Yani mkuu kuna baadhi ya vitu sielewi hata unataka nifanyaje? Ishu ya messi main point ni kuhusu kama anastahili kuwa G.O.A.T je ntajuaje ukweli bila comparison na wachezaji wengine ambao naona wanadeserve kuwa ma goat
Mda mwingine shida huwa ni mtazamo tu pengine mawazo yako yamekariri aina fulani tu ya uchambuzi
Anyway nmekuelewa
Nazungumzia relevance ya mifano.
Ulimzungumzia Messi kama GOAT, then ukaweka mfano wa magoli ya msimu huu peke yake. GOAT - of all time, Messi amevunja records ngapi za ufungaji? Kwa nini hukuzizungumzia?
Messi amewahi kuchukua UEFA ngapi? Na hizo UEFA zote alichukua kwa kukutana na timu ndogo?
Hao kina Maradona na Pele, wamechukua makombe yote waliyoshindania? Hawakuwahi kufungwa au kupoteza makombe?
Brazil iliyochukua mwaka 1958 Pele akiwemo, unadhani asingekuwemo ingeshindwa kuchukua? Unajua kama 1970 Brazil alichukua huku Pele akiwa amecheza mechi chache na akaumia, hivyo sehemu kubwa timu ilicheza bila yeye? Mpira ni team work, hata uwe bora vipi huwezi kufanya peke yako, unahitaji kuwa na wachezaji wazuri kuchukua ubingwa.
Messi ni FIFA Player (Balon D'or) mara 6, ambayo ni World Record, lakini kwa kujua kwamba hii itampa edge umeiondoa kwenye vigezo vyako vya kumpima mchezaji.
Naomba nisijikite kwa Pele, twende na Maradona.
Ukiacha kombe la dunia, amechukua domestic cups ngapi, UEFA ngapi, Best Player ngapi kwa level ya FIFA, amekuwa mfungaji bora mara ngapi, ana career goals ngapi, assists ngapi.
Na swala la kwamba Messi aende Newcastle, hili ni utetezi wa kizembe kabisa.
Hapa ninacholalamikia ni merits za mifano unayoitumia kutetea arguments zako unachagua weak points kufanya justification ya point zako.