TIC, TAN-TRADE, EPZA, TTB & BRELA: Mrundikano wa Taasisi zinazofanya kazi zinazofanana

Uuuuufffffff....duh,kweli tanzania niya wajanja pekee.
 
watuache hivi hivi taasisi zikiwa nyingi hata watu tunapata vyeo (posho, magari V8 na dili za procurement)angalau mtu unaweza jenga nyumba zako kadhaa za kupangisha. mishahara yenyewe midogo
 
hatarii ngoja nianze kutafuta kazi aisee
 
To me ni namna ya kucreate ualaji serikalini tuu hamna kingine.
Mwisho wa siku wanatupiana mzigo kwenye kutelekeza majukumu yao.
 

Ungeuliza tofauti ya hizo organizations ni nini?

TTB haileti investors bali iko busy na watalii, TIC haifungui export processing zones bali inafacilitate invenstors kwa sera na mazingira wezeshi, BRELA ni kitu kingine tofauti kabisa, same kwa TAN-TRA

Sevu muda kidogo, nenda google, pitia organization moja baada ya nyingine, halafu kwa kukusaidia tu, chora jedwali uwe unaorodhesha kwa kila organization vitu vifuatavyo: mision, vision, malengo/objectives, kazi zao za msingi, wadau wao wa karibu na baadhi ya mifano ya mafanikio yao.

Ukikuta kama wameweka na strategic plans zao pia summarize

Ukimaliza uje na mrejesho
 
janjaweed! nyie ndo mizigo ya nchi hii, rudi shule ELIMU ni BURE kwa sasa, katika muendelezo ule ule wa kubana matumizi taasisi tajwa (zote) zinaweza kuunganishwa na kuwa na taasisi na idara kadhaa.
 
1. NIDA - Vitambulisho,
2. Tume ya Uchaguzi - Vitambulisho,
3. Immigration Dept. - Passport=vitambulisho
4. TRA - Leseni/kitambulisho
5. PPF/NSSF, GEPF n.k - Vitambulisho.
 
Mheshimiwa Mkuu unganisha hizi taasisi kwa dhana ile ile ya kubana matumizi.
 
Taasisi za elimu zinazofanana nazo ni kero;
1. Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam. DIT
2. Chuo cha ufundi Arusha, ATC,
** Changanya pamoja, Mkuu wa Chuo awe mmoja hiyo ya Arusha iwe tawi/campus ya DIT
 
tufike mahala serikali ipunguze hizi gharama za kuwa taaasisi lukuki za kufyonza pesa za mlipa kodi na tija ikiwa ndogo mno
 
Kwa maana nyingine ni sawa na kusema tuivunje IMF na WB tuunde kitu kimoja kwa maana hata hizo zinafanana majukumu
 
Hapa nakukubali ila si kwa hii mifuko ya jamii iliyolundikana
 
Walaji wengi TZ bado imeibuka Workers Compensation Fund.
 
Inashindikana nini Taasisi kama NIDA ambayo inafanya kazi zinazofanana kabisa na RITA kuwa taasisi moja?
 
Ukitaka maendeleo halisi ni lazima taasisi za uzalishaji ziwe nyingi dhidi ya zile za usimamizi.
Kama wasimamizi ni wengi kuliko wazalishaji, maendeleo yatakuwa ya kinadharia tu. Ni lazima uzalishe kwanza ndipo upange na kusimamia matumizi ya kilichozalishwa.
 
Lesabu11 umezungumza jambo la maana mno. Fikiria hata vyu vikuu vyetu vinatoa kozi za kuwafanya vijana wasubiri kuajiriwa (wasimamizi) badala ya kuwapa maarifa ya kuzalisha.
cc. TEKU, MUM & SAUT.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…