Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa huja na makala za "Kwa Maslahi ya Taifa" Makala ya leo ni The Voices From Within kuwa "Japo Hawakutendewa Haki Ndani ya Chama Chao Chadema Kwa kufukuzwa Kwa kuvuliwa uanachama Kikangroo na CC ya Chadema iliyokaa as a kangaroo court, ikawavua uanachama na baadae kikao cha Baraza Kuu kuyabariki maamuzi yale batili ya Kikangroo ya CC yao. Wakakimbilia mahakamani ili kutafuta haki, na huko Mahakamani kwa mara ya kwanza waligonga mwamba na sasa wamefile kesi nyingine.
Sauti hii "The Voices From Within" imeniambia " Safari hii huko Mahakamani pia Watashindwa Tena!" Sababu ni Kuwatumia Mawakili ambao ni mawakili tuu. Kuna mawakili na mawakili bora. Hii kesi ilihitaji Mawakili Bora wa calbre ya Murtaza Lakha. Jee kwenye safu ya mawakili wetu Tanzania, Jee tuna Mawakili wa Calibre ya Murtaza Lakha?. Kama wapo, please Jitokezeni Kusaidia ili kuepusha hukumu ya karma kuwashukia wahusika wa kadhia hii.
Mtu ukikosa haki kwenye Taasisi yako, ukakimbilia mahakamani, ili upate haki, ukakosa haki mahakamani, jee uende wapi baada ya hapo?.
Kitachobaki ni kitu kimoja tuu kumuachia Mungu ambaye ndiye pekee hutoa hukumu za haki kupitia kitu kinachoitwa karma
"The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!
Leo mchana huu, nilikuwa napitia bandiko fulani, mara nikaisikia sauti, "the voices from within" ikinieleza kuwa japo wamefile upya kesi, lakini Watashindwa tena and this time it will be fatal, hivyo uamuzi hautakuwa struck out kama mwanzo, this time the case will be dismissed entirely on its totality and kila mmoja will bear his own costs!.
The voices from within, huwa haitoi sababu, lakini kwenye suala hili mimi nazijua sababu ambazo ni just some simple logic, wanawatumia mawakili wenye uwezo duni!. Sasa kabla hata hiyo kesi mpya haijapangiwa siku ya kusikilizwa, natoa wito kwa manguli wa sheria, hata kama hawajawa contracted, wajitokeze wajitolee kuwasaidia hawa wadada, ili watendewe haki.
Kwa jinsi nilivyoisoma ile hukumu, kusema ukweli wanawatumia mawakili wenye uwezo mdogo au wa wastani sana kiasi kwamba kuna baadhi ya makosa ni silly mistakes, hivyo mtu aliyefanya silly mistakes kama zile, hata akirejebisha makosa na ku file tena, I doubt kama atakuwa na uwezo wa kuargue kesi writs kama za
habeas corpus, mandamus, prohibition, quo warranto and certiorari, sio kesi za kumpa tuu wakili yoyote ili mradi ni wakili, hizi zinahitaji kuwa handled na mawakili mawakili kweli ambao ni mawakili bora na sio hawa ma bora wakili wanaofile kesi kwa makosa ya kijinga kabisa na kupeleka mahakama ku struck out!. Leo mpaka nimemkumbuka Wakili Murtaza Lakha.
Kwa vile mimi ni mtu wa mastori hivyo naomba kuikatiza kwanza hii mada, nianze na mastory mastory ya Pasco Mayalla, halafu nije kumrudia Wakili Murtaza Lakha kisha ndio ni drive home hoja yangu. Hivyo kama wewe sio mtu wa mastori mastori, ishia hapa halafu rukia kule chini
Sasa ndio narejea baada ya mastory mastory ya Pasco Mayalla.
As days go by nikiangalia mienendo ya baadhi ya kesi, nimemkumbuka sana wakili Murtaza Lakha, nimejiridhisha hata fani ya sheria nayo imevamiwa, kila mtu mwenye LL.B, anaweza kuwa wakili.
Japo kila mtu mwenye LL.B anaweza kuwa wakili, na fani ya uwakili imevamiwa, ili kuwa wakili mzuri, zaidi ya kuwa admitted kwenye Bar, lazima pia uwe na uwezo fulani na kipawa fulani.
Kwa haya yanayoendekea mahakamani sasa, nimemkumbuka sana wakili Murtaza Lakha alikuwa ni wakili mzuri, kama sio Murtaza Lakha, Mzee wangu asingetoka!.
Ile sauti ilioniambia Watashindwa tena kesi sababu ya kuwatumia mawakili ili mradi ni mawakili tuu, badala ya kuwatumia mawakili bora, wao wanawatumia na bora wakili!.
Kwa vile mhusika mkuu wa kesi hiyo na yeye pia ni mwasheria, nilitaraji kwa vile Zitto Kabwe na yeye pia aliwahi kutimuliwa na chama kile kile kwa mtindo ule ule wa a Kangaroo Court, Zitto alifungua kesi hivyo hivyo na kesi yake ilitupwa katika hatua za awali, hivyo Bi dada alipoamua kufungua kesi hii ilipofunguliwa tulitaraji wangewatumia mawakili manguli wa sheria na sio wakili tuu alimradi ni wakili.
Hata kwa majaji wetu, niliwahi kusema kitu kuhusu utoaji haki na uwezo wa baadhi ya majaji
Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?
Kitendo tuu cha shauri kuwa struck of fatal procedural improperity ni uthibitisho tosha wa mawakili wenye uwezo wa wastani?.
Natoa wito kwa manguli wa sheria wajitokeze wajitolee kuwasaidia hawa wadada ili watendewe haki, lengo la kuwasaidia watendewe haki sio tuu ili kuwatendea haki hawa Wabunge 19 bali kuiepuka adhabu ya karma itakayo itandika chama chao na viongozi wake, kufuatia the consequences of karma ya Zitto kwa chama hicho na viongozi wake, wasipotendewa haki, the karma consequences will be bad, big and devastating!.
Paskali