Tiba/Dawa kwa mtoto au mtu kikojozi

Tatizo kubwa ni wewe ulizembea toka mtoto akiwa mdogo, mtoto anatakiwa kuamshwa kila baada ya mda flani akojoe, unaweza Anza utaratibu uo kaa na poti lake karibu na kitanda muamshe akojoe ata akiwa usingizi muweke kwenye poti mwambie kojoa atakujoa, Acha kabisa kumvalisha pampers na nepi.
Kuacha ugonjwa tatizo kubwa la mtoto kukojoa kitandani linasababishwa na wazazi wazembe na kujipendekeza usingizi
 
Pole sana Mkuu!! Kuna cku nilikuwa wilaya ya Namtumbo kikaz, xo kuna cku ilo tatizo lako kuna jamaa akawa anatuambia dawa yake alituambia ni Ndizi Mbichi bt nashindwa kukumbuka unaitumiaje iyo ndiz kama dawa
Unaichomeka kunakotokea mkojo
 
Kukojoa kitandani kuna sababu zaidi ya mnazozizungumzia. Mimi binafsi nilikuwa mhanga wa kukojoa kitandani mpaka nikiwa secondary. Actually huwa nilikuwa nakuwa kwenye hali flani ya usingizi mzito sana kiasi cha kupoteza ufaham. Yaani ni kwamba naweza sema ubongo unakuwa unashindwa ku control hali ya kudhibiti mkojo.

Hakuna njia itayosaidia hapo huyo ni kumuacha mpaka akue mkubwa atakuja kuacha kama mimi. Ila wanasemaga watoto wanaokojoa kitandani wanakujaga kuwa na akili sana. maana kama nilivosema bongo zao zinakuwa bado zipo busy sana wakiwa watoto ndo mana zinashindwa ku control mambo kama hayo. Btw mimi mwenyewe sahiv ni kipanga hatari mpaka najikubali. 1 st class si mchezo jamani......

mwache mwanao akojoe bana kwa raha zake na usiwe unampiga maana kujikojolea kwa kweli inatokea automatically.
 
Na dawa ya kuhisi mkojo kila wakati ni ipi tena nyakati za usiku
 
Labda ndio mtoto wake wa kwanza huyo
Tatizo kubwa ni hii fasheni ya dada zetu kuzaa bila kuwa tayari kulea. Kuzaa si kazi kazi ni kulea. Unakuta mdada anazaa mtoto na bado usichana anaupenda, anamwacha mtoto katika ulezi wa housegirl masaa yote. Yeye kutwa kuchwa kukimbizana na madushe, madisko n.k.
 
Wengi wanawaachia mama zao watoto...yaani watoto wanaishi na bibi zao.
 
Hakikisha anapotaka kulala asinywe kinywaji chechote,, pia uwe unamuamsha sanaa
 
Mkuu asipo pona kukojow akitandani nitafute mimi nitaweza kumtibia mtoto wako ana akapona kabisa ukiweza kunitafuta bonyeza hapa.Mawasiliano
 
duh nilikua najikojolea hadi kidato cha 5, nilikua naumia sana japo hali ulikua imepungua sana ilibidi nikaombewe tu, toka.siku hiyo nimesahau, sema siwez laumu mtu, unaota upo mahal.kabisa unakojoa vzr ila ile unamaliza tu ndo unashituka daah nilikua naumia

kikojozi halal ugenini ni kwel, yaan nilikua silali.au nalala sakafuni.kabisaa
 
Ndugu zangu wana JF habari za jioni?

Hakika 'mficha maradhi kifo humuumbuwa' na kamwe mimi nisingependa kifo kiniumbue. Nibora hata mimi nijiumbuwe kuliko kifo kije kuniumbua.

Naam wana jamvi wenzangu naombeni , niwaeleze tatizo langu bila ya woga kwani nina taka kupona.

Wana JF ukweli mimi ni "Kikojozi" kwa hakika mimi hukojoa kitandani tangu nilipozaliwa.

Napia mwili wangu nikama kiwanda cha kuzalisha maji (mkojo) kwani nikinywa maji Lita1 basi mimi hukojoa lita2 au na zaidi. Na siyo usiku tuu bali hata mchana.

Mfano:
Leo asubuhi saa 12:00 nilikunywa maji lt1 lakini paka saa 1:00 nilikuwa nimekojoa mkojo Lt 2. Na hii ni kila siku hata nikinywa soda 1 ya ml350 basi nitakojoa mkojo zaidi ya nusu lt1.

Yaani mimi hutoa ujazo wa mkojo Mara 2 zaidi ya vimiminika nilivyo vitumia.

Huwa nina kojoa kitandani, hata kama kutwa nzima sijatumia kimiminika chochote kile. Mfano; juzi nilikunywa maji saa 11:00 asubuhi, na baada ya hapo sikutumia kimiminika chochote kile, na nililala saa 8:00 usiku ila bado nilikinukisha balaa.

Huwa nina kojoa zaidi nikiwa nimelala kuliko nikiwa macho.

Mfano; Mimi huchelewa kulala mpaka muda mwingine hulala saa9:00 usiku na katika muda wote nikiwa sijalala na nikiwa sijatumia vimiminika naweza kukojoa mara moja (1) tu. Lakini nikilala nitakojoa mara nyingi sana.

Nikinywa maji au kimiminika chochote ndani ya nusu saa hujikuta nishakitoa chote yaani ni kama kinapitiliza moja kwa moja.

Naombeni msaada wenu wa kiushauri nifanyeni nini? Nimejaribu dawa nyingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…