Thomas Sowell: Jinsi Ujamaa wa Nyerere ulivyoiharibu Tanzania

Thomas Sowell: Jinsi Ujamaa wa Nyerere ulivyoiharibu Tanzania

Kizazi cha Mwalimu Nyerere katika uongozi wao walikuwa na kazi kubwa ya kuunganisha makabila mbalimbali ili kujenga taifa na wakati huohuo kujenga misingi ya Uchumi,siyo kazi rahisi sana.Lakini Mwalimu Nyerere alijitaidi kujenga taifa lenye umoja na ata kwenye Uchumi alijitaidi kujenga viwanda na kuanzisha mashirika ya umma ambayo Wahuni waliyaua.
Huwa sielewi kusema sera ya ujamaa iliturudisha nyuma, kwani sera ya ubepari imetufikisha wapi, maana naona viwanda tulivyojenga wakati wa ujamaa ndiyo viliuzwa wakati wa sera ya ubepari, which is which!!!
Shida yetu Watanzania ni uvivu, wizi serikalini na uongozi mbovu ndiyo vinaturudisha nyuma!!
Majitu mavivu na majizi ndio hao wanakuja na hoja mufilisi kabisa baada ya kuona hawana cha kuwaambia Watz.

Waafrica UBINAFSI,wizi na kupenda shortcut ndio limeharibu hili bara.
 
Nimezaliwa wakati President Mkapa ni Raisi, hivyo siwezi nikasema nina jua yaliyojiri wakati wa Urais wa Nyerere.

But, kutoka hadithi za Babu na Babaangu, na kutoka vitabuni n.k. Nyerere was the Greatest, still the greatest amongst African and World leaders alike Today.

His intellect and vision were unmatched then and still unmatched Today.

Hata hivyo sihitaji mzungu aje kuniambia mazuri au mabaya yake.

Ushahidi upo wazi leo hii.

Watanzania wanajitambua.
Aisee!
 
Huwa sielewi kusema sera ya ujamaa iliturudisha nyuma, kwani sera ya ubepari imetufikisha wapi?
🫡🫡

Subiria majibu ya kiufundi hapo. Kwanza watahamisha magoli na kisha waseme you know what. Wizi Rushwa, na Ubadhirifu.
 
Mzee Yoda. Kwa fikra zako bila ya kukukwaza ni kama za Sowel, ni biased! hata nikitaja mafanikio yake utajiondoa ufahamu.
Ni vizuri ukaonyesha mafanikio ya Nyerere katika uchumi angalau kuweka rekodi sawa hata kama hatutayakubali.
 
You nailed it man!
Hofu yangu ni kiwango cha akili cha watakaosoma hii comment yako!
Chawa na viroboto hawatamuelewa hapa😀😀😀watz wengi bado wana very low critical and analytical thinking ways.
 
Labda tukuulize ww, ambacho hakufanikiwa kiuchumi ni nn?
Viwanda alivyorithi enzi za ukoloni vilikufa.
Mashamba ya Mkonge, Ngano, Chai na kahawa yalikuwa mahututi wakati anaondoka.
Vyama vya ushirika vilikufa.
Reli alizorithi kutoka kwa wakoloni zilikuwa hoi.
Sekta binafsi ilikuwa kama imekufa tu.
Wakati anaondoka madarakani Tulikuwa masikini wenye madeni tele, uchumi uliodumaa, miondombinu hafifu na huduma duni sana za kijamii.
 
Majitu mavivu na majizi ndio hao wanakuja na hoja mufilisi kabisa baada ya kuona hawana cha kuwaambia Watz.

Waafrica UBINAFSI,wizi na kupenda shortcut ndio limeharibu hili bara.
Huwa uko mwepesi sana kutoa lawama, tena kwa lugha za kikaburu na kibaguzi.

Kama ni kweli unavyojitutumua hapa kwamba una akili, kwanini usituwekee hizo hoja zisizo mufilisi tuone mapovu yako.

Inaelekea ww ndie mvivu hata wa kuleta hoja😂
 
Viwanda alivyorithi enzi za ukoloni vilikufa.

Mashamba ya Mkonge, Ngano, Chai na kahawa yalikuwa mahututi wakati anaondoka.

Reli alizorithi kutoka kwa wakoloni zilikuwa hoi.

Sekta binafsi ilikuwa kama imekufa tu.
Sio kweli hata kidogo, umejaribu lakini. Sekta binafsi ndio nn?

Wazungu? Ndio maaan wamengang'ania PPP?

The truth shall set you free.
Wakati anaondoka madarakani Tulikuwa masikini wenye madeni tele, uchumi uliodumaa, miondombinu hafifu na huduma duni sana za kijamii.
👆Ukilinganisha na wapi?

Ndio unasema hatuna madeni tele comparetively na leo?

Hata hivyo Uchumi kudumaa ndio economics zenyewe hizo.

hata Marekani leo hii Trump analia uchumi wao umedumaa.

Miundombinu hafifu ndio nn? Maana yake sielewei.
 
Ni vizuri ukaonyesha mafanikio ya Nyerere katika uchumi angalau kuweka rekodi sawa hata kama hatutayakubali.
Nimekupata.

Kwa sas naenda kutumikia Taifa. Baadae
 
Kwa msiomjua, Thomas Sowell ni mchumi, mwanahistoria, mwandishi, mkufunzi mwandamizi katika Taasisi ya Hoover nchini Marekani,na kadhalika.

Sowell ni mzaliwa wa Gastonia, NC.

Kwenye hii video, anaizungumzia Tanzania na sera yake ya Ujamaa chini ya Rais Nyerere.

Isikilize/ iangalie halafu tuambie ni wapi kakosea.

I think he is spot on!

View: https://youtu.be/H-tUQmXQ-xk?si=UryuPvS5grgzt_rr

Nyerere aliharibu vipi Tanzania wakati alizuia raslimali zetu za ardhi na madini zibakie zetu?

Nyerere aliharibu vipi Tanzania kwa kufanya tuachane na ukabila nankuwa na lugha moja?

Nyerere aliharibu vipi Tanzania kwa kutusomesha bure hadi Chuo Kikuu??

Tanzania iliyiharibika iko wapi wakati kwa sasa ni moja kati ya nchi 10 zenye uchumi mkubwa Afrika??

Ni upuuzi kumsikiliza mtu aliyezaliwa Amerika Kaskazini aiongelee nchi yetu wakati sisi wenyewe tnaishi na tunaiona ni mzuri
 
Kizazi cha Mwalimu Nyerere katika uongozi wao walikuwa na kazi kubwa ya kuunganisha makabila mbalimbali ili kujenga taifa na wakati huohuo kujenga misingi ya Uchumi,siyo kazi rahisi sana.Lakini Mwalimu Nyerere alijitaidi kujenga taifa lenye umoja na ata kwenye Uchumi alijitaidi kujenga viwanda na kuanzisha mashirika ya umma ambayo Wahuni waliyaua.
Huwa sielewi kusema sera ya ujamaa iliturudisha nyuma, kwani sera ya ubepari imetufikisha wapi, maana naona viwanda tulivyojenga wakati wa ujamaa ndiyo viliuzwa wakati wa sera ya ubepari, which is which!!!
Shida yetu Watanzania ni uvivu, wizi serikalini na uongozi mbovu ndiyo vinaturudisha nyuma!!
Nyerere alifanikiwa kujenga umoja wa kitaifa, kubakiza ardhi kwa raia na pia hakuwa fisadi, swali la msingi ni Je, ilihitaji ujamaa kufanya haya? ilihitaji miaka 20 kufanya haya? Ilihitaji ku sacrifice demokrasia kufanya haya??
 
Kwa mtazamo wangu kinachokosewa ni implementation ya socialism, hautakiwi kuanza nayo bali socialism inabidi iwe the final stage of society:
1. Tunaanza na communism (ujima) ambapo taifa (state) linamiliki kila kitu (hapa naweza kutumia yamkini ya mfalme)

2. Kisha inafuata ubepari (capitalism) ambapo "taifa" lina "privatize" ili wananchi wajigawie keki ya taifa kwa nguvu zao

3. Baada ya msuguano wa kipebari uliosababisha rasiliamali za nchi zikatumika kweli kweli basi Sasa ndio inaingia ujamaa (socialism) maana tayari taifa linakuwa na rasiliamali tosha kwenye mzunguko kutunza wananchi wake

Ukiangalia kwa makini utagundua ujima, ubepari na ujamaa mifumo yote mitatu ni msuguano/uhusiano kati ya taifa (state) na wananchi wake (working class)

Katika Ujima taifa linakuwa kama vile "limeshikilia" rasiliamali kwa niaba ya rasiliamali kazi

Katika ubepari taifa linakabidhi rasiliamali katika mikono ya rasiliamali kazi na katika mfumo huu wanazaliwa mabepari ambao wataiongoza na kuitumikisha rasiliamali kazi hii kuelekea katika malengo Fulani ya kimaendeleo (uchumi kukua)

3. Tukifika katika steji ya ujamaa (socialism) hapa ni kama vile taifa linachukua zao la ubepari na kulitawanya baina ya wananchi/working class/rasiliamali kazi

Kiufupi....... Utaanzaje na ujamaa wakati hata hizo rasiliamali za kugawana hazijatoka ardhini wala kwenye bongo (mawazo) zenu
Well said kiongozi!
 
Tanzania iliyiharibika iko wapi wakati kwa sasa ni moja kati ya nchi 10 zenye uchumi mkubwa Afrika??
GDP kubwa tu sio kitu cha muhimu sana bila kuitafsiri katika GDP per capita, unaweza kuwa na nchi yenye uchumi mkubwa kama Ethiopia lakini ikiwa bado na ufukura mkubwa sana tu.
 
IMG_20250225_084035_325.jpg

Nime attach hiki kitabu kwa Makusudi kabisa.

Nimelithi kwa Babu yangu alikinunua Mwaka 1 April 1969.

Nilitamani sana nipate mawazo yenu ambayo yanaeleweka.

1. Ujamaa ni nini???

2. Ujamaa Ulianzaje Tanzania.

3. Ulihusisha Mambo gani???

4. Mafanikio ya ujamaa yalikuwa ni yapi???

5. Hasara za Ujamaa zilikuwa ni zipi????????

6. Nchi za kijamaa ni zipi???

7. Zimefanikiwa ama zimefeli wapi?????

Watu wengi hapa wamejiandikia tu vitu ambavyo hawavijui.

Mwalimu alisistiza kuwa ameandika hiki kitabu hajakosea sehemu yoyote hata Nukta

MSIONGEE BILA KUWA NA UHAKIKA NA KITU.
 
GDP kubwa tu sio kitu cha muhimu sana bila kuitafsiri katika GDP per capita, unaweza kuwa na nchi yenye uchumi mkubwa kama Ethiopia lakini ikiwa bado na ufukura mkubwa sana tu.
Usihamishe magoli. Hakuna indicator ya uchumi ya hovyo kama GDP per capital. Pengine tumia HDI uniambie Tanzania ina rank vipi
 
Usihamishe magoli. Hakuna indicator ya uchumi ya hovyo kama GDP per capital. Pengine tumia HDI uniambie Tanzania ina rank vipi
Kwa HDI ni ya 167 imepitwa hadi na Rwanda, Uganda na Zimbabwe.
 
You nailed it man!
Hofu yangu ni kiwango cha akili cha watakaosoma hii comment yako!
Mkuu huu mtandao umekuwa wa Kisenge sana,kuna watu wana majina makubwa humu ila ukisoma comment zao kwenye mambo ya msingi kuhusu nchi au Historia yetu unabaki kushika kichwa tu,

Kwa mfano Nyerere aliandika Kitabu cha Tanu Na Raia kuwakumbusha viongozi juu ya wajibu wao katika Taifa hili changa,bado akaja na kauli mbiu ya Uhuru Na Kazi ili watu wajue Uhuru sio kukaa kwenye vibanda vya kahawa na kubishana mambo ya Yesu na Mtume Mohammed nani ni mkweli au Simba na Yanga,
Akabinafsisha na shule za Misheni ili hawa mbwa wanaomtukana leo babu zao wajue hata kusoma na kuandika,akaja na UPE ili kila mtanzania kwanza ajue kusoma na kuandika na wachache waende Elimu ya juu ili kuja kuiokomboa hii nchi kiuchumi,

Mimi nipo Katavi huku,miaka ya 70 huyo mzee alileta Timu ya wataalamu kutoka Urusi kufanya tafiti za kijiolojia kufahamu Assets za Madini tulizokuwa nazo,wale warusi waligundua vitu vya hatari ila inavyosemekana walipotaka kuchimba Mzee alikataa na kusema nataka mpaka wananchi wangu wawe na Elimu ya mambo hayo,mimi nimebahatika kupata Geological Map ya hao warusi,ni hatari yaliyomo na namshukuru Nyerere mpaka naingia kaburini,leo hii mimi namiliki Leseni za Madini ya Dhahabu na Kopa sababu yake.

Wachina wanakimbilia Katavi kuvuna Copper na Gold watu weusi wanabaki kubishana Simba na Yanga au harusi ya Mobeto na msenge mwenzake.

Shida ya watu weusi lipo Kichwani,tunapenda kulalamika bila ya kuja na suluhisho,hata kujaribu tunashindwa na mtu akijaribu ikitokea matokeo hayajakuwa mazuri ndio hapo hapo tunapoonesha kuwa hana Akili wakati wewe mwenye Akili umeshindwa kujaribu chochote.

Fikra Za Mwalimu Zidumu.
 
Siku akiiingia kiongozi mpya Tanzania asiyetokana na CCM/TANU ni lazima tufanye maombi ya toba kwa ajili ya nchi yetu. Nchi hii imeendeshwa kwa uongo na siasa za kinafiki tangu luzaliwa kwake. Hivyo tusahau maendeleo ya kweli chini ya CCM.
 
Back
Top Bottom