Tiba/Dawa kwa mtoto au mtu kikojozi

Habari za jioni,

Nisiwachoshe ngoja nielekee kwenye mada, nina mtoto wangu wa miaka 3, amekuwa akikojoa kitandani wakati akiwa amelala iwe mchana au usiku.

Mwanzo nilifkiri labda ni utoto tu lakini hadi kufikia umri wa miaka mi 3 nafikiri ilibidi awe ameacha.

Hivyo kwa anayefahamu namna ya kumdhibiti ili aache kukojoa maana magodoro yanaharibika sana.

Natanguliza shukrani
 
Muamshe kila mara,usione kazi pia mlimit unywaji wa maji na vinywaj vingine!
 
PIA awe analala usingizi wa mchana.
 
Pole mkuu watu wanaona ni tatizo dogo ila linaumiza sana sijajua specific dawa ila itafika umri ataacha

Dogo mimi aliacha akiwa na 14 ila inaweza kua chini ya hapo
 
Mzoeshe kumwamsha mara kwa Mara atazoea ......mchana usimvalishe pampers ili aanze kujifunza
 
Pole sana Mkuu!! Kuna cku nilikuwa wilaya ya Namtumbo kikaz, xo kuna cku ilo tatizo lako kuna jamaa akawa anatuambia dawa yake alituambia ni Ndizi Mbichi bt nashindwa kukumbuka unaitumiaje iyo ndiz kama dawa
 
Anayekojoa ni ww but acha kumsingizia mtoto mm nakupa ila ni kwa manufaa yako na watu wengine watakao pitia thread hii

Nenda sokoni nunua ufuta mbichi unauzwa kama sh miatano tu anza kutafuna kutwa Mara tatu ndani ya siku mbili tu utaacha kabisa afu pia ufuta unasaidia kupunguza kujihisi haja kubwa ovyo ovyo
Ufuta ni kiboko mpaka sasa usha pona mkuu reta mrejesho hapa baada ya siku mbiliiii
 
Pole kwa tatizo la mtoto wako, Kama wadau wengi waliochangia hapo Juu hakikisha unamjengea mazoea ya kumwamsha mara kwa mara na Akikojoa muonyeshe alichokifanya na madhara yake pia. Limit pia kiasi cha maji ya kunywa mara tu inapokaribia Jioni na Usiku. Naomba Uwapuuze wale wote wanaofanya utani kwa tatizo unalipitia kwa sasa sisi wazazi tunajua ni namna gani unavyoumia
 
Asante sn Mkuu nmekuelewa vyema
 
Sawa mkuu najarib iyo dawa then ntaleta mrejesho, lakin bado nasisitiza kua co Mim ni mwanang mpendwa kwaiyo natafuta dawa ili aache
 

Pole sana mzazi mimi ninae ana miaka 8 sasa. Nimeshajitahidi sana sijapata ufumbuzi. Lakini hili la kulimit unywaji wa vimiminika lina saidia sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…