Tido Mhando aongoza kikao cha kwanza cha Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari

Tido Mhando aongoza kikao cha kwanza cha Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari

Blasio Kachuchu

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2016
Posts
366
Reaction score
243

Na Mwandishi Wetu.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari ( Journalists Accreditation Board- JAB) Bw. Tido Mhando, akiongoza kikao cha kwanza cha Wajumbe wa Bodi hiyo ikiwa ni siku moja baada ya kuzinduliwa rasmi na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Palamagamba Kabudi na kukabidhiwa Vitendea kazi ambavyo ni Sera, Sheria na Kanuni.

Kikao hicho kimefanyika leo (Jumanne Machi 4, 2025) katika Ukumbi wa Mikutano wa Bodi uliopo Mtaa wa Jamhuri Jijini Dar es Salaam, ili kupokea na kujadili taarifa za utendaji kazi za Bodi, kupitishwa katika Sheria iliyounda Bodi na Kanuni zake, Hati Idhini na miongozo mbalimbali ya uendeshaji wa Bodi kwa nusu mwaka wa Fedha 2024/2025.



Pamoja na mambo mengine, Bw. Mhando na wajumbe wa Bodi wametambulishwa Sekretarieti ya Bodi, ambapo ametumia fursa hiyo kuipongeza Sekretarieti hiyo kwa kazi iliyokwisha kuifanya tangu Oktoba mwaka 2024 hadi sasa na kuahidi ushirikiano ili kuboresha na kuitendea haki dhamana waliyopewa ya kuongeza thamani ya taaluma ya Uandishi wa Habari.


 
Wana ccm Hao wala siyo waandishi wa Habari.
Mhimili wa nne wa serikali
Not at all.
 
Back
Top Bottom