The Zanzibar political paradox: Mapinduzi sasa yamekosa mashiko?

The Zanzibar political paradox: Mapinduzi sasa yamekosa mashiko?

Wanyarwanda wangekuwa na akili kama zako saa hizi wangekuwa bado wanafukua mafuvu kwa kutafuta History
Mkuu an un informed mind like yours is rich for manipulations.
Kama huna utajiri wa ufahamu heri ukae kimya tu, Zanzibar huijui na wala hujui kwamba ukienda huko kwanza utabaguliwa kidini na pili kwa ulivyo tu wewe kama mbara utakuwa si lolote.
Sasa ninyi mliopewa ubwabwa badala ya ndizi za halale za kwenu mnaimba kama hamna akili nzuri kwa kitu msicho kifahamu juu ya Zenj.
Mi nimekaa huko 2yrs, and I know wat I am talking about, weye piga porojo ukifikiri unajua kumbe kila mtu anaona kichwa ni kitupu.
Zanzibar na Rwanda wapi na wapi?
 
Simji Trump ni mdudu gani, sasa wewe unayemsoma na huna mbeke wala nyuma ni kikaragosi tu cha kufagia upenuni mwa wazungu unaowahusudu.
Msome Mandela, Che Guavara, Samora , Mwalimu , Abeid Karume na nitakuelewa.
Huu ndiyo Udhaifu wa ccm maana ikifika mwisho wanataka kushinda kwa nguvu ikionekana hakuna namuna matusi. Haya bwana mkubwa mimi kigalagosi ila hoja zako hazina mashiko hata kama umekaa Zanzibar miaka mia
 
Usijisumbue kubishana na Maso, knywa maji ya bendera huyo.
Mwachie mwaka huu CUF inachukua Zanzibar pamoja na historia yske ya mivutano.
 
Zanzibar ni koloni la tanganyika tokea mwaka 64,huu ni mwaka wa wakoloni kuicha huru zanzibar yenye mamlaka yake.
Mkuu Bobwe2,
kuna aina mbalimbali za makoloni kutokana na sababu za ukoloni wenyewe!, kwenye mkutano wa Berlin wa mwaka 1884, sababu za kutafuta makoloni ilikuwa ni kupata sources of raw materials na markets!, kufuatia Industrial Revolution, sasa tuko kwenye market economy na digital age, masoko ni popote na sio tena territories!.

Kwenye issue ya Zanzibar, ni kama mwanamke mrembo aliyejitongozesha kwa mwanamume rijali!. Baada ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 1964, ili kuizuia Zanzibar kuvamiwa na mabeberu na kurejeshwa kwa Sultani, ni Karume ndio alivuka bahari kuja bara kumuomba Nyerere waungane!, ili Zanzibar ipate ulinzi!, huku ni kujitongozesha!. Nyerere akakubali, mwali tukamposa, na mahari tukalipa, ndoa ya muungano ikafungwa!. Mke tunampenda kwa dhati, tunalisha, tulinamvisha na kumgharimia kwa hali na mali ikiwepo asilimia 4.5% ya pato la misaada la taifa letu!.

Kama kuna mwenye mategemeo kuwa mwaka huu ni mwaka wa wakoloni kukiacha kipenzi chake hiki, kilichojitongozesha chenyewe na kujikabidhi kwa jibwana rijali, wasahau kabisa, kwa sababu, japo mwali alijileta mwenyewe, lakini pia ikatokea huyo bwana rijali Tanganyika, amempenda kwa kweli na dhati ya moyo wake Binti Zanzibari, hadi kukubali, kujifuta utaifa wake wa Tanganyika na kulifuta jina lake zuri la Tanganyika, kwa ajili ya mwanamwali huyu!, hivyo hawezi kukubali kumwachia tuu ajiondokee hivi hivi!.

Wajenga hoja ya Zanzibar kuondoka, wanajenga hoja katika misingi kuwa eti kwa vile mwanamwali huyu alijileta mwenyewe, hivyo akitaka kuondoaka mwenyewe, aachwe tuu ajiondokee kama alivyokuja!. Hoja hii haina mashiko na kamwe mwanamwali huyu hataruhusiwa kujiondokea zake kwa sababu sasa anapendwa kwa dhati!, na ni kufuatia upendo huu, ndio maana hata aliyeshinda uchaguzi kihalali hapewi, kwa sababu mwenye mke wake, hana uhakika na majaaliwa ya usalama wa ndoa hii, bila kuwa na uhakika na mlinzi mpya wa mwanamwali huyu, hivyo kuamua bora matokeo yafutwe, uchaguzi ufanyike tena, kujihakikishia usalama wa mwanamwali wetu!.
Paskali
 
Maalim Seif anajichosha tu...hata afanye nn Urais hatoupata milele.Ccm itaendelea kutawala kama kawaidah.
 
Usipojua asili ya ugonjwa dawa utakayo toa ni pata potea.
Tatizo liliopo ni ubakaji wa demokrasia unaofanywa na CCM. Utaliondoaje tatizo hili?
Wewe ni mtaalamu wa asili na utatuzi wa matatizo,tusaidie mawazo yako.
Weka uccm wako pembeni, ukuje kama mzalendo, mdomo-krasia na mpinga demokrasia.

Unaondoaje uhuni huu wa ccm wa kubaka demokrasia?

Mazoea ni kusikia Tume za NEC na ZEC zikimtangaza Mgombea wa CCM kila linapofanyika igizo la uchaguzi mkuu kuwa ameshinda, kwa nini mara hii ZEC ilishindwa kumtangaza Shein kuwa ameshinda kura za Urais huko Zanzibar?

Asili ya ubakaji wa demokrasia unatokana na nini? Na vipi litatatuliwa tatizo hili lenye asili yake huko ccm?

Mungu hampendi mnafiki, sema kweli, msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

Hatutafuti asili ya ccm wala Cuf but aliyeshinda apewe nchi hilo ndilo la msingi
Unafikiri Mkapa, Kikwete na Warioba kwenda Ikulu kumpongeza Magu na kumpa salamu za mwaka mpya kunakupa ishara yoyote ya ubakaji wa demokrasia Tanzania kupatiwa ufumbuzi?

CCM imetahadharishwa siku zote kujenga muundo wa Muungano unaokidhi ushirikiano wa nchi mbili wabia kwa haki, wao wanaangalia maslahi ya ccm na uccm tu. Sasa hawana njia ya kutokea isipokuwa kubaka demokrasia. Aibu ya ccm imegeuka kuwa aibu ya Tanzania.

So unfair!

Warioba, ccm mwenzao alipowaambia mbeleni ni mbinde, hii Katiba iliyopo ni uoza, hawakumwamini na badala yake wamemwamini Lukuvi, "Sisi ni kaka mkumbwa, tuna jeshi, tuna polisi, tuna tume za uchaguzi"

Sasa nani katika CCM anaweza kumfunga paka (ubakaji wa demokrasia) kengele?
 
Mtaongea yote lakini muungano utadumu. CCM bara ikishinda LAZIMA CCM kisiwa ishinde pia.
Kuna uhakika gani kuwa CCM inashinda bara?
Au ni zisipotosha zinatoshelezwa tu?
Kwa hisani mwenyekiti wa tume au domo-krasi?

Na bado hakuna mccm anaeona umuhimu wa tume huru ya uchaguzi na Katiba ya wananchi mpaka pale mshikamano, amani na utulivu wa nchi hii utakapoazima ukurasa kutoka nchi jirani?
 
Kuna aina mbalimbali za makoloni kutokana na sababu za ukoloni wenyewe!, kwenye mkutano wa Berlin wa mwaka 1884, sababu za kutafuta makoloni ilikuwa ni kupata source of raw materials na markets! kufuatia Industrial revolution, sasa tuko kwenye market economy na digital age, masoko ni popote na sio tena teritories!.

Kwenye issue ya Zanzibar, ni kama mwanamke mrembo aliyejitongozesha kwa mwanamume rijali!. Baada ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Januari 1964, ili kuizuia Zanzibar kuvamiwa na mabeberu na kuejeshwa kwa Sultani, ni Karume ndio alivuka kuja baa kumuomba Nyerere waungane!, ili Zanzibar ipate ulinzi!, huku ni kujitongozesha!. Nyerere akakubali, mwali tukamposa, na mahari tukalipa, ndoa ya muungano ikafungwa!. Mke tunampenda, tunalisha, tulinamvisha na kumgharimia kwa hali na mali ikiwepo asilimia 4.5% ya pato la taifa!.

Kama kuna mwenye mategemeo kuwa mwaka huu ni mwaka wa wakoloni kukiacha kipenzi chake hiki, kilichojitongoshesha na kujikabidhi, wasahau, kwa sababu sasa Tanganyika ameipenda kweli Zanzibar, hadi kufuta utaifa wake na jina lake kwa ajili ya mwanamwali huyu!.

Japo mwanamwali huyu alijileta mwenyewe, hata akitaka kuondoaka mwenyewe kama alivyokuja, hatarruhusiwa kwa sababu sasa anapendwa!, na ndio maana hata aliyeshinda uchaguzi kihalali hapewi, kwa sababu mwenye mke, hana uhakika na majaaliwa ya usalama wa ndoa hii!.
Pasco

Mhhhh maneno makali kaka Pasco na ya kutia UCHUNGU kabisa !!!!!
 
Ni mtazamo hasi katika suala la muungano wa Tanganyika na Zanzibar!
Ni kweli kabisa mojawapo ya madhumuni ya muungano ni kuiondoa Zanzibar katika lindi la machafuko na kuipa stability sehemu hii ya ufukwe wa Afrika Masgariki.
Sababu nyingine, tena mwa shinikizo la wakubwa, ni kuondoa uwezejano wa Zanzibar kuangukia mikononi mwa makomunisti ambao walikuwa wanainyemelea.
Hii ni real politik , na hizo hadithi za mapenzi ni a result of your fertile imagination.

Lakini wazanzibari, kama nilivyoonyesha huko myuma, wana matatizo ya kisiasa yanayotoksna na ukoloni mkongwe wa kiarabu.
Matatizo hayo ndio yaliyopelekea mapinduzi ya 1964.
Misingi ya matatizo hayo hayajatstuliwa hadi leo, na kuna wakati Mwalimu alisema angekuwa na uwezo angevivuta visiwa hivi hadi katikati ya bahari ya hindi!
Kuitazama Zanzibar kwa misingi kwamba Tanganyika insitawala Zanzibar ni kukosea kabisa.
Hawa watu ukiwaachia tu kesho wajitawale, watauana, na hata 1964 itakuwa cha mtoto.

Tatixo kubwa la watu wa Bara ni kutoelewa the fierce divisions in Zanzibar.
 
Last edited:
Tatizo liliopo ni ubakaji wa demokrasia unaofanywa na CCM. Utaliondoaje tatizo hili?
Wewe ni mtaalamu wa asili na utatuzi wa matatizo,tusaidie mawazo yako.
Weka uccm wako pembeni, ukuje kama mzalendo, mdomo-krasia na mpinga demokrasia.

Unaondoaje uhuni huu wa ccm wa kubaka demokrasia?

Mazoea ni kusikia Tume za NEC na ZEC zikimtangaza Mgombea wa CCM kila linapofanyika igizo la uchaguzi mkuu kuwa ameshinda, kwa nini mara hii ZEC ilishindwa kumtangaza Shein kuwa ameshinda kura za Urais huko Zanzibar?

Asili ya ubakaji wa demokrasia unatokana na nini? Na vipi litatatuliwa tatizo hili lenye asili yake huko ccm?

Mungu hampendi mnafiki, sema kweli, msema kweli ni mpenzi wa Mungu.

]
Demokrasia kwa Zanzibar ni kama ngoma ya kuigiza!
Hilo ni upende usipende.
Ndio maana katika mada yangu nimeuliza, je Mapinduzi ya mwaka 1964 yameshapitwa na wakati?
Ukilijibu hilo, na swala lako umelijibu!
 
Ni mtazamo hasi katika suala la muungano wa Tanganyika na Zanzibar!
Ni kweli kabisa mojawapo ya madhumuni ya muungano ni kuiondoa Zanzibar katika lindi la machafuko na kuipa stability sehemu hii ya ufukwe wa Afrika Masgariki.
Sababu nyingine, tena mwa shinikizo la wakubwa, ni kuondoa uwezejano wa Zanzibar kuangukia mikononi mwa makomunisti ambao walikuwa wanainyemelea.
Hii ni real politik , na hizo hadithi za mapenzi ni a result of your fertile imagination.
........
Tatixo kubwa la watu wa Bara ni kutoelewa the fierce divisions in Zanzibar.
Endelea kujidanganya na kuudanganya umma.

Kama Zanzibar ingeangukia mikononi mwa makomunisti ingekuwa tofauti gani na Tanzania(Tanganyika) chini ya siasa ya ujamaa na kugawiana umaskini?

Moyo ni mbara? Je Mzee Moyo haijui historia ya Zanzibar?

Kama ni mbara na anaijua historia ya Zanzibar anasemaje kuhusu siasa za Zanzibar na migogoro hii ya ubakaji wa demokrasia unaofanywa na ccm?
 
Kuna uhakika gani kuwa CCM inashinda bara?
Au ni zisipotosha zinatoshelezwa tu?
Kwa hisani mwenyekiti wa tume au domo-krasi?

Na bado hakuna mccm anaeona umuhimu wa tume huru ya uchaguzi na Katiba ya wananchi mpaka pale mshikamano, amani na utulivu wa nchi hii utakapoazima ukurasa kutoka nchi jirani?
Una maswali mengi lakini nimekwambia ukweli mtupu kwasasa CCM hawana mpango wa kupoteza madaraka Zanzibar. CCM siyo wajinga kama mnavyodhani.
 
Samahani naomba kuuliza, hivi serikari ilitoa kauli gani baada ya yule mama kuongea waziwazi bungeni kwamba " Zanzibar ni nchi ya kimapinduzi na serikari haiwezi kutolewa kwa vijikaratasi vya kura" kama serikari haikutoa tamko au kauli yoyote kuhusiana ma matamshi ya yule mama basi haina haja ya maalimu Seif kuendelea na vikao wakati msimamo wa serikari na ccm unajurikana wazi kuwa Zanzibar ni ya ccm na kamwe CUF hawapa pata kitu!
 
Back
Top Bottom