Aga Khan haihudumii wa vipato vya chini kumuona specialist wa dental ni zaidi ya TZS 170,000 per single visit wananchi wangapi wanaweza mudu hiyo gharama?
Hata hiyo ruzuku isingetosha halafu elewa aga khan haikuanzishwa ili kuhudumia maskini hamna issue za charity pale ni biashara ile kama ilivyo saifee, tmj, hindumandal na regency sasa ushawahi kusikia saifee, tmj au regency wanaombwa na serikali watoe huduma pungufu ya bei then wapewe ruzuku?
Unafikiri Aga Khan hata wangeombwa wangekubali? unafikiri Aga khan wanapenda kuhudumia wagonjwa hohe hahe tena wengi ka nyuki? ile ni hospital ya wanaojimudu kichumi ni ya wachache ile huwezi linganisha na KCMC au Bugando inayohudumia mpaka mwananchi maskini wa kutupwa hohehahe wa kazuramimba.
KCMC, Bugando lengo ni kuhudumia maskini kabisaa na kuna sadaka kibao za watu mle na ndiyo maana zilianzishwa ilikuwa ni watu walitoa sadaka zao kuwasaidia wengine.
Aga Khan ni pure business na ni kwa ajili ya wachache
Infact vitu vya Aga Khan ni kwa ajili ya wachache na wenye hela na hasa jamii yao na sio akina pangu pakavu. Akina pangu pakavu wao watibiwe za kanisa na serikalini.