Tiketi za 'Simba Day - Ubaya Ubwela' zinakaribia kuisha, Yanga mnafeli wapi?

Mkuu sold out ndiyo, je hizo tiketi zilikuwa ngapi? Isijekuwa sold out kumbe tiketi yenyewe zilikuwa 20,000 kwa ujumla.
Kwa mujibu wa takwimu za Tff Yanga ndio timu inayo ingiza mashabiki wengi viwanjani ata msimu ulio malizika 2023/2024 Yanga walikua vinara kwa mashabiki wengi viwanjani.
Simba kwenye tamasha lao uwa Wana jitekenya na kucheka wenyewe uwa wanaweka mabango ya Sold out wakati ukienda uwanjani unakuta uwanja una mapengo yakutosha.
Ila sio mbaya wanajifurahisha wenyewe.
 
Simba ni kawaida kutangaza Sold out ila uwanja unajaa mapengo mpaka aibu.
Tff Walisha toa takwimu, Yanga ndio timu inayo ongoza kwa mashabiki wake kujaza viwanja iwe nyumbani au ugenini..
Msimu uliopita wa 2023/2024 Kwa mujibu wa Tff Yanga ndio vinara wa kujaza viwanja, Hii michezo ya Simba ya kujitekenya na kucheka wenyewe Yanga haipo na hutoiata.

Tarehe 04/08 ni full house ambayo si ya Mchongo.
 
Mfumo wa mauzo ya tiketi za mpirani kwa sasa huwa hakuna mwanya wa kufanya udanganyifu. Kubali haya matokeo b... ili mjiruhusu kujifunza katika hili.

Ova
Nikukumbushe tu, msimu jana mlisema hivihivi mkaishia na uwanja nusu. Sasa sijui tujifunze lipi hapo?
 
Wazee wa bure mmekumbukwa

[emoji599] Young Africans SC kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa Damu Salama kesho Alhamisi kutakuwa na zoezi la uchangiaji Damu.

Zitatolewa tiketi za bure kwa mashabiki na wanachama wa Yanga wote watakaoshiriki.
Simba hawawezi kutoa za bure kwasababu ndiyo njia pakee mfadhiri anaweza pata pesa,(,punguza makali ya uwekezaji)
 
Nikukumbushe tu, msimu jana mlisema hivihivi mkaishia na uwanja nusu. Sasa sijui tujifunze lipi hapo?
Mwaka jana ilikuwa hairuhusiwi kuuza tiketi elfu sitini. Serikali iliruhusu watu elfu hamsini tu uwanjani, ila Simba iliomba iingize japo watu elfu hamsini na tano.

Ndiyo ikapewa nafasi ya kuongeza watu elfu tano, wakawa elfu hamsini na tano, ndiyo maana unaona kulikuwa na hayo mapengo. Ila mwaka huu ni elfu sitini.

Ova
 
Sawa b…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…