Thea Ntara ahoji kuhusu Sheria Mpya ya Umri wa Ndoa ili uanzie miaka 18

Thea Ntara ahoji kuhusu Sheria Mpya ya Umri wa Ndoa ili uanzie miaka 18

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma (CCM), Mhe. Dkt. Thea Medard Ntara amehoji “Suala hili lina muda mrefu sana na Watoto wanazidi kunyanyasika kwa kuolewa na umri mdogo, Je, Serikali imejiwekea muda gani wa kufanya mabadiliko ya sheria!?, pia hamuoni haja ya kusitisha maoni ya Wadau kwasababu suala lipo wazi na Wadau wengi ni haohao wanaopenda kuoa Watoto wadogo?”

Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imesema imekamilisha kukusanya maoni na mapendekezo na sasa ipo tayari kupeleka muswada wa mabadiliko ya sheria ya ndoa 1971 katika Bunge hili la Bajeti linaloendelea, ili kuweka umri wa miaka 18 kama umri wa chini wa kuolewa na kuoa.

Akijibu swali hilo Ndumbaro amesema “Baada ya Mahakama ya Rufani kutoa maamuzi kwamba Serikali ibadilishe umri wa chini wa Mtoto kuoa au kuolewa, Serikali ilileta mapendekezo hapa Bungeni, Bunge likaagiza Serikali ikachukue maoni zaidi kwa Wadau mbalimbali.

“Mh.Spika maelekezo hayo tumeyatekeleza na tumeyakamilisha na tupo tayari kuja mbele za Bunge kushare maoni hayo pamoja na mapendekezo yaliyoko mezani, tupo tayari kuleta muswada”

Kwa mujibu wa sheria ya ndoa inayotumika sasa ya mwaka 1971 (kifungu namba 13), Mtoto wa kike anaweza kuolewa kuanzia umri wa 14 kwa ridhaa ya Mahakama na kifungu namba 17 kinasema anaweza kuolewa kwa miaka 15 kwa ridhaa ya Wazazi lakini sheria hiyohiyo inasema Mtoto wa kiume ananza kuoa kuanzia umri wa miaka 18.

WhatsApp Image 2023-04-20 at 18.52.38(2).jpeg
WhatsApp Image 2023-04-20 at 18.52.39(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-04-20 at 18.52.39.jpeg
WhatsApp Image 2023-04-20 at 18.52.39(4).jpeg
 
Back
Top Bottom