tiGO wajitenga na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Lissu. Wasema mmiliki wa sasa ni mwingine si yule wa nyakati za shambulio!

tiGO wajitenga na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Lissu. Wasema mmiliki wa sasa ni mwingine si yule wa nyakati za shambulio!

Tatizo linapokuja ni kwamba inakuwa ngumu kuishitaki Tigo kwasababu zifuatazo:

Taarifa za Lissu zilivuja kipindi ambacho kampuni mama iliyomiliki Tigo ni "Millicom International Cellular public limited company"

Mwaka 2022 hadi sasa kampuni mama mmiliki wa Tigo ni "Honora Tanzania Public Limited company"

Ni sawa na kushambuliwa na jirani, akihama nyumba ni ngumu kuishtaki nyumba yenye jirani mpya,
Anajichoshaaaa tu tigo 3yrs back imeuzwaaa
 
Tatizo linapokuja ni kwamba inakuwa ngumu kuishitaki Tigo kwasababu zifuatazo:

Taarifa za Lissu zilivuja kipindi ambacho kampuni mama iliyomiliki Tigo ni "Millicom International Cellular public limited company"

Mwaka 2022 hadi sasa kampuni mama mmiliki wa Tigo ni "Honora Tanzania Public Limited company"

Ni sawa na kushambuliwa na jirani, akihama nyumba ni ngumu kuishtaki nyumba yenye jirani mpya,

Madeni yanayokuwepo wakati huo
Sio kesi za mafao ya wafanyakazi

Ndio maana kampuni zilizobinafsishwa hadi leo wafanyakazi wanasota kutafuta mafao yao hawaendi kwa wawekezaji wapya
Clifford kule London anamshtaki Nani?acheni utetezi wa Kitoto.
 
Tatizo linapokuja ni kwamba inakuwa ngumu kuishitaki Tigo kwasababu zifuatazo:

Taarifa za Lissu zilivuja kipindi ambacho kampuni mama iliyomiliki Tigo ni "Millicom International Cellular public limited company"

Mwaka 2022 hadi sasa kampuni mama mmiliki wa Tigo ni "Honora Tanzania Public Limited company"

Ni sawa na kushambuliwa na jirani, akihama nyumba ni ngumu kuishtaki nyumba yenye jirani mpya,

Muhimu ni kujua mualifu yuko wapi na siyo anayemmiliki mualifu. Ndiyo maana unaweza kufungua kesi X ukashutukia na Y anaingizwa na pengine kufungwa pia.
Kumbuka kesi ya Kihiyo wa TEMEKE
 
Imeshtakiwa kampuni sio wamiliki
Samahani, lakini tulia kwanza kwani hauna akili za kuweza kumjibu haraka msemaji wa kampuni kubwa kama hiyo. Fikiria vizuri, elewa, kwa upana (kama una ufahamu wowote wa mambo hayo) Kisha ndo useme lolote.
 
Inayoshtakiwa ni Kampuni siô Mmiliki.
Hivyo Kesi bado Ipo palepale.

Nilitegemea Wakanushe kuwa hawakufanya hivyo lakini Kwa kauli yao inathibitisha kuwa kitendo kilifanyika na kilifanywa na Kampuni ya Tigo, semà Mmiliki ni Mwingine.

Jina la Kampuni NI lilelile.
Wateja wa Tigo na Namba za tigo ni zilezile ikiwemo Mhanga àmbaye ni Tundu Lisu

Hivyo Kesi Hapo bado yamoto.
Naona mnakimbilia haraka kujibu kijf jf.......niko paleee nimetulia.😊😊😊
 
Kampuni ya TIGO imesema haihusiki na sakata la kuvuja Taarifa za Tundu Antipas Lisu

HONORA imesema kampuni mama ya Tigo haikuwa mmiliki Wakati Makamu mwenyekiti wa Chadema mh Tundu Antipas Lisu anashambuliwa
----
Dar es Salaam. Kampuni ya Honora Tanzania Public Limited Company ("TIGO") imejitenga na taarifa za kuvujisha taarifa za simu za Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu, ikisema kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa.

Taarifa hiyo inatokana na kesi inayoendelea nchini Uingereza kati ya Kampuni ya Millicom iliyokuwa ikimiliki Tigo na aliyekuwa mfanyakazi wake, Michael Clifford ambaye sasa amefukuzwa kazi.

Kwa mujibu wa Gazeti la The Guardian la Uingereza la Septemba 24, 2024, Clifford aliwasilisha maelezo yake katika mahakama ya London kuwa, chanzo cha kufukuzwa kwake ni kutoa ripoti ya jinsi kampuni hiyo ilivyotoa taarifa za mawasiliano ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu.

Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa kwenye gari lake alipokuwa akielekea kwenye makazi yake baada ya kuhudhuria vikao vya Bunge jijini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa la Honora Tanzania Public Limited Company leo Septemba 26, 2024 imeleza kutambua taarifa ya kesi inayoendelea nchini Uingereza ya ajira katika mahakama ya London inayomhusisha mfanyakazi wa zamani wa Millicom, kampuni mama ya Tigo hadi mwaka 2022.

Soma Pia:

“Kampuni mama ya sasa ya Tigo haikuwa mmiliki wake wakati tukio lililoripotiwa lilipotokea,” imesema taarifa hiyo.

Imesema japo hawawezi kutoa maoni kuhusu undani wa kesi hiyo kwa kuwa hawahusiki moja kwa moja, bali wanahakikisha ulinzi wa taarifa za wateja wao.

“Tunataka kuwahakikishia wateja wetu na wadau wetu kwamba kulinda data zao binafsi kwa kuzingatia sheria na kanuni za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, bado ni kipaumbele chetu kikuu,” imesema taarifa hiyo.”

Chanzo: Mwananchi
Kama mmiliki alibadilika mbona hakubadilisha kuna kama akina Zain ni?
 
Clifford kule London anamshtaki Nani?acheni utetezi wa Kitoto.
Anashitaki kampuni ya Milicom sio Tigo sababu hata yeye anajua hakuna kampuni inaitwa Tigo kwenye daftari la msajili wa makqmpuni Ulaya wala Tanzania

Ni Lisu tu ndie kakurupukq kama kawaida yake huwa kichwa chake utulivu huwa zero

Tigo haina kesi ya kujibu mahakama yeyote duniani iwe uingereza au Tanzania sio kampuni nanhaijawahi sajiliwa popote duniani.kwenye daftari la msajili wa makampuni popote duniani kama kampuni na haimo kwenye hati ya mashtaka

Lisu ana ujinga fulani hivi kwenye sheria ila ana kelele nyingiiiiiiiiii

Kichwani sheria nyingi yuko zero

Kwa Chadema Kibatala tu ndio yuko vizuri

Lisu hamna kitu
 
Back
Top Bottom