ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 83,659
- 90,151
My Take
Tiba zingine ni upuuzi mtupu 😂
😂
============
Wakati wanawake wakikabiliana na changamoto mbalimbali za kiafya zinazohusiana na sakafu ya nyonga, matumaini mapya yanaanza kuonekana kupitia tiba za kisasa, zikiwemo huduma za kurekebisha na kuboresha via vya uzazi pamoja na urembo wa sehemu za siri.
Miongoni mwa changamoto hizo zimewafanya baadhi ya wanawake kutumia vilainishi kujitibu ukavu ukeni, kupungua kwa hisia za kimapenzi, uchafu ukeni na maambukizi ya mara kwa mara, kutumia dawa zisizothibishwa kisayansi kubana uke na kunywa antibaotiki kiholela wakijitibu.
Hayo yameelezwa Machi 25, 2026 na Daktari bingwa wa uzazi na magonjwa ya wanawake, pamoja na mbobezi wa afya ya sakafu ya nyonga (Urogynecology) kutoka Hospitali ya CCBRT, Dk Said Suleiman alipofanya mahojiano na Mwananchi Digital kuhusu huduma hiyo.
Mbali na matibabu ya kiafya, Dk Suleiman amesema sasa kuna huduma za urembo wa sehemu za siri (vaginal aesthetics) ambazo zimeanza kupatikana nchini.
“Wanawake wengine wanakerwa na mabadiliko ya maumbile ya sehemu za siri, kama kulegea au kubadilika kwa ukubwa wa baadhi ya sehemu. Sasa tunaweza kurekebisha kulingana na mahitaji yao kwa njia salama na za kitaalamu,” amesema.