Kim Jong Jr
JF-Expert Member
- Mar 15, 2014
- 11,074
- 20,608
Ifio
Hii mada ndio nimeamini kweli hii nchi watu uwezo wa kufikiri ni mdogo sana,huyo Mzungu ni Mpumbavu kama wanaomuunga mkono walivyo Wapumbavu zaidi yake,
Unapomzungumzia Nyerere lazima Akili itulie sio anaropoka ropoka kama kuna kitu kimeingia sehemu za Siri,
Swali la kwanza la kujiuliza kama Great Thinkers mnavyojiita humu ndani,nini maana ya Uhuru kwa wakati ule kipindi watu weusi wametoka kunyanyaswa, kufanywa watumwa na kila baya kutoka kwa hao mabwana zenu weupe?
Kwann tulipigania Uhuru?
Nyerere anakabidhiwa nchi tulikuwa na wataalamu wangapi wazalendo wa kuleta hayo maendeleo ya haraka haraka?
Kwanini tulikuja na Azimio La Arusha?
Mmesoma au kusikiliza hotuba ya Nyerere ya miaka 10 ya kujitawqla tangu nchi ilipopata Uhuru maendeleo ambayo tuliweza kupiga kuzidi miaka ya hao mbwa weupe waliyotutawala?
Anguko la jumuia ya Afrika mashariki?
Vikwazo vya kiuchumi hasa upatikanaji wa vipuri katika mitambo ya viwanda vyetu tulivyokuwa tumeanza kuanzisha hao mbwa kutotupa kwa wakati ili viwanda vife?
Kupanda kwa bei ya Mafuta miaka ya 70s kulikopelekea mtikisiko wa uchumi karibu Dunia nzima je?
Vita vya Uganda na Ukame uliokuja baadae?
Nyerere tunamuheshimu kama kiongozi aliyejharibu kujenga Misingi ya hii nchi licha ya changamoto zilizokuwepo kipindi hiko,bila ya Nyerere sisi tuliopo kwenye sekta ya Madini tusingeweza kupata Leseni za umiliki wa Uchimbaji wa Dhahabu au hata kumiliki Ardhi pengine,
Huko nchini China raisi wa kwanza Mao anaheshimika sio sababu ya kujenga Fly Over au Bullet Trains,watu wengi walikufa chini yake ila yeye alipigania China kwanza na maendeleo ya mtu mmoja mmoja baadae,Deng Xiaoping kaleta mabadiliko ila misingi ya Mao unafanya kazi mpaka leo.
Nchi haijengwi na mtu mmoja na ndio maana alitoka madarakani akawaachia wengine,lakini mpaka leo watu wapumbavu bado mnalaumu.
Swali la kujiuliza kabla hujamlaumu Nyerere wewe binafsi umefanya nini kuisaidia hii nchi?
Zidumu Fikra Za Mwalimu!