Timu ndogo kubalini kufungwa na Simba na Yanga ili mpone.

Timu ndogo kubalini kufungwa na Simba na Yanga ili mpone.

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Baada ya mechi za Simba au Yanga kufanya vizuri mechi zinazofuata timu ndogo hazifanyi vizuri, zinafungwa na timu ndogo wenzao. Hii inatokana na makocha au wachezaji wenyewe wa timu ndogo kwa sababu zao kutumia nguvu nyingi sana kupita kiasi kutaka kulazimisha kuzifinga Simba na Yanga kwa gharama yoyote Ile hata kwenye viwanja vibovu.

Hali hii inasababisha wachezaji wengi kuumia na kuchoka sana kimwili na kiakili ndanii kwa ndani na kubaki na maumivu hayo kwa muda mrefu kiasi Cha kushindwa kufanya vizuri zinapokutana na timu za kimo chao. Mifano ya mechi na timu za aina hii Iko mingi sana kwenye ligi yetu.

Makocha na wachezaji wa Timu ndogo lazima wafahamu kuwa Simba na Yanga ni timu kubwa kwenye ligi zenye vikosi vipana, walimu wazuri, fedha nyingi na matibabu mazuri kwa wachezaji wao. Hivyo, ukiwakamia sana unaweza kupata maumivu na uchovu wa kudumu kwenye kikosi chako kiasi kushindwa kucheza na kupata matokeo na timu za aina yako, hivyo kuweza kushuka daraja.

Ligi Ina meshi 30 ukifungwa na timu 2 TU kwenye ligi utabaki sehemu salama TU kwenye msimamo wa ligi. Conserve your energy by not exercising DO or DIE against Simba and Yanga to avoid permanent and long lasting injuries and exhaustion.

Kwa shujaa kunaingia kilio
 
Back
Top Bottom