Thread maalum kwa ajili ya kutakiana heri ya mwaka mpya na sikukuu ya X-mass, pia kuorodhesha matukio yote yatakayotokea kwenye X-Mass na mwaka mpya

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2020
Posts
7,799
Reaction score
14,215
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Leo nimeona bora nije na thread ya pamoja kwa ajili ya kutakiana heri ya mwaka mpya na sikukuu ya X-mass.

Lakini pia kila mtu atakuwa huru ku share picha za jinsi watu walivyo celebrity, na kusherehekea mkesha wa mwaka mpya huko atapokuwa, au kuandika matukio yote yatakayotokea katika siku hizo mbili.

Binafsi napenda kutumia nafasi hii kuwatakia heri ya mwaka mpya na sikukuu ya X-mass wanaJF wote waliopo humu, haswa wale ambao wapo tayari kwa ajili ya kusherehekea sikuu hizo.

Najua kwa baadhi ya nchi (ikiwemo hii niliyopo mimi), hiki ni kipindi kigumu kwetu kuumaliza mwaka salama, lkn kwa uwezo wa Mungu wetu alie mwema, mwenye upendo na huruma ya kweli kwetu, basi tutaumaliza salama salmin.. Ameen.

Update 👇

Wakuu kama thread ilivyojieleza hapo juu, kwamba mbali na kutakiana heri ya mwaka mpya na sikuu ya Christmas, lkn pia tutakuwa tukileta picha, video au masimulizi mbali mbali yanayohusiana na sikuu hizi, pamoja na matukio mbali mbali ya mwisho wa mwaka yanayotokea katika nchi, au maeneo mbali mbali hapa duniani.

Mchana huu nilipokuwa nikipita maeneo ya kitongoji cha Bertram jijini Johannesburg, nilikumbana na mkasa fulan wa kutisha na kushtua, ambao umefanyika saa chache tu kabla ya mimi kupita eneo husika.

Inasemekana wazee wa "tupe chetu ubaki na roho yako" walivamia katika ofisi ya betting na kuchukua kila kitu, kisha kutokomea kusikujulikana. Ila kabla ya kufanya operation walimuomba meneja wa ofisi hiyo (muethiopia) awape chao mapema wasepe, yeye akajifanya kuleta ngonjera, ndo wazee wa "tupe chetu ubaki na roho yako" wakampa njugu kadhaa mwilini mwake (sina uhakika kama alikufa au hakufa) kisha wakachukua kwa nguvu kilichowaleta na kupotea.

Kwa mbali, ni picha ikionesha askari kadhaa na gari yao wakiwa katika eneo la tukio. Hakuna gari iliyokuwa inaruhusiwa kusogelea au kupita eneo la tukio (ukizoom utauona utepe wa askari) hivyo nlichukua hiyo 4to kwa mbali na kuendelea na mishe zangu zilizonifanya nipite eneo hilo.

Pliz msikose kuwa mnatupia picha na matukio yote yanayotokea na kufanyika sehem mbali mbali za dunia.

Asanteni
 

Attachments

  • 20231215_113935.jpg
    1 MB · Views: 12
nawatakia heri ya christmas na mwaka mpya singles wote humu jukwaani😀😀😀😀Mungu awatie nguvu

na mnaoteswa na mapenzi mwaka huu ikawe mwisho mwakani mapenzi yawauwe kabisa
Amiin mimi ni m1 wa waliokwama kuowa mwaka huu kutokana na ukata wa fedha.

I hope next year mambo yatajiset na nitaweka jiko ndani tho..
 
nawatakia heri ya christmas na mwaka mpya singles wote humu jukwaani😀😀😀😀Mungu awatie nguvu

na mnaoteswa na mapenzi mwaka huu ikawe mwisho mwakani mapenzi yawauwe kabisa
Mapenzi yameondoka na roho za ndugu zetu wengi 😄😂.

Mungu ajaalie mwaka ujao uwe wa amani na mafanikio katika ndoa zetu 🤲
 
No bad ila umeniwahi

Nawatakia Heri ya Christmas [emoji319] na mwaka mpya Kwa Wana wooooooote niliowakuta humu na walionikuta humu Niko kitambo na Mimi tangu 2018
Amiin mkuu 🤲🤲🤲

Mungu akulinde, akujaalie na akutangulie katika kila jambo jema na lenye manufaa utakalofanya mwaka ujao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…