Timu inashinda bao 7 na mpira mwingi sana, ya nini kutafuta Kocha mpya wa kumrithi Mgunda?

Mwishokambi

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2020
Posts
390
Reaction score
1,425
1. Hakuna kocha wa ligi kuu aliyeshinda bao 7 hadi sasa zaidi ya Simba.

2. Kuna siku Mgunda atamfunga mtu 10.

3. Kuondoka kwa Barbra watu wa kazi wamerudi ndani ya timu.

4. Onyango amechoka na hastahili kuendelea kuwa Simba, kuna siku tutalia.

5. Simba imuongeze Kevin Nashon, Mudathiri Yahya na yule Zibona wa Prisons.

6. Saido Ntibazonkiza mtu mbad sana.

7. Mpira mwingi sana unapigwa Simba, ya nini kutafuta kocha mgeni.

8. Mgunda Kocha Bora mwezi Disemba.

9. Kombe la Mapinduzi tuwapime
wachezaji tunaotaka kusajili.

10. Tunataka wachezaji kama Ntibazonkiza, anasajiliwa anaanza sio anakuja kukaa benchi kama Akpan, Okwa, Quattar.

11. Simba impeleke kwa mkopo Peter Banda, kwani pembeni imekamilika sana.

12. Kumleta kocha wa kigeni wakati mpira unapigwa mwingi ni kuivuruga timu.
 
Mimi ni Simba pia,
Timu kushinda bao 7 inaonyesha wamecheza na timu iliyocheza chini ya kiwango na wao pia wamecheza chini ya kiwango.

Mimi sidhani kama kulikuwa na mpira wa kutumia akili na technics.

Hayo magoli hayamaanishi timu ni Bora na kocha ni next level.
7 goals😳 out of one walipiga penalty nini🤗.

Kwa mpira wa hivi Kuna mengi ya kujifunza, Bado sana
 
Maboresho kwenye timu ya SIMBA SC yanahitaji umakini sana.

Hakuna haja ya kuleta kocha atakuja kuvuruga timu, kikubwa nafasi chache tu zinahitaji kuongezewa nguvu mfano; beki mmoja imara wa kati, mshambuliaji mmoja na kiungo mkabaji mmoja.
 
Goli 5 kadi nyekundu, goli 7 kadi nyekundu.....nawaza tu [emoji143][emoji87]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Utazeeka kwa kuwaza.
Maana njia pekee kuizua Simba kufunga goli tatu ni kuwachezea rafu mbaya wachezaji wake hatari.Lakini waamuzi wameanza kung'amua hiyo mission yenu utopolo.

Labda muongeze dau kwa waamuzi ili wavae miwani ya mbao mara michezo ya rafu mbaya inapofanyika.

Utopolo mmewaponza wenzenu

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Magoli mazuri ya mipango kabisa yale, ajabu hamuoni, mnashangaza sana.

Combination ya Saidoo na Bocco kwenye goli la kwanza ilikuwa superb.

Saidoo himself magoli aliyofunga, yana quality za kutosha;

- jamaa ni fighter ( anafunga akiwa amezungukwa na mabeki) ana mbio, nguvu, na anajua goli lilipo.

- anatumia miguu yote, anafumua mashuti makali sana.

Ubora wa Chama kama kawaida hayupo wa kuutilia shaka..
 
Sio kila mechi mtacheza na wapinzani 9 uwanjani msiongee maneno mkamaliza, mechi na mtibwa mlishinda goli 5 baada ya kadi 2 nyekundu, mechi na prison mmeshinda goli 7 baada ya kadi moja nyekundu, Na mshaanza midomo mirefu mnaferi wapi nyie vijana wa rage
 
Msiongee maneno mkamaliza Utopolo ... Na nyinyi mtatendewa haki... mtafanyiwa msako kama jana na kufungwa mabao ya kutosha
 
Umesoma ulichoandika ukakielewa?! Timu inachezaje chini ya kiwango halafu ifunge goli Saba?! Haya hao waliokuwa wamecheza kwa kiwango cha juu walimfunga goli ngapi huyo Prisons?!
 
Umesoma ulichoandika ukakielewa?! Timu inachezaje chini ya kiwango halafu ifunge goli Saba?! Haya hao waliokuwa wamecheza kwa kiwango cha juu walimfunga goli ngapi huyo Prisons?!
Hata wewe huelewi ulichoandika,
Ni ngumu kuniaminisha kuwa hiyo timu IPO vizuri na kocha yupo njema, kwa mtazamo wangu BADO SANA
 
Nauhifadhi huu Uzi kwa ajili ya mechi zijazo
 
Kadi nyekundu ndio ujinga gani yani mtu acheze madhambi halafu aachwe tu

NB: MSIMU WA 2016/2017 SIMBA AKIWA NA NYEKUNDU ALIMGONGA UTO 2:1.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…