu kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni, lakini watu tuliojaaliwa jicho la haki, tunaiona haki with naked eyes.
  1. Kama kina Mdee hawakuteuliwa na vikao vyovyote vya chama, maana yake ni wamefanya forgery hivyo kabla ya kutimuliwa, Chadema walipaswa kwanza wathibitishe kosa.
  2. Baada ya kuuthibisha forgery walipaswa kuandikiwa barua za mashitaka na kutakiwa kujieleza kwa maandishi na kupewa siku 14.
  3. Baada ya siku 14, ndipo Chadema ingeitisha kikao cha CC kinachokaa kama mamlaka ya nidhamu na kuzisoma majibu ya barua za utetezi wa wabunge hao 19. Mdee anakuwa amesimashwa tuu na barua ya utetezi ya Mdee haisomwi na CC ya Chadema kwasababu CC ya Chadema sio mamlaka ya nidhamu ya Mwenyekiti wa Bawacha, Halima Mdee.
  4. CC ya Chadema kama havijaridhika na maelezo yao, inawata kujieleza na kuhojiwa, kisha inafikia uamuzi wa kuwatimua kihalali na kwa asiye ridhika na uamuzi wa CC anapewa fursae ndani ya siku 30 kukata rufaa Baraza Kuu.
  5. Kikao cha Baraza Kuu kinaitishwa na kukaa kwa ajenda 2. Ajenda ya kwanza, kinakaa kama mamlaka ya nidhamu na kulisikiliza shauri la Halima Mdee na kuusoma utetezi wake, na wasiporidhika na maelezo yake, wanamuita kumhoji na kufikia uamuzi.
  6. Kisha Baraza Kuu linakaa kama Mamlaka ya rufaa za wale wabunge 19. Kazi ya kwanza ya kikao kinachokaa kama mamlaka ya rufaa ni kwanza kujiridhisha katika hukumu ikiyotolewa katiba sheria taratibu na kanuni zilifuatwa. Kisha inasikiliza rufaa zilizo mbele yake na kuzitolea maamuzi ya kikao cha Baraza Kuu Chadema kwa wale wabunge 18, ni final and conclusive.
  7. Baraza Kuu la Chadema halina mamlaka ya kumtimua Mdee bali lina uwezo wa kupendekeza kwa Mkutano Mkuu Mdee atimuliwe, na Mdee ataarifiwa aumuzi huo, asiporidhika anaweza kukata rufaa Mkutano Mkuu.
  8. Kisha Mkutano Mkuu unaitishwa ndio pekee wenye mamlaka ya kumtimua Mdee.
  9. Uanachama wa chama cha siasa sio sawa na mapenzi ndani ya ndoa, mapenzi yakiisha unaandika tuu talaka mnaachana, uanachama wa chama cha siasa unalindwa na katiba sheria taratibu na kanuni, haufukuzi mwanachama kama kufukuza mke penzi limekwisha!.
  10. Lazima Chadema wajifunze kufanya mambo yake kwa mujibu wa katiba yake, wasipofuata katiba yao kwa hiari yao wenyewe, watafuatishwa katiba yao kwa lazima.
P
 
Mkuu, mahakama haitungi sheria, inatakiwa kutafsiri sheria na kuishia kwenye tafsiri tu, kazi ya kutunga sheria ni kazi ya bunge, maana mahakama kutunga sheria kwenye hukumu zake inakuwa imeingilia muhimili wa bunge.

Rejea maamuzi ya Jaji Mkuu Nyalali kwenye kesi ya Bi. HAWA MOHAMED v ALLY SEFU 1983 TLR 32 aki-quote maamuzi ya Jaji Parke kwenye kesi ya EGERTON v BROWNLOW (1853) 4 HL Cas 196.

"It is the province of the legislature to determine what is best for the public good and to provide by proper enactments. It is the province of the judge to expound the law only by sound reason and just interference, not to speculate upon what is best in his opinion for the advantage of the community."
 
Kama ho mawakili wa kina Mdee watashindwa kesi basi watakuwa wameshindwa na mawakili wenye caliber ya Lakha.
 

Sehemu ambayo chadema walifeli ni like kikao chao Cha kwanza cha kuwafukuza

Pale ndio walifeli, na Jambo lingine paskali serikali inajua wale wameingiaje, kuwatoa Leo kwamba waliingia kinyume wakati time ndio ilipeleka majina am so sure watu wengi mpaka Haji mutungi atakuwa kwenye shida
 
Mkuu Paskali, nilikuwa nje ya DSM ndiyo naweza ku comment sasa baada ya kutulia.
Mkuu Jidu, Jidu La Mabambasi , hakuna kitu kizuri kama kusoma kitu huku umetulia
Inaelekea una some sort of personal attraction to Mdee and the 18.
Mimi ni pia ni binadamu, na mwili wangu umeumbwa kwa nyama na unamahitaji yale ya kibinaadamu kama binadamu wengine wote, miili yetu inahitaji chakula na sisi watu wa Kanda ya Ziwa toka makabila ya wafugaji, tunapenda sana kutafuna na ni watafunaji wazuri kuanzia kutafuna Karanga hadi kutafuna nyama, hivyo kama kuna nyama yoyote na inatafunika hakuna ubaya wowote kwa mtu yoyote kutaka kuitafuna kama inalika na inatafunika!.

Na kuna wanadhani utetezi wangu kwa wanaoporwa haki nimeanza na kina Mdee, no!

Angalia terehe ya bandiko hili Mbunge wa CCM, Esta Bulaya, Afanya Tukio la Kishujaa Mjini Dodoma!
na hili Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili Kuwatendea Haki Watanzania 2015!
na Vicky Kamata Anastahili Pongezi!, Asimama Kidete Kupinga Uonevu, Ubabe na Double Standards za Zungu!
na Membe, Japo Umeonewa, Usifanye Kosa la Lowassa!, Ila CCM ya Ajabu!, Uamuzi based on Illegal Evidence ni Void Ab Initial!. hivyo utetezi wa kutetea watu sikuanza leo na sikuanza na Halima Mdee!
Tatizo lililopo kisheria ni jinsi Mdee and the 18, walivyofika pale walipo.
Hapa ndipo mzizi wa fitna ulipoanzia. Wewe mwenzetu inajua walifikaje Bungeni?.
Sasa mwanasheria anayeweza kutetea forgery ya nyaraka zilizowakilishwa bungeni kwa Ndugai, naye akazikubali, huyo mwanasheria atakuwa kiboko.
Kumbe unadhani Bungeni zimewasilishwa nyaraka za forgery?. Naomba nikusaidie kama kuna forgery yoyote, then ni nyaraka zilizo wasilishwa Tume lakini barua za uteuzi kutoka Tume kwenda Bungeni ni authentic bonafide genuine.
Chadema kabla ya kuwahukumu kilipaswa kujiridhisha kwanza. Je kuna ushahidi wowote usiotia shaka wa forgery?.
Kwa jinsi ndugu yangu Paskali unavyoliweka syala inaelekea ume kuwa subjective, na siyo objective.
Kwenye hili nakubaliana na wewe, kiukweli kabisa hapa nakubali udhaifu, nina hasira sana na mibaba iliyokataliwa na wananchi kwenye sanduku la kura halafu wadada wanapewa viti vya ubwete, mibaba inawaonea wivu inaamua kuwazuia ili tukose wote.
P
 
Karma amkwa sababu zipi!?

Ujiunge na yule mzilankende alieunajisi uchaguzi na kuua baadhi ya watu halafu karma iwa strike wengine walionewa halafu wewe ubaki salama.!? Basi karma haitokuwa fair.

Na there will nothing so called karma.

Unafonyi barua unajipitisha ubunge unsshirikina na dhalimu mnajiapisha mnaanza kula jasho la walipa kodi isivyo haki maana hamkuipata hio nafasi kwa haki eti karma iwapige wale waliokata kuwa hawakuchagua na kupitisha.

Hii karma itakuwa karma ya aina gani !?

Labda kuna aina za karma tofauti tofauti!?

Tunatumia karma kupotosha !? Au kuitumia karma ya personal interests.!?

Mr shaman , prophet of doom. At his best.

Aisee!!
 
Mkuu Selikavu , kwanza mimi sio learned brother, kwasababu mimi sio wakili, na ili uitwe a learned brother lazima kwanza uwe ni wakili msomi.
niseme hakuna wakili ambaye ni competent kwenye maeneo yote...
True, ila pia kwenye filing, sio issues za competence ni issue ya procedures tu ombi linajazwa by application ya chamber summons supported by affidavits kwa makosa kama haya wakili wa type hii ata argue kitu kweli kwenye certiorari na mandamus?.
P
 
Pole Paskali,
Kama kweli una uhakika kutokea moyoni mwako kuwa akina Mdee waliidhinishwa kihalali na CHADEMA kuwa wabunge, KUUWEKA huo ushahidi na vielelezo vyenu hadharani, KUNGEMALIZA kila kitu. PASINGEKUWA na haja tena ya 'Covid 19' kuhangaikia kesi au mawakili uchwala wala kuhitaji ulinzi wa 'Betina' ili kubakia Bungeni. Kinyume chake, Ndugu yangu ENENDA ukatubu ili umrudie Mungu akusamehe upate nguvu ya kushinda majaribu ya shetani. AMEN
 

Sikiliza , watashindwa si kwasababu ya mawakili mzigo Bali kwa sababu haki IPO upande wa Chadema.
 
Ukiona unajiona una haki, na kila unakokwenda hupewi hiyo haki unayodhani unayo, BASI UJUWE HUNA HAKI HIYO
 
Mkuu si ufanye tu fasta hapo law school mwaka mmoja uje usimamie utetezi?
 

Kitendo Cha akina Halima kupewa nafasi ya kujitetea kwenye baraza kuu na kugoma kumewaondolea Haki ya kwenda mahakamani. Seema tu kwa Tanzania sheria hubadilika kwa chadema pekee.
 

Tofautisha conviction na case to answer. Hata Sabaya alikutwa na case to answer lakini hakuwa convicted. Kukutwa na kesi ya kujibu haimaanishi una hatia, Bali Kuna ushahidi dhidi yako unao hitaji kuupinga ili kuthibitisha kutokuwa na hatia.
 
Kitendo Cha akina Halima kupewa nafasi ya kujitetea kwenye baraza kuu na kugoma kumewaondolea Haki ya kwenda mahakamani. Seema tu kwa Tanzania sheria hubadilika kwa chadema pekee.
Mkuu econonist , hapa umesema jambo fulani kubwa sana!, watu wafukuzwe chama kinyume cha sheria, wakate rufaa, siku ya rufaa wanaambia wajitetee wananyamaza!, unajua ni kwa nini walinyamaza na hawakujitetea?
sababu ni moja tuu, heshima na utilii. Silence is an admission of guilty kwasababu Voices From Within: Unaweza usiamini! Aliyetoa A Go ahead kwa Mdee na Wenzake ni Kigogo wa Chadema!. Alikuwepo Ukumbini na Vikaoni! Je, ni nani?
Hata ungekuwa wewe ungefungua mdomo kusema chochote?. One thing is for sure, kati ya hao 19, kuna 5 ni partners wa wajumbe wa CC wanaishi kwa co habitation, wakilala chumba kimoja kitanda kimoja kwenye dhana ya ndoa!, unamini wenzi zao kweli walikuwa hawajui chochote juu ya ukweli wa waliingiaje?. Ila pia Halima ana command respect ya ajabu, aliwezaje kuwafunga modomo wote 18 wasijibu kitu!.
P
 
Subutuuuuu yako, hio voice from within, iite Voice from CCM! Kwa uelewa wako walishindwa? Au Kuna kusigina tu Katiba na Mahakama? Kuna kiburi tu Cha madaraka? Unadhani huu upuuzi unaofanywa na Spika unaweza kufanywa nchi nyingine zenye viongozi wenye akili?? Waza nje ya box
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…