Timu bora imepoteza mechi kwa penalti, mashabiki na wanachama msihuzunike mnayo timu bora msimu huu

Timu bora imepoteza mechi kwa penalti, mashabiki na wanachama msihuzunike mnayo timu bora msimu huu

Majok majok

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2023
Posts
783
Reaction score
2,057
Najua wanachama na mashabiki mmehuzunika kupoteza ngao leo lakini huzuni yenu itakwisha siku sio nyingi!
Yanga wameonyesha bado wanacho kikosi bora sana kuanzia beki na viungo but tatizo lipo kwenye final third, ambalo nafikiri kocha gamond anatakiwa alifanyie kazi, na aanze kumtumia Hafidh konkoni pale kati badala ya mzize maana Mzize bado hana ukomavu kwenye kuamua matokeo pindi timu inapohitaji uwezo binafsi wa mchezaji.

Yanga ikisharekebisha ilo eneo basi itakuwa imekamilika kwa 100% kupambana na timu yoyote ile barani africa, Leo simba amejikuta kama second team, viungo wake wote wamepotezwa vibaya sana, sikuona kapombe wala mohamed hussein wakipanda kama walivyozoea, kina miquison na chama walikuwa kama watumishi hewa, boco ntibanzokiza nao walikuwa kama awapo uwanjani walifichwa vibaya sana, Na mwisho ball possesion ni 56 kwa 44 ya simba!

Ninaamini yanga anakwenda kutetea tena ubingwa wake wa ligi kuu msimu huu bila shida yoyote ile, squad aliyonayo sio ya kitoto, ni hatari, na simba nawashauri ya kwamba bado wana kazi kubwa ya kufanya, kikosi kilichoanza kwa asilimia kubwa ni kile kile cha msimu uliopita na wanacheza mpira utafikiri ni timu mpya,
Kina baleke wamebaki majina tu na kina miksoni, akuna lolote la ziada waliloongeza, labda yule beki che malon angalau ana kitu alichokiongeza.

Pongezi kwa kocha Gamondi kazi yake inaonekana anatengeneza timu tishio sana
 
Kuna tofauti ya kucheza mpira na kuchezea mpira, ila mwisho timu bora huwa inashinda.
Kwa kweli...naona maelezo mengii...ajue tu timu mbovu ndiyo inayofungwa
 
  • Thanks
Reactions: K11
Diego Semeone aliwahi kuwakebehi Fc Barcelona . Aliwaambie nyie endeleeni kumiliki mpira mtakavyo lkn sisi tumiliki nafasi kati ya mchezaji wetu na mpinzani. Mwisho wa game Barca alikula kipigoooooooooo
 
Back
Top Bottom