dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,502
- 3,483
Waziri huyo wa zamani aliyehamia Chadema mwaka 2010 akitokea CCM, alifariki dunia Jumatano Februari 10, 2021 katika hospitali ya Mloganzila alikokuwa akipatiwa matibabu.
Akisoma wasifu marehemu leo, Thomas amesema baba yake alikuwa akisumbuliwa na tatizo la changamoto ya kupumua na alipata matibabu mbalimbali.
"Februari 2, 2021 baba alizidiwa na kupelekwa hospitali ya Regency lakini hakupata kitanda tukashauriwa tumpeleke hospitali ya Mloganzila na kupokelewa kwenye kitengo cha dharura," amesema Thomas.
Amesema Februari 9, 2021 baba yake aliyewahi kuwa mbunge wa Muhambwe alizidiwa na kuhamishiwa chumba cha uangalizi maalum (ICU) hadi umauti ulipomkuta Februari 10,2021.
Ntagazwa amewahi kuwa naibu waziri wa fedha, ujenzi na uchukuzi, ardhi na waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi
Zaidi, soma:
TANZIA - Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini CHADEMA, Arcado Ntagazwa afariki dunia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo, kwa masikitiko makubwa kinatangaza kifo cha Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chama, Mhe. Dennis Arcado Ntagazwa, kilichotokea asubuhi, Jumatano, Februari 10, mwaka huu katika Hospitali ya Mlonganzila, alikokuwa amelazwa kwa matibabu. Zaidi. soma: Thomas...