THRDC: Ujio wa Kamala Harris ni matokeo ya kuimarika kwa Haki za Kibinadamu na Utawala Bora

kalacha mateo

Senior Member
Joined
Sep 27, 2021
Posts
119
Reaction score
240
Mratibu wa mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa anasema ziara zozote za viongozi wakubwa zinakuwa na manufaa ya kuboresha uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo na kwamba Tanzania imekua kwenye nafasi nzuri.

"Viongozi hawa wakuu wanapopanga ziara zao kwa nchi zinazozungumza utawala bora na haki za binadamu huwa wanaangalia vitu vingi sana ndio watembelee. Hii inaonyesha Tanzania ni ya kidemokrasia na inaheshimu haki za binadamu, ni ishara nzuri kwa namna mambo yanavyoendelea nchini kwamba tupo vizuri inaridhisha." alisema Bwana Onesmo

Aidha alisema ujio wa makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris utafungua fursa za kibiashara baina ya Tanzania na Marekani, ikiwemo vikwazo viliyopo na namna bora ya kuviondoa.

AP22105550438556.jpg
 
Sawa hayo.
Maoni ya....

Onesmo, na yamekaa kujishaua tu.

Onesmo anasemaje kuhusu haki za watu weusi Marekani?

Aibu........

Je na sisi tukiwa tunatembelea makwao huwa tuna uliza haki za watu kama sisi huko zikoje kabla hatujatembelea....Kuna haki kweli?
Kwani wao ndio wanaoelewa haki ni nini na sisi hatujui haki ndio nini?

Waandishi wa habari Tanzania wamejipanga kumuuliza huyo Camara maswali kama hayo? Ya haki za watu weusi huko?

Kuna umuhimu wa kuwa na misimamo thabiti. Tuna maadili yetu, tuyazingatie.
 
Kwani hapa haki za wapinzani zilikuwaje enzi za Lucifer Magufuli?
 
Una lazimisha, halafu uko nje ya mada.

Kama umepotoshwa, usipotoshe wengine.
Nilinena

no hate, sio? Onyesha mfano au ukubali kuwa mna visasi.
 
Umeliweka vizuri binadamu wanaishi mbezi beach, obey na masaki, halafu Watu wako temeke, mbagala, kilingule, riverside, buguruni, chanika
Yeah unaonekana ulikula sana maziwa na samaki ukiwa mtoto. 🤣🤣🤣
 
Nafikiri haki umeielewa ni ipi
Eeh mzee haki ya watu kunyanyaswa na vibopa, mafisadi na wafanyabiashara ambao ndio binadamu hao. Going extra mile unakuta wengine wanaliwa viboga humo humo.
 
Mratibu wa mtandao wa watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa anasema ziara zozote za viongozi wakubwa zinakuwa na manufaa ya kuboresha uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizo na kwamba Tanzania imekua kwenye nafasi nzuri.

"Viongozi hawa wakuu wanapopanga ziara zao kwa nchi zinazozungumza utawala bora na haki za binadamu huwa wanaangalia vitu vingi sana ndio watembelee. Hii inaonyesha Tanzania ni ya kidemokrasia na inaheshimu haki za binadamu, ni ishara nzuri kwa namna mambo yanavyoendelea nchini kwamba tupo vizuri inaridhisha." alisema Bwana Onesmo

Aidha alisema ujio wa makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris utafungua fursa za kibiashara baina ya Tanzania na Marekani, ikiwemo vikwazo viliyopo na namna bora ya kuviondoa.

AP22105550438556.jpg
Mbowe ndio kawezesha hayo hongera fundi wa siasa zetu.
 
Back
Top Bottom