Tigo mnatunyonya sana na MB zenu...

Tigo mnatunyonya sana na MB zenu...

Tigo Tanzania mmezidi kutunyonya na bando zenu, hawa jamaa wana calculate vip hizi MB? Haiwezekani hata robo saa haijaisha GB1 imeisha..!

Hivi tatizo nini hii kitu imeanza kujitokeza wiki sasa, Tigo embu jitafakarini bwana...
Achana kabisa na TIGO.Ni majambazi.

Tumia airtell na TTCL
 
Nadhan Kuna haja ya kuhama hayo makampuni nankurudi kwenye kampuni yetu ya Taifa TTCL....TTCL wakati kama huu tumieni fursa za weakness za washindani wenu mpae..msijifanye na nyie kama wafanya biashara Hawa wanaopiga hela
 
Ujitafakkari pia na wewe..
unanunua bando sungura halafu matumizi tembo
cheki mzigo huu.
View attachment 2273662
Mwenzako anazungumzia ulaji mbaya wa bando wa hayo makampuni wewe unakuja na majingambo, sidhani kama hiyo ni sawa mkuu.

Hizo GB 5 sometimes mimi nazitumia kudownload movies na series kwa siku moja, kwahiyo na mimi nije nikukashifu wewe?

Mwingine akija kukutharau kwakua unatumia Tecno au Infinix utamuona mbaya?

TUJIREKEBISHE.
 
Mwanzoni makampuni ya simu yalikuwa yanajipangia, tukalalamika, wakapangiwa bei
 
Haichelewi kumaliza mb,,

Kiufupi tu,, kwa sasa mitandao gharama ziko juu mno, na kama tusipopiga kelele itabaki hivi hivi au kwendelea kupanda

Kipindi cha nyuma TIGO NA HALOTEL ilikua wanakupa, 3000/=3GB,,,,

Sasaiv LIMTANDAO LA TIGO👉🏽 1500 mb900, 1500 mb750, 2000 1GB, 2500 1.4GB,,,,Halotel hawapishani sana na tigo.

Kwahiyo hama hama haina maana, hawa wote kitu kimoja, may be wanakaa meza moja na kukubaliana tufanye hivi mara hivi.

Kwakweli Kila mtu analalamikia upande wake, tigo, halotel, airtel, voda, ttcl


Ushauri wangu, kwa upande wa MB tutumie WIFI UNLIMITED, MB za simu tususe, acha waumie. Kama kuna mtu anajua atujuze kuhusu hii kitu.
 
Mwanzoni makampuni ya simu yalikuwa yanajipangia, tukalalamika, wakapangiwa bei
Kwa upande mwingine serikali pia ya kulaumiwa,,,kama serikali yenyewe inawapandishia makodi unadhani bei za vifurushi vitabaki kama mwanzo!! Acha walegezewe ili vifurushi vishuke bei. Mimi nafikiri ni hilo ndio sababu ya wao kupandisha mkuu,, au wewe unalionaje!!
 
Tigo leo mbona haielewek Upande wa tigo pesa tukitaka kununua vifurushi inakataa
 
Hao Tigo ni WEZI kama tu wengine. Wanaiba data za wateja wao kwa kuzimaliza ili ununue tena na tena.

Tanzania tunaibiwa sana na haya makampuni uchwara ya simu
Halafu hatuna mtetezi wa kweli, wanapiga kelele bungeni hakuna utekelezaji
 
Tigo Tanzania mmezidi kutunyonya na bando zenu, hawa jamaa wana calculate vip hizi MB? Haiwezekani hata robo saa haijaisha GB1 imeisha..!

Hivi tatizo nini hii kitu imeanza kujitokeza wiki sasa, Tigo embu jitafakarini bwana...
mimi nilikuaga tigo na namba yangu ilikuwa 0653808003...lakini niliachana nao miaka kama 6 hivi na sasa niko kwa airtell
 
Tigo ni matapeli ,mbwa kabisaa

Wanaiba MB za watu.

Nina miezi miwili Sasa nmehamia AIRTEL Kwa kweli Nina AMANI kabisa !!

Internet ya Kasi, hawaibii yaan ni matumizi yako .
 
Hawa ni wahuni, usije ukaingia mkenge kutumia huduma hii
👇
Huduma ya Niwezeshe inakuwezesha kupata mkopo wa salio la muda wa maongezi au kifurushi ukiwa hauna salio. Piga *147*00# chagua Niwezeshe.

Kopa mkopo wa salio kwa kupiga *147*00# chagua Niwezeshe. Unaweza nunua kifurushi cha Combo Tsh500 chenye Dk35+MB200+SMS20 kutumia salio lako la Niwezeshe.

Tangu lini mtu akakukopesha halafu akakupangia masharti ya kutumia mkopo wako, yaani unakopa 10,000.00 halafu anakuambia
  • 2500 nunua nguo za ndani,
  • 3000 nunua dawa ya mswaki
  • 1500 nunua ufagio
  • 3000 nunua chanuo
 
Back
Top Bottom