Kampuni mama ya tiGO Tanzania 'HONORA TANZANIA MOBILE SOLUTIONS LTD' wamefikishwa mahakama ya mwanzo Ilala wakidaiwa fidia ya shilingi milioni 26,880,000/=
Shauri hili namba 270/2024 litaanza kusikilizwa mbele ya hakimu mfawidhi Judith Kobo baada ya tigo kutuhumiwa kuanzia kipindi cha tarehe 30 April mpaka 16 May 2024 kumkata mteja Aitwae Benedict K. Kiasi cha shilingi 118,000/= kinyume cha utaratibu.
Madai haya yamefikishwa mahakamani baada ya hapo awali Mteja kuwasilisha malalamiko yake dawati la malalamiko la tiGO kwa mujibu wa kanuni za benki kuu zinazomlinda mteja za mwaka 2019, ambapo tiGO hawakujibu.
Mteja aliwasilisha malalamiko yake Benki Kuu ya Tanzania kwa mujibu wa kanuni, ambao benki kwa barua yao ya tar 1/9/2024 walimshauri mteja kuwasilisha malalamiko hayo mahakamani ili kupata uamuzi wa mahakama.