Timu kubwa kubebwa na marefa waziwazi kutakuja kusababisha maafa makubwa nchini

Ninachosema tff inashindwa nini kuweka tv pale uwanjani ili magoli na adhabu zenye utata ziwe replayed palepale uwanjani ili kusaidia kutoa haki kwa timu zote bila kujali ukubwa wake? TFF inaogopa nini kuongea na Azam tv kuhusu hili?
TFF haiwezi kuleta kitu kipya ambacho CAF na FIFA hawajapitisha ,hata ligi za misri na south africa sidhani kama inatumia VAR ,labda mfumo wa VAR utumike lakini huo mfumo wa kutumia reply ya tv kufanya maamuzi pale pale haupo
 
Kavae kjora chako uanze kucheza singeli. Ile penalty ya yanga dhid ya simba hukusema lolote. Penalty ya yanga dhid ya Kmc ulikaa kimyaa. Zuzu kwel ww
 
Ninachosema tff inashindwa nini kuweka tv pale uwanjani ili magoli na adhabu zenye utata ziwe replayed palepale uwanjani ili kusaidia kutoa haki kwa timu zote bila kujali ukubwa wake? TFF inaogopa nini kuongea na Azam tv kuhusu hili?
Hujui mambo ya football wewe. Unawaza mambo yako ya singeli. Kavae dela lako Dada. Aaah
 
Hakuna maafa yoyote yatakayotokea, labda useme ni matamanio yako maafa yatokee. Pole sana, naona umeandika kwa uchungu sana. Machi imeisha, Simba imeenda Harare, Yanga imeenda Arusha
 
Nilivyoona tu ushauri kwamba picha za Azam tv zitumike kama VAR nikaishia hapohapo.
 
Timu za Tanzania ndio maana hazifiki mbali kila mara ni kubebwa tu.

Timu kubwa kama Simba pamoja na kuwekeza pesa zote zile lakini bado haiwezi kuishinda timu ndogo kama KMC mpaka hadi wabebwe kwa kupewa penalti ambayo haikuwepo..!! Bure kabisa.
Utopolo huwa haibebwi?
 
haya mabo ya 'match fixing' wanayo fanya simba sport club si yakuyafumbia macho kabisa, yaani mwaka juzi + mwaka jana na msimu mambo ni yale yale tuu, tff inaishia kuwafungia waamuzi tuu badala ya kukata mzizi wa rushwa
 
Point yako ingeweza kuwa ya kujenga zaidi kama usingeweka biasness, Simba na Yanga wote ni wanufaika wa hii michezo michafu.

Otherwise unaonekana kama lialia tu anayeleta malalamiko baada ya kuona Simba anakukaribia.
 
haya mabo ya 'match fixing' wanayo fanya simba sport club si yakuyafumbia macho kabisa, yaani mwaka juzi + mwaka jana na msimu mambo ni yale yale tuu, tff inaishia kuwafungia waamuzi tuu badala ya kukata mzizi wa rushwa
Na ya yanga umesahau kona goli na mapenati mnayopewa na ile mechi ya simbaa mlopewa penati ya nje Gsm alinunua mechi
 
Utopolo huwa haibebwi?
Lazima kuwe na mjadala mpana na kina kuhusu ligi yetu. Timu ndogo zinatumia gharama kubwa sana kwa taabu kuhudumia timu zao, watu hawawezi kupata matokeo ya uwanjani kwakutumia marefa. Iko siku kuna jambo kubwa litatokea tena litaanzia kwenye timu za taasisi za umma dhidi ya waamuzi au mashabiki kwa mashabiki, mashabiki kwa viongozi wa timu. Iko siku enough itakuwa enough, it is just a matter of time wakati tolerance thresholds zinapoendelea kwenda chini.
 
haya mabo ya 'match fixing' wanayo fanya simba sport club si yakuyafumbia macho kabisa, yaani mwaka juzi + mwaka jana na msimu mambo ni yale yale tuu, tff inaishia kuwafungia waamuzi tuu badala ya kukata mzizi wa rushwa
Mechi na gwambina refa alikataa goli la wazi la gwambina, mechi na kmc yanga walipewa penati isiyo halali, mechi na Simba yanga walipewa penati isiyo halali na Simba walinyimwa penati mbili za wazi lakini hatukukusikia ukisema chochote sanasana matukio ya yanga kubebwa yamepungua baada ya Senzo kupelekwa polisi.
 
Hebu ona TFF kukaa kimya wakati Morrison akinyooshea watu kidole cha kati kuonyesha matusi. Kama angekuwa mchezaji wa timu nyingine isiyo simba mchezaji huyu angeshashukiwa na tff. Iko simu mambo makubwa yataonekana nchini
 
Timu za Tanzania ndio maana hazifiki mbali kila mara ni kubebwa tu.

Timu kubwa kama Simba pamoja na kuwekeza pesa zote zile lakini bado haiwezi kuishinda timu ndogo kama KMC mpaka hadi wabebwe kwa kupewa penalti ambayo haikuwepo..!! Bure kabisa.
Simba wamewahi kufika robo fainali African Champions League 2019.

Vipi utopolo huwa wanafika popote ?
 
Yaani Young African inabebwa na waamuzi mpaka aibu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…