Fafanua raia anategemea serikali kwa lipi?Kufa kwa sekta binafsi, utegemezi wa raia kwa serikali kuu kwa karibia kila kitu, siasa za mfumo wa chama kimoja kisichowajibika ipasavyo kuleta maendeleo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Fafanua raia anategemea serikali kwa lipi?Kufa kwa sekta binafsi, utegemezi wa raia kwa serikali kuu kwa karibia kila kitu, siasa za mfumo wa chama kimoja kisichowajibika ipasavyo kuleta maendeleo.
Hujawahi kusikia watu wanalalamika kwa waziri au hata Rais shule ya kijijini kwao haina madawati au matundu ya choo?? Halafu shule yenyewe unakuta iko sehemu wanazalisha mbao!Fafanua raia anategemea serikali kwa lipi?
Na akitokea mtu akataka kujenga hiyo shule,kununua madawati na kujenga vyoo kwa gharama zake na kwa kutumia michango ya wanainchi wazalendo, basi mkurugezi na watendaji wa halimashauri,diwani,mbunge na serikali lazima watamtangazia vita na kumuona ni mhaini na mhujumu uchumi. Mixer kumharibia biashara zake na kumbambikia kesi za kumchafua na kumshusha kiuchumi.Hujawahi kusikia watu wanalalamika kwa waziri au hata Rais shule ya kijijini kwao haina madawati au matundu ya choo?? Halafu shule yenyewe unakuta iko sehemu wanazalisha mbao!
Wanataka Nyerere afufuke akawafanyie yote hayo ili wazidi kuneemeka.Hadi leo hii viongozi wapumbafu wa serikali ya ccm wanagombea viwanja oysterbay wameshindwa kuplani miji mipya iliyo ya kisasa zaidi ya aliyo acha mkoloni...toka mkoloni kaondoka ....Fukwe ya koko beach haijawai kusafishwa ndani ya maji toka mkoloni kuondoka hadi leo, ile fukwe ina ukwokwa chini ya maji na miamba tembezi na kuna ile miba ya wadudu weusi yenye kutoboa ukiogelea hadi leo ...wameshindwa kuuondoa na kumwaga mchanga safi mweupe mpya ndani ya maji na nje ya maji ....wakati ni jambo jema na jepesi tu ....
Kwa msiomjua, Thomas Sowell ni mchumi, mwanahistoria, mwandishi, mkufunzi mwandamizi katika Taasisi ya Hoover nchini Marekani,na kadhalika.
Sowell ni mzaliwa wa Gastonia, NC.
Kwenye hii video, anaizungumzia Tanzania na sera yake ya Ujamaa chini ya Rais Nyerere.
Isikilize/ iangalie halafu tuambie ni wapi kakosea.
I think he is spot on!
View: https://youtu.be/H-tUQmXQ-xk?si=UryuPvS5grgzt_rr
Bila wakoloni mngekuwa mshapotea kwa kuugua UKIMWI,vipindupindu na Malaria.Bila mkoloni mpaka kesho mngekuwa mnakunya machakani.Mkoloni mpaka kesho anaendelea kutujengea mashimo ya choo😂😂😂upendo ulioje huo.Kula ule wewe ila karaha ya mavi yako anaona mtu yupo huko maelfu ya maili Ulaya😣😣😣Ishu sio kuwalaumu to wakoloni, sema wakoloni walifanya yapi mabaya na madhara yake yalikuwa nini. Mimi kwenye suala la uchumi sioni kama wakoloni walifanya mabaya makubwa. Wakoloni pia walihusika kutuharakisha kuwa na mataifa badala ya himaya ndogo ndogo za kikabila za kichifu. Mabaya ilikuwa na kuchukua ardhi kubwa kupitiliza jambo ambalo hata wapigania uhuru waliorithi nchi waliendeleza kwa kuhodhi ardhi kubwa na hawakuwa wanajua jinsi gani wanaweza kurudishia watu ardhi bila kufifisha uzalishaji.
Ukimsoma Deng Xiaoping vizuri ukamsoma na Mao Zedong vizuri ukasoma kipindi ilichopitia China wakati wa Mao hasa miaka kumi ya mwisho wa utawala wake na ukasoma kipindi ilicho pitia China chini ya Deng hasa miaka ya mwanzo ya utawala wake ukarudi kusoma tena ulicho andika utaona umeandika ujinga.Hii mada ndio nimeamini kweli hii nchi watu uwezo wa kufikiri ni mdogo sana,huyo Mzungu ni Mpumbavu kama wanaomuunga mkono walivyo Wapumbavu zaidi yake,
Unapomzungumzia Nyerere lazima Akili itulie sio anaropoka ropoka kama kuna kitu kimeingia sehemu za Siri,
Swali la kwanza la kujiuliza kama Great Thinkers mnavyojiita humu ndani,nini maana ya Uhuru kwa wakati ule kipindi watu weusi wametoka kunyanyaswa, kufanywa watumwa na kila baya kutoka kwa hao mabwana zenu weupe?
Kwann tulipigania Uhuru?
Nyerere anakabidhiwa nchi tulikuwa na wataalamu wangapi wazalendo wa kuleta hayo maendeleo ya haraka haraka?
Kwanini tulikuja na Azimio La Arusha?
Mmesoma au kusikiliza hotuba ya Nyerere ya miaka 10 ya kujitawqla tangu nchi ilipopata Uhuru maendeleo ambayo tuliweza kupiga kuzidi miaka ya hao mbwa weupe waliyotutawala?
Anguko la jumuia ya Afrika mashariki?
Vikwazo vya kiuchumi hasa upatikanaji wa vipuri katika mitambo ya viwanda vyetu tulivyokuwa tumeanza kuanzisha hao mbwa kutotupa kwa wakati ili viwanda vife?
Kupanda kwa bei ya Mafuta miaka ya 70s kulikopelekea mtikisiko wa uchumi karibu Dunia nzima je?
Vita vya Uganda na Ukame uliokuja baadae?
Nyerere tunamuheshimu kama kiongozi aliyejharibu kujenga Misingi ya hii nchi licha ya changamoto zilizokuwepo kipindi hiko,bila ya Nyerere sisi tuliopo kwenye sekta ya Madini tusingeweza kupata Leseni za umiliki wa Uchimbaji wa Dhahabu au hata kumiliki Ardhi pengine,
Huko nchini China raisi wa kwanza Mao anaheshimika sio sababu ya kujenga Fly Over au Bullet Trains,watu wengi walikufa chini yake ila yeye alipigania China kwanza na maendeleo ya mtu mmoja mmoja baadae,Deng Xiaoping kaleta mabadiliko ila misingi ya Mao unafanya kazi mpaka leo.
Nchi haijengwi na mtu mmoja na ndio maana alitoka madarakani akawaachia wengine,lakini mpaka leo watu wapumbavu bado mnalaumu.
Swali la kujiuliza kabla hujamlaumu Nyerere wewe binafsi umefanya nini kuisaidia hii nchi?
Zidumu Fikra Za Mwalimu!
Mwl. Dr Julius Kambarage Nyerere aliyemuingiza chaka la Ujamaa ni Wazanzibari waliokuwa wamesomea uhanaharakati Cuba,East Germany, Soviet, Yugoslavia n.kMalengo yalikuwa mazuri ila matokeo yakaja ndivyo sivyo
Ingawa maendeleo aliyokua anayapigania Mzee Nyerere na Hali ilivyo kwa nchi zilizoiga ubepari toka mwanzo hata hatutofautiani sana, South Africa hiyo hapo mbona nao wamefeli tu
Historia za nchi za Afrika zinasikitisha na kuaibishaMwl. Dr Julius Kambarage Nyerere aliyemuingiza chaka la Ujamaa ni Wazanzibari waliokuwa wamesomea uhanaharakati Cuba,East Germany, Soviet, Yugoslavia n.k
Mmoja wao ni Profesa Abdullah Babu waziri wa Uchumi na mipango.
Pili muungano na Zanzibar,wao walifungua ubalonzi wa Ujerumani Mashariki wakati Tanganyika tulikuwa na Ujerumani Magharibi.
Mara baada ya Tanganyika kupata uhuru the mighty West Germany ilikuja kwa nia mmoja kuijenga Tanganyika kiuchumi,viwanda,Elimu iwe mfano wa kuigwa duniani.Mjerumani alikuuja kwa mbwembwe tena akitaka kumuonyesha Mwingereza kuwa hawakufanya lolote kwa miaka 70.
Mara huko Zanzibar nayo ikafungua ubalozi na East Germany.mbaya wa West Germany.
Mbabe West Germany akamtaka Raisi Nyerere afunge ubalozi wa East Germany mara mmoja. Nyerere akawajibu wasimchagulie rafiki.
West Germany ikafuga ubalozi Dar ndio hivyo Mjerumani akatutosa mmoja kwa mmoja.
Karata yake Nyerere aliwakimbilia Israel wahimarishe vya vya Ushirika,kilimo cha kisasa kwa peasants. Kuanzisha Jeshi la kujenga Taifa Cooperative zikashahimili,Mashamba darasa ya kilimo yakafunguliwa,ukakamavu wa kujenga utaifa kwa wasomi kupitia JKT ukatamalaki.
Lakini 1967 six days war kati ya Israel na Nchi za Misri, Jordan na Syria,Tanzania ikavunja uhusiano na Israel.
Nyerere akajaribu kwenda China ya Mao kutafuta ufadhili wa kujenga reli ya Tazara na mengine yakafuata ndio ikazaliwa Azimio la Arusha ambalo ndio siasa ya ujamaa na kujitegemea.
Kuna makala ya Profesa Babu anasema Western trained Nyerere hakujua kabisa propaganda za nchi za Kikominist katika safari yao ya kwanza kutembelea China anasema alionyeshwa vijiji vya ujamaa viko na nyumba,maji umeme,shule,hospitali, barabara nzuri,maduka.Kumbe ni vya kuigiza tu.Historia za nchi za Afrika zinasikitisha na kuaibisha
Mao mwenyewe alikuwa kashaingia chaka , mamilioni waliokufa kutokana na sera zake tushukuru hatukupitia hayoKwa lugha nyepesi Nyerere was Compromised by Chinese.Alifuata njia nyingine ya siasa za kijamaa alizokuwa hazielewi vizuri.
Ni kweli, Ujamaa wa Nyerere ulikuwa na matokeo mabaya sana kwa Tanzania japo lengo lilikuwa zuri. Hata hivyo umekuwa na faida pia katika suala la umiliki ardhi.
Kuna makala ya Profesa Babu anasema Western trained Nyerere hakujua kabisa propaganda za nchi za Kikominist katika safari yao ya kwanza kutembelea China anasema alionyeshwa vijiji vya ujamaa viko na nyumba,maji umeme,shule,hospitali, barabara nzuri,maduka.Kumbe ni vya kuigiza tu.
Anasema Nyerere alienda amevaa western suit lakini kurudi Tanzania akaja amebatizwa na ki Mao,hakuvaa tena western suit.
Kwa lugha nyepesi Nyerere was Compromised by Chinese.Alifuata njia nyingine ya siasa za kijamaa alizokuwa hazielewi vizuri.
Uelewe Jambo moja unapojadili haya mambo.Ujamaa/Ukomunisti ni Kitu kibaya sana, hakuna ubishi juu ya suala hili.
Kufeli kwa nchi nyingi sana za Afrika zaidi sana kumesababishwa na Ubovu wa akili za waAfrika wenyewe (especially for Black Africans countries).
Rais wa zamani wa nchi ya Afrika Kusini enzi za Utawala wa Ubaguzi wa rangi Bw. Pieter W. Botha aliwahi kusema kwamba "Tuliwakataa, tuliwatenga na kuwaengua kabisa Watu weusi katika mchakato wa maendeleo ya nchi na ujenzi wake kwa sababu hawana akili nzuri. Endapo kama tungewajumuisha basi wangetuharibia mambo yetu mazuri yaliyopo Afrika Kusini leo hii."
tafadhali tupatie mfano wa hizo faida zilizopatikana kwenye umiliki wa ardhi, ambao kwa sasa ni utapeli na dhuluma kwa asilimia kubwaNi kweli, Ujamaa wa Nyerere ulikuwa na matokeo mabaya sana kwa Tanzania japo lengo lilikuwa zuri. Hata hivyo umekuwa na faida pia katika suala la umiliki ardhi.
Profesa Babu alikuwa mjamaa haswa akiamini katika Ujamaa wa Kisayansi Mwanaharakati mahili wa Pan Africanism,Kati ya Prof Babu na Mwalimu Nyerere, nani alikuwa mkomunisti kindakindaki?
Uelewe Jambo moja unapojadili haya mambo.
Ujamaa na ukomunisti Ni vitu viwili tofauti.
Kiingereza Socialism na Communism.
Tanzania haijawahi kuwa nchi ya ukomunisti bali Ujamaa.
Kuna nchi nyingi tu duniani hata Ulaya zenye Ujamaa na wajamaa zilizo endelea. Ndani ya Marekani, Germany na kwingineko wapo watu wanachama wa chama cha kijamaa.