The Watchers: Salamu Toka ICC..."Tread Careful"

The Watchers: Salamu Toka ICC..."Tread Careful"

Kabla ICC haijaamua kumuindict mtu pale ushahidi wa kutosha upo wa vitendilo vya uhalifu inayoa nafasi kwanza kwa vyombo vya ndani kushughulikia. Mkutano wa Naibu Mwendesha Mashtaka wa ICC ulikuwa ni kutoa nafasi kwa serikali kuelezea nini kinafanyika kuwawajibisha wote waliohusika na mauaji na uhalifu dhidi ya ubinadamu uliofanyika October 29th.

Serikali inatakiwa itoe taarifa ya ni chombo gani cha ndani kinashughulikia kuleta mashtaka juu ya wahusika. Jibu la serikali ni Tume ya Chande. ICC wanatakiwa kuamua kama tume hiyo inakidhi viwango vya kimataifa kutokana na Mkataba wa Roma kuhusiana na uchunguzi na mashtaka ya uhalifu.

Kama ICC ikiona tume hiyo haikidhi viwango hivyo ni LAZIMA ilete mashtaka dhidi ya wahusika. Kama Samia baada ya kuapishwa tu angeonesha kushtushwa na matukio na mara moja kuanza kuwawajibisha watuhumiwa nanhivyo kujitenga nao angeweza kukwepa kuhusishwa. Tunajua alichofanya na anachoendelea kufanya.

mimi siyo mwanasheria, lkn kwa uelewa wangu raisi ndiye mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, hivyo wakati mauaji yanafanyika kulikuwa na mkuu ambaye anatoa command, majeshi hayawezi kamwe kuanza tu kushoot to kill watu bila ya kupata amri ktk kwa mkuu wao na huyo mkuu alikuwa na uwezo wa kutoa tu amri kusitisha mauaji, isitoshe raisi mwenyewe alitoka public na kuhutubia dunia nzima na kusema nguvu iliyotumika iliendana na hali iliyokuwepo hivyo yeye mwenyewe emeji-implicate kuhusika sasa watoe (icc) nafasi kwa wahusika washughulikiwe ndani ya nchi ni nani amshughulikie mkuu wa vyombo na ulinzi na usalama ndani ya nchi? na kama kungekuwa na huo uwezekano tusingewahitaji icc na international community in the first place ...
 
mimi siyo mwanasheria, lkn kwa uelewa wangu raisi ndiye mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, hivyo wakati mauaji yanafanyika kulikuwa na mkuu ambaye anatoa command majeshi hayawezi kamwe kuanza tu kushoot to kill watu bila ya kupata amri ktk kwa mkuu wao na huyo mkuu alikuwa na uwezo wa kutoa tu amri kusitisha mauaji, sasa watoe (icc) nafasi kwa wahusika washughulikiwe ndani ya nchi ni nani amshughulikie mkuu wa vyombo na ulinzi na usalama ndani ya nchi? kama kungekuwa na huo uwezekano tusingewahitaji icc na intzernational community in the first place ...
Kwa mfumo wetu ni Bunge tu linaweza kumwajibisha Rais siyo mahakama.
 
kwa vyombo vya ndani kushughulikia. Mkutano wa Naibu Mwendesha Mashtaka wa ICC ulikuwa ni kutoa nafasi kwa serikali kuelezea nini kinafanyika kuwawajibisha wote waliohusika na mauaji na uhalifu dhidi ya ubinadamu uliofanyika October 29th.
Kama hivi ndivyo; kuwa utaratibu ni huo wa wahalifu kufanya juhudi za kujisafisha kabla ya kufikishwa madarakani; basi hapo hakuna kesi.

WaTanzania watafute tu njia zao za kupata haki.

Mhalifu apewe fursa ya kujirekebisha kwa uhalifu aliowafanyia watu, nani atashindwa kufanya hata maigizo asionekane kuwa juhudi zinafanyika? Si ndiyo hizo za Tume Teuli ya Jaji Chande? Kwani wanafanya kazi gani hawa kama siyo kusafisha uhalifu wa waliowapa hiyo kazi.

Habari za "maridhiano" kila leo inazungumziwa, na maridhiano ni hayo wanatakayoyaongoza wahalifu wenyewe.
Hapo kutakuwepo na maridhiano?
 
Kama ICC ikiona tume hiyo haikidhi viwango hivyo ni LAZIMA ilete mashtaka dhidi ya wahusika. Kama Samia baada ya kuapishwa tu angeonesha kushtushwa na matukio na mara moja kuanza kuwawajibisha watuhumiwa nanhivyo kujitenga nao angeweza kukwepa kuhusishwa. Tunajua alichofanya na anachoendelea kufanya
Nashukuru umemaliza na huo mstari wa mwisho.

Bila Samia kuwa mhusika mkuu, pasingetokea yaliyotokea Oktoba 29 na kuendelea; na wala yote yaliyotangulia kabla ya hapo yasingetokea; kama watu kutekwa hovyo hovyo na kuuliwa.
 
mimi siyo mwanasheria, lkn kwa uelewa wangu raisi ndiye mkuu wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, hivyo wakati mauaji yanafanyika kulikuwa na mkuu ambaye anatoa command majeshi hayawezi kamwe kuanza tu kushoot to kill watu bila ya kupata amri ktk kwa mkuu wao na huyo mkuu alikuwa na uwezo wa kutoa tu amri kusitisha mauaji, isitoshe raisi mwenyewe alitoka public na kuhutubia dunia nzima na kusema nguvu iliyotumika iliendana na hali iliyokuwepo hivyo yeye mwenyewe emeji-implicate kuhusika sasa watoe (icc) nafasi kwa wahusika washughulikiwe ndani ya nchi ni nani amshughulikie mkuu wa vyombo na ulinzi na usalama ndani ya nchi? na kama kungekuwa na huo uwezekano tusingewahitaji icc na international community in the first place ...
Samia alitaka kutoa ujumbe kwa waTanzania wote wasithubutu kupinga nia yake ya kubaki madarakani kwa njia yoyote ile.
Aliruhusu waTanzania wauliwe; siyo wadhibitiwe ili kuonyesha mfano na kutia woga; akiwa na matumaini kwamba baada ya mauaji hayo hakuna yeyote atakayethubutu tena kuhoji lolote juu ya utawala wake.

Alitumia nguvu kubwa kabisa, ya kuua kwa lengo la kuzima na kuogopesha watakaokuwa bado wanataka kuhoji..

Sasa kaua, zaidi hata ya kiasi cha kuogopesha watu. Museveni huua waganda na kuwatia woga, na kila baada ya mauaji hakuna yeyote ambaye huthubutu kuuliza chochote. Samia kajifunza na kutumia mfano ambao haukukaa vizuri hapa Tanzania. Kasahau kuwa yeye ni Samia, na wala hafanani kabisa na Museveni; kama ilivyo tofauti kwa waTanzania na waganda.
 
Kama ICC ikiona tume hiyo haikidhi viwango hivyo ni LAZIMA ilete mashtaka dhidi ya wahusika. Kama Samia baada ya kuapishwa tu angeonesha kushtushwa na matukio na mara moja kuanza kuwawajibisha watuhumiwa nanhivyo kujitenga nao angeweza kukwepa kuhusishwa. Tunajua alichofanya na anachoendelea kufanya.
Tume iliulizwa kuhusu 'conflict of interest'' nyingi na mojawapo ni ya Mjumbe Tax. Kwamba ni mtu wa Chama na alikuwa waziri wa ulinzi wakati wa machafuko. Nilitegemea Jaji Chande angeliona hilo swali kama ''heads up'' akapuuzia. Impartiality inaangaliwa kuliko jambo jingine katika matukio kama haya

Pili, kauli za viongozi zina wa implicate explicitly and implicitly. Kwa mfano, Rais alitamka nguvu iliyotumika ilikuwa na uwiano na tukio. Tukio lilihusisha vikosi vya ulinzi na usalama ambavyo mkuu wake ni Rais!!!
Kuna viongozi walisema zipo Bilioni 5 zilizoletwa. Zipo kauli za Vijana kutoka Kenya n.k.

Maana yake ni kwamba Tume ya Chande ipo njia panda! Tume ya Kijaji lipaswa kuundwa!
 
Lakini, si wamekwenda hadi Vatican, mkuu 'Mpwimbe'; hatujui hadi sasa wamewasilisha taarifa gani huko; pengine wakitarajia kuwabana hao TEC hapa nyumbani.

Ni sahihi kwa hao wanasheria wa Madrid, na hiyo NGO walivyofanya kwa niaba yetu; lakinii hili haliwezi kutupa matumaini makubwa sisi waTanzania.
Wahusika ni sisi, tunao wajibu wa kushiriki karibu zaidi katika swala linalotuhusu sisi; kwa sababu ni sisi tulioumia na tunaendelea kuumia.
Hakuna chochote cha maana wanaweza kuwasilisha huko.

Unajua UKWELI ni UKWELI tu, hata ukisemwa na kitoto cha miaka 2.

Kupingana na ukweli ni jambo gumu, ambalo Kombo hana akili hiyo wala Kabudi.

Halafu wameshateka watu, ikiwemo mapadre na wengime kutaka kuwaua. Unadhani huyo Papa hana hizo taarifa???
 
Back
Top Bottom