PreGE2025 THRDC yapendekeza mambo 10 ya muafaka wa Kitaifa kufanikisha Uchaguzi wa Amani

PreGE2025 THRDC yapendekeza mambo 10 ya muafaka wa Kitaifa kufanikisha Uchaguzi wa Amani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umetoa wito wa kupatikana kwa Muafaka wa Kitaifa utakaoliwezesha taifa kuelekea kwenye uchaguzi kwa umoja, utulivu na mshikamano. Kwa mujibu wa THRDC, muafaka huo ni muhimu kwani utatoa fursa ya kushughulikia changamoto na dukuduku zilizopo kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Aprili 11, 2025, jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Wakili Onesmo Olengurumwa, aliwasilisha mapendekezo kumi yanayolenga kufanikisha mazungumzo ya pamoja na hatimaye kuundwa kwa muafaka wa kitaifa unaowanufaisha Watanzania wote.

THRDC inapendekeza kuwa mchakato wa muafaka huu uwahusishe wadau wote muhimu wa jamii wakiwemo viongozi wa dini, asasi za kiraia, vyama vya siasa, na taasisi za kiserikali. Aidha, inasisitizwa kuwa usimamizi wa mazungumzo hayo ufanywe na viongozi wenye uzalendo, busara na ambao hawana maslahi binafsi na uchaguzi.

Miongoni mwa hoja zilizotolewa na THRDC kama msingi wa muafaka huo ni pamoja na:
  • Wasimamizi wa uchaguzi wasitegemewe kuwa watumishi wa serikali pekee;
  • Kudhibiti tabia ya maafisa wa uchaguzi kufunga ofisi wakati wagombea wanawasilisha fomu;
  • Kuepuka kuenguliwa kwa wagombea wa upinzani bila sababu za msingi;
  • Kuweka utaratibu mzuri wa uapisho na uwepo wa mawakala kwenye vituo vya kupigia kura;
  • Kutambua makosa ya uchaguzi kama makosa ya jinai pale inapofaa;
  • Kuruhusu vyombo vya habari na waangalizi kutoa taarifa za kasoro za uchaguzi bila kuzuiwa;
  • Kukomesha matumizi ya nguvu kutoka kwa vyombo vya dola wakati wa uchaguzi;
  • Kufanyia kazi upungufu uliopo kwenye sheria na kanuni za uchaguzi;
  • Kuweka uwazi katika mchakato wa uandikishaji wapiga kura na manunuzi ya vifaa vya uchaguzi;
  • Kuhakikisha usalama wa kura na uwazi katika utoaji wa matokeo.
Kwa mujibu wa THRDC, mapendekezo haya yanakusudia kujenga mazingira yenye haki, usawa na amani kuelekea uchaguzi mkuu ujao.
 
Kuna kucha ....huwezi kuandikisha vidudu ati wapiga Kura

Tukutane KISUTU
 

 
Back
Top Bottom