Thomas Sowell: Jinsi Ujamaa wa Nyerere ulivyoiharibu Tanzania

Thomas Sowell: Jinsi Ujamaa wa Nyerere ulivyoiharibu Tanzania

Hata kuwafunga wapinzani/ wakosoaji, kuondoa demokrasia, nayo malengo yake yalikuwa mazuri?
Miaka hiyo haya mambo ya demokrasia yalikuwa ni changamoto kila sehemu. Kwanza Kenya kulikuwa na udikteta kuliko Tanzania. Mobutu alikuwa darling wa West, nchi yake iko wapi? Malawi na nchi kibao za Afrika zilizokuwa hazina ujamaa bado zina changamoto... ni Nyerere aliziharibu?
 
Ukomunisti au ujamaa ni mfumo wa kijinga na siku zote lazima ushindwe tu na sababu ziko nyingi sana. Soko huria japo sio perfect lakini ndio kichocheo kikubwa cha ubunifu, uvumbuzi, maendeleo na uhuru wa binadamu kulinganisha na mfumo wowote ule.
Ukomunisti sio Ujamaa mbona unalazimisha sana kuweka correlation?

Africa haijawahi kuondoka kwenye mfumo wa masoko huria, laiti ungefahamu hilo usingekuwa unalazimisha.
 
Mtu aliyeasisi kuua mawazo binafsi, huyu pia ndio aliasisi watanzania kuwa na kile kitabia cha kujifungia utasikia uende nje ya nchi kwanini na maswali ya kipuuzi na msururu wa nyaraka watu wakiomba pasi za kusafiria.

Huyu mtu alishiriki uchaguzi mmoja tu wa kidemokrasia mwaka 1965 baada ya hapo TANU na baadaye CCM ilikuwa ni order of the day siasa iliingia hadi jeshini hadi leo unakutwa wanajeshi wanapewa uRC japo walisema waliondoa siasa jeshini 1993 ila ni kama kiinimacho.

Kwa huyu kuzuia mawazo binafsi ya watu wengine badala yake yeye nchi kutumbukia kwenye dimbwi la umasikini hadi alipoona sasa ameshindwa ndio akajitoa.
 
Miaka hiyo haya mambo ya demokrasia yalikuwa ni changamoto kila sehemu. Kwanza Kenya kulikuwa na udikteta kuliko Tanzania. Mobutu alikuwa darling wa West, nchi yake iko wapi? Malawi na nchi kibao za Afrika zilizokuwa hazina ujamaa bado zina changamoto... ni Nyerere aliziharibu?
Tuangalie nchi kwa muktadha wao,
Wakoloni waliotawala Congo, Angola na Msumbiji hawakuacha mifumo au miondombinu yoyote ya maana ya utawala tofauti na makoloni mengi ya Uingereza.

Ukija upande wa Malawi je utalinganisha potential yetu na Malawi nchi ambayo inategemea kilimo kwa 90% na ni landlocked iliyozungukwa na mataifa yanayozalisha vitu vile vile inayozalisha?
 
Miaka hiyo haya mambo ya demokrasia yalikuwa ni changamoto kila sehemu. Kwanza Kenya kulikuwa na udikteta kuliko Tanzania. Mobutu alikuwa darling wa West, nchi yake iko wapi? Malawi na nchi kibao za Afrika zilizokuwa hazina ujamaa bado zina changamoto... ni Nyerere aliziharibu?
Mkulu, unataka kusema Africa haikuwa na mifumo ya kidemocrasia kabla ya wakoloni kuja na kuharibu mifumo ya kiutawala?

Hata hivyo ni ukweli usiopingika, Nyerere hakuharibu chechote in the context of socio- political, socio Economics and social fabric of Tanzania. It was quite the opposite na ninaweza kusema, Aliimarisha mifumo yetu iliyokuwa teyari ishaanza kulegezwa na itikadi za kimagharibi.
 
Kitu gani Nyerere alifanikiwa katika masuala ya uchumi wa nchi?
 
Ujamaa ulifeli kwasababu haikuwa muda wake, ujamaa unauingiza taratbu taratibu kwa kupitia mfumo wa kibepari (nchi kama Denmark na nyingine za ukanda huo baadhi ya watu hupenda kuziita "capitalist countries with strong social policies)
Ujamaa wa Nyerere ni wa tofauti na nchi za Scandinavia, jina zuri la uchumi wa hizo nchi ni Welfare states. Huo mfumo wao haufanyi matajiri kuwa haramu, hauweki watu katika vijiji vya Ujamaa na pia una kiwango cha juu cha demokrasia duniani. Huo unaitwa Ujamaa kwa sababu serikali inatumia nguvu nyingi sana kuhakikisha watu wote wanapata huduma bora za elimu na afya kwa gharama karibia na bure au bure kabisa.
 
Hii mada ndio nimeamini kweli hii nchi watu uwezo wa kufikiri ni mdogo sana,huyo Mzungu ni Mpumbavu kama wanaomuunga mkono walivyo Wapumbavu zaidi yake,

Unapomzungumzia Nyerere lazima Akili itulie sio anaropoka ropoka kama kuna kitu kimeingia sehemu za Siri,

Swali la kwanza la kujiuliza kama Great Thinkers mnavyojiita humu ndani,nini maana ya Uhuru kwa wakati ule kipindi watu weusi wametoka kunyanyaswa, kufanywa watumwa na kila baya kutoka kwa hao mabwana zenu weupe?

Kwann tulipigania Uhuru?

Nyerere anakabidhiwa nchi tulikuwa na wataalamu wangapi wazalendo wa kuleta hayo maendeleo ya haraka haraka?

Kwanini tulikuja na Azimio La Arusha?

Mmesoma au kusikiliza hotuba ya Nyerere ya miaka 10 ya kujitawqla tangu nchi ilipopata Uhuru maendeleo ambayo tuliweza kupiga kuzidi miaka ya hao mbwa weupe waliyotutawala?

Anguko la jumuia ya Afrika mashariki?

Vikwazo vya kiuchumi hasa upatikanaji wa vipuri katika mitambo ya viwanda vyetu tulivyokuwa tumeanza kuanzisha hao mbwa kutotupa kwa wakati ili viwanda vife?

Kupanda kwa bei ya Mafuta miaka ya 70s kulikopelekea mtikisiko wa uchumi karibu Dunia nzima je?

Vita vya Uganda na Ukame uliokuja baadae?

Nyerere tunamuheshimu kama kiongozi aliyejharibu kujenga Misingi ya hii nchi licha ya changamoto zilizokuwepo kipindi hiko,bila ya Nyerere sisi tuliopo kwenye sekta ya Madini tusingeweza kupata Leseni za umiliki wa Uchimbaji wa Dhahabu au hata kumiliki Ardhi pengine,

Huko nchini China raisi wa kwanza Mao anaheshimika sio sababu ya kujenga Fly Over au Bullet Trains,watu wengi walikufa chini yake ila yeye alipigania China kwanza na maendeleo ya mtu mmoja mmoja baadae,Deng Xiaoping kaleta mabadiliko ila misingi ya Mao unafanya kazi mpaka leo.

Nchi haijengwi na mtu mmoja na ndio maana alitoka madarakani akawaachia wengine,lakini mpaka leo watu wapumbavu bado mnalaumu.

Swali la kujiuliza kabla hujamlaumu Nyerere wewe binafsi umefanya nini kuisaidia hii nchi?

Zidumu Fikra Za Mwalimu!
 
Ujamaa wa Nyerere ilikuwa ni KABURI la Uchumi wa Tanzania. Uchumi wa Tanzania ulikufa na kuzikwa rasmi kwa kupitia Sera na Itikadi mbaya sana za Ujamaa. Azimio la Arusha ndiyo ilihitimisha Safari na Uhai wa Uchumi wa nchi hii ya Tanzania.

Takribani 60% ya Umaskini na Ufukara uliotopea hapa Tanzania umesababishwa na Siasa za Kikomunisti/Ujamaa za Mwl. J.K. Nyerere. Mwalimu aliiga Siasa mbaya sana za Kikomunisti kutoka kwa Marafiki zake wakubwa waliokuwepo enzi hizo kutoka nchini Urusi, China, Cuba, na Korea ya Kaskazini.

Mbaya zaidi Sana, Mwl. Nyerere alifuata na kuiga Itikadi na Falsafa Mbaya zaidi za Siasa za Kikomunisti, Itikadi ya Juche.
Itikadi za Juche ni falsafa kali zaidi za misimamo mikali ya Siasa za Kikomunisti/Ujamaa.

Siasa za Azimio la Arusha kuhusu Ujamaa na Kujitegemea ni Misingi ya Itikadi kali sana ya JUCHE, Yaani Jaju, Jurip and Jiraw.
Una hasira...
Hivi nchi zote masikini hapa Afrika, zilikuwa za kijamaa?
 
Kizazi cha Mwalimu Nyerere katika uongozi wao walikuwa na kazi kubwa ya kuunganisha makabila mbalimbali ili kujenga taifa na wakati huohuo kujenga misingi ya Uchumi,siyo kazi rahisi sana.Lakini Mwalimu Nyerere alijitaidi kujenga taifa lenye umoja na ata kwenye Uchumi alijitaidi kujenga viwanda na kuanzisha mashirika ya umma ambayo Wahuni waliyaua.
Huwa sielewi kusema sera ya ujamaa iliturudisha nyuma, kwani sera ya ubepari imetufikisha wapi, maana naona viwanda tulivyojenga wakati wa ujamaa ndiyo viliuzwa wakati wa sera ya ubepari, which is which!!!
Shida yetu Watanzania ni uvivu, wizi serikalini na uongozi mbovu ndiyo vinaturudisha nyuma!!
 
Kitu gani Nyerere alifanikiwa katika masuala ya uchumi wa nchi?
Mzee Yoda. Kwa fikra zako bila ya kukukwaza ni kama za Sowel, ni biased! hata nikitaja mafanikio yake utajiondoa ufahamu.

Sera za Nyerere, kwa ninanvyojua zilijikita kulingana na muktadha mahasusi wa Tanzania baada ya uhuru. Yaani Kila kitu na zama zake.

hali ya uchumi wa dunia yetu hii leo imebadilika kwa kiasi kikubwa, na kufanya ulinganishi wowote ule wa hali aliyoikuta wa uchumi, na uchumi wa dunia ya sasa ni uduwanzi.

Labda tukuulize ww, ambacho hakufanikiwa kiuchumi ni nn?
 
Lawama kwa nyerere zinasaidia nini kipindi hiki
Pale mfa maji anaposhindwa kuacha kutapatapa.

Hawa mapopoma wanakazi ya kutafuta mchawi of which hakuna siku watampata😀😀😀

Waafrika na wajingawajinga wengine wote acheni lawama.Tatizo la Afrika ni UBINAFSI mijitu ikipewa uongozi inafanya nepotism ,wizi wa mali za umma na kwenda kuficha hela ulaya na Dubai.

Hivi nyerere ndo amewakataza kusambaza gesi nchi nzima ili mpunguze garama za matumizi ya mafuta ya petroli na deasel???

Nyerere na ujamaa wake ndio aliwaelekeza muwe mnanunua maV8 zero kilometer katika nchi maskini???

Ujamaa ndo umewaelekeza msaini mikataba ya kifisadi???

Ujamaa ndio umewaelekeza kutokuwa na upimaji wa ardhi na kuwa na mipango miji inayoeleweka???

Ujamaa ndo umewaelekeza kuwa na uchumi wa Fremu kiasi kwamba mnajenga na masoko ya kichina kama lile la UBUNGO???

Acheni lawama miaka zaidi ya 60 na bado mmeshindwa kulaumu ujinga wenu mnalaumu historia.Haya hizo nchi za kiafrika zilizofata sera za kibepari UCHUMI WAKE UKO WAPI???

📌📌📌Ifike mahali MTU MWEUSI AACHE LAWAMA NA AFANYE KAZI KWA BIDII APUNGUZE KUOMBAOMBA, PIA MTU MWEUSI AKATUBU KWENYE MIZIMU YA MABABU ASAMEHEWE ZAMBI YA UBINAFSI.
 
Hii mada ndio nimeamini kweli hii nchi watu uwezo wa kufikiri ni mdogo sana,huyo Mzungu ni Mpumbavu kama wanaomuunga mkono walivyo Wapumbavu zaidi yake,

Unapomzungumzia Nyerere lazima Akili itulie sio anaropoka ropoka kama kuna kitu kimeingia sehemu za Siri,

Swali la kwanza la kujiuliza kama Great Thinkers mnavyojiita humu ndani,nini maana ya Uhuru kwa wakati ule kipindi watu weusi wametoka kunyanyaswa, kufanywa watumwa na kila baya kutoka kwa hao mabwana zenu weupe?

Kwann tulipigania Uhuru?

Nyerere anakabidhiwa nchi tulikuwa na wataalamu wangapi wazalendo wa kuleta hayo maendeleo ya haraka haraka?

Kwanini tulikuja na Azimio La Arusha?

Mmesoma au kusikiliza hotuba ya Nyerere ya miaka 10 ya kujitawqla tangu nchi ilipopata Uhuru maendeleo ambayo tuliweza kupiga kuzidi miaka ya hao mbwa weupe waliyotutawala?

Anguko la jumuia ya Afrika mashariki?

Vikwazo vya kiuchumi hasa upatikanaji wa vipuri katika mitambo ya viwanda vyetu tulivyokuwa tumeanza kuanzisha hao mbwa kutotupa kwa wakati ili viwanda vife?

Kupanda kwa bei ya Mafuta miaka ya 70s kulikopelekea mtikisiko wa uchumi karibu Dunia nzima je?

Vita vya Uganda na Ukame uliokuja baadae?

Nyerere tunamuheshimu kama kiongozi aliyejharibu kujenga Misingi ya hii nchi licha ya changamoto zilizokuwepo kipindi hiko,bila ya Nyerere sisi tuliopo kwenye sekta ya Madini tusingeweza kupata Leseni za umiliki wa Uchimbaji wa Dhahabu au hata kumiliki Ardhi pengine,

Huko nchini China raisi wa kwanza Mao anaheshimika sio sababu ya kujenga Fly Over au Bullet Trains,watu wengi waliokufa chini yake ila yeye alipigania China kwanza na maendeleo ya mtu mmoja mmoja baadae,Deng Xiaoping kaleta mabadiliko ila misingi ya Mao unafanya kazi mpaka leo.

Nchi haijengwi na mtu mmoja na ndio maana alitoka madarakani akawaachia wengine,lakini mpaka leo watu wapumbavu bado mnalaumu.

Swali la kujiuliza kabla hujamlaumu Nyerere wewe binafsi umefanya nini kuisaidia hii nchi?

Zidumu Fikra Za Mwalimu!
You nailed it man!
Hofu yangu ni kiwango cha akili cha watakaosoma hii comment yako!
 
Back
Top Bottom