Southern Highland
JF-Expert Member
- Mar 22, 2017
- 14,938
- 25,405
Hii ni moja ya timu zinazonivutia sana kwenye ligi kuu uingereza nje ya kushabikia Chelsea. Sera yao ni kukuza na kulea vipaji pamoja na kuuza kama anapatikana mteja. Kinachonivutia zaidi ni namna wanaweza kusumbua vigogo na kutawala kwa kiasi fulani ligi ya EPL japo wanakua wamepitia vipindi tofauti kwa wachezaji wao na benchi la ufundi. Wanaweza kuuza wachezaji na hata makocha lakini kukuta wanasua sua ni mara chache sana.
Toka kipindi cha Graham Potter, akaja De Zerbi na sasa wana kocha mdogo kuliko wote EPL Fabian Hurzeler wanaonekana tayari wamepshajipata. Hii timu haiogopi kuuza wachezaji wala kuondokewa na makocha. Wachezaji kama Lallana, Mac Allister, Caicedo, Cucurella n.k ni kati ya biashara nzuri walizofanya kwa vilabu vingine.
Sio kila timu inakua na malengo ya kubeba makombe.