Thread ya Show ya "I am Zuchu": Kutoa Tsh. million 5 kumuona Zuchu kwenye VVIP inaitaji uwe na utajiri wa Bakhresa

Mkuu utakua hujatenda haki kuhitimisha kwamba show ilikua mbovu kwa kusoma comments za watu ambao wanachojua wao ni kuponda usafini hata iweje.
Ingawa wanao sifia pia ni watu wanaosifia usafini hata iweje, lakini ingetosha kuangalia na kujiridhisha ili angalau maoni yako kuwa show mbovu yapate uhalali badala ya ku base na maoni ya wapinzani wa usafini unless otherwise na wewe ni wa upande wa pili
 
Hawa watu wa usafini wanavyosifia hadi ambavyo havistahili domo akiwaambia inameni niwapige mti hawawezi kukataa
 
Parokiani [emoji23][emoji23][emoji23][emoji1316]
Yaani kila nikipata wasaa wa kuangalia ile show nazidi kupata kituko kipya,
Wanatakiwa wakadai milions zao sio kwa upuuzi ule walai,
Au babe unasemaje??? Lol
Na Bado unaendelea tu kupata wasaa wa kuiangalia tena... Kaazi kweli kweli!
 
Mkuu kuna msemo unaosema wengi wape wachache wasikilize,mbona nimesema show ya mboso ilikuwa nzuri? Kwasababu ya maoni ya wadau,kwani mboso hayupo usafini? ITOSHE KUSEMA Show ya Zuchu ilikuwa MBOVU.
 
Mkuu kuna msemo unaosema wengi wape wachache wasikilize,mbona nimesema show ya mboso ilikuwa nzuri? Kwasababu ya maoni ya wadau,kwani mboso hayupo usafini? ITOSHE KUSEMA Show ya Zuchu ilikuwa MBOVU.
Basi sawa mkuu
Itoshe kusema kuwa maoni yako yaheshimiwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…