Tigray Kuna mkono wa Egypt?

Tigray Kuna mkono wa Egypt?

Ugomvi wa Watigray na Serikali inatokana na kosa lililofanywa na PM AA baada ya kuingia madarakani kwa kutaka kufanya siasa za exclusion. Yaani kujaribu kuwaondoa watu waliokuwa wamejaa ndani ya Jeshi, Intelligence, Polisi, Utumishi wa Umma, Utawala na Siasa.
Na hili ndio jibu sahihi kabisa.
 
Yeah. Alifanya kosa sana. Madaraka yanalevya kwa sababu haitarajiwi mtu aliyewahi kuwa mkuu wa intelligence kutojua nguvu ya mifumo na madhara ya kujaribu kuwaondoa.
Mimi Huyo jamaa nilimpuuza mapema Sana,Ile siku wanajeshi wame protest wakaenda mpk ofisini kwake,eti na yy ili kuwashusha mzuka akaanza kupiga nao push up.Nikajua huyo hajui maana ya kua Commander in chief
 
Na kitu kingine ni jinsi muundo na mgawanyo wa nchi ya Ethiopia kiutawala. Kwa Ethiopia mikoa /majimboimegawanyika kikabila. Kila kabila lina mkoa wake. Kuna Amhara, Tigray, Somali, Oromo etc. Mtu anaweza akauliza mbona hata hapa kwetu zamani karibia kila mkoa na kabila lake? Lakini hali ni tofauti kwa Ethiopia. Hii ni kwa sababu yale majimbo yanakuwa na utawala wake na wanaweza kuanzisha vikosi vya ulinzi na usalama na hata vyama vyao vya kisiasa. Yaani Ethiopia ni shirikisho. Kwa hapa kwetu mikoa haikuwa na mamlaka yoyote. Na ndio maana hata hadi leo ngazi ya mikoa kwa hapa kwetu is pure administrative na hutegemea ruzuku kutoka serikali kuu. Na haina authority wala powers of establishments.
 
Tukumbuke kipindi Eritria inapigana vita ili kujitenga na Ethiopia, Ethiopia walipeleka silaha nyingi Tigray ili wapambane na Eritria na baada ya Eritria kujitenga, Tigray walibaki na silaha nyingi za nchi hiyo. Moja ya sababu ya Tigray kuwa na silaha nyingi ni hiyo. Ethiopia iliamua kuziacha silaha hizo katika jimbo la Tigray ili kujihami na Eritria.
 
Vita Ethiopia ipo sehemu ndogo sana ila media zinakuza mambo. Utasikia TPLF wakaribia kupata ushindi, wakati Addis Abbab watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida, sana sana ni umeme tu unasumbua
 
Umeme umetika tangu asubuhi afu ndo nategemea ju pump maji ndo niishi kila kitu kuoga na joto hili , chooni tena vya ku flush...familia ya wageni wapp kwangu sijui wanaondoka lini?
 
Al Sisi mjeda mwenye intelijensia makini. Huenda hata ndo anawanyoosha Sudani
 
Vita Ethiopia ipo sehemu ndogo sana ila media zinakuza mambo. Utasikia TPLF wakaribia kupata ushindi, wakati Addis Abbab watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida, sana sana ni umeme tu unasumbua
USA ndo anavumisha hayo mambo! Ili amkomoe mfadhili wa Abbiy Mchina. Angalia CNN ndo utawaelewa vzr Marekani
 
Watigray wakichukua nchi wataendelea na ujenzi wa bwawa na Ethiopia itarudi kwenye economic growth yake.
Sema wakichukua nchi kwa hisani ya Misri (Kibaraka wa Uzayuni)
 
Back
Top Bottom