Mwl. Dr Julius Kambarage Nyerere aliyemuingiza chaka la Ujamaa ni Wazanzibari waliokuwa wamesomea uhanaharakati Cuba,East Germany, Soviet, Yugoslavia n.k
Mmoja wao ni Profesa Abdullah Babu waziri wa Uchumi na mipango.
Pili muungano na Zanzibar,wao walifungua ubalonzi wa Ujerumani Mashariki wakati Tanganyika tulikuwa na Ujerumani Magharibi.
Mara baada ya Tanganyika kupata uhuru the mighty West Germany ilikuja kwa nia mmoja kuijenga Tanganyika kiuchumi,viwanda,Elimu iwe mfano wa kuigwa duniani.Mjerumani alikuuja kwa mbwembwe tena akitaka kumuonyesha Mwingereza kuwa hawakufanya lolote kwa miaka 70.
Mara huko Zanzibar nayo ikafungua ubalozi na East Germany.mbaya wa West Germany.
Mbabe West Germany akamtaka Raisi Nyerere afunge ubalozi wa East Germany mara mmoja. Nyerere akawajibu wasimchagulie rafiki.
West Germany ikafuga ubalozi Dar ndio hivyo Mjerumani akatutosa mmoja kwa mmoja.
Karata ya pili Nyerere aliwakimbilia Israel wahimarishe vyama vya Ushirika,kilimo cha kisasa kwa peasants. Kuanzisha Jeshi la kujenga Taifa .
Cooperative Unions zikashahimili,Mashamba darasa ya kilimo yakafunguliwa,ukakamavu wa kujenga utaifa kwa wasomi kupitia JKT ukatamalaki.
Lakini 1967 six days war kati ya Israel na Nchi za Misri, Jordan na Syria,Tanzania ikavunja uhusiano na Israel.
Nyerere karata ya tatu akiambatana na Abdullah Babu kwenda China ya Mao kutafuta ufadhili wa kujenga reli ya Tazara na mengine yakafuata ndio ikazaliwa Azimio la Arusha ambalo ndio siasa ya ujamaa na kujitegemea.