PreGE2025 THRDC: Mwanaharakati Boniface Mwangi wa Kenya na Mwanasheria Agather Atuhaire wa Uganda wanashikiliwa na Jeshi La Polisi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeeleza kuwa mwanaharakati kutoka Kenya Boniface Mwangi, pamoja na mwanasheria kutoka Uganda Agather Atuhaire wanashikiliwa katika kituo cha polisi cha Kati Dar es Salaam.

Mwangi na Atuhaire walikuja Tanzania kufuatilia kesi inayomkabili mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Antiphas Lissu, ambapo katika taarifa yake THRDC inaeleza Mwangi anatuhumiwa kuingia nchini kwa kutoa taarifa za uongo.

Chama cha Mawakili Tanganyika, Chama cha Mawakili Afrika Mashariki na THRDC ni sehemu ya mawakili wanaofuatilia suala hili. Mwangi ni mmoja ya wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu mashuhuri zaidi barani Afrika, anafahamika kwa kuwasemea watu wanaoonewa na kukandamizwa haki zao.
 
Wahuni hao waswekwe ndani, Kenya watu wanauliwa na Polisi kwa kupigwa risasi mchana kweupe, juzi hapa wamepigwa risasi watu watano na hakuna yeyote aliyechukuliwa hatua.

Kenya inamatatizo mengi sana yanayohitaji uwepo wa hawa watu ila wapo kimya ni vijana pekeyao wameamua kuikemea serikali yao. Warudi kwao wakashughulikie changamoto zao.
 
Napongeza vyombo vya dola kwa kuwadhibiti hawa wahuni walioshindikana huko kwao. Itakuwa fundisho kwa wahuni wengine... Mama asiwachekee
 
THRDC: Mwanaharakati Boniface Mwangi wa Kenya na Mwanasheria Agather Atuhaire wa Uganda Wanashikiliwa Kituo cha Kati

Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeeleza kuwa mwanaharakati kutoka Kenya Boniface Mwangi, pamoja na mwanasheria kutoka Uganda Agather Atuhaire wanashikiliwa katika kituo cha polisi cha Kati Dar es Salaam.

Mwangi na Atuhaire walikuja Tanzania kufuatilia kesi inayomkabili mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Antiphas Lissu, ambapo katika taarifa yake THRDC inaeleza Mwangi anatuhumiwa kuingia nchini kwa kutoa taarifa za uongo.

Chama cha Mawakili Tanganyika, Chama cha Mawakili Afrika Mashariki na THRDC ni sehemu ya mawakili wanaofuatilia suala hili. Mwangi ni mmoja ya wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu mashuhuri zaidi barani Afrika, anafahamika kwa kuwasemea watu wanaoonewa na kukandamizwa haki zao.
there is no escape routes for criminals and puppets within the country 🐒
 
Ndiyo hekima hiyo. Na kuwashikilia kunawashitua wengi kufatilia hii kesi zaidi kwa mtazamo wa ukakasi Sababu inatengeneza maswali mengi sana.
Je kwao ni kusafi?mbona ardhi nchi kwao inashikiriwa na makabaila kwa 15% wakati waliowengi hawana ardhi kwani wasiwateteee??
 
Back
Top Bottom