Timu ya hamasa AFCON mnasemaje kuhusu jezi ya taifa stars?

Timu ya hamasa AFCON mnasemaje kuhusu jezi ya taifa stars?

sisi uchumi wetu mdogo. tuna poor purchasing power. nike, adidas, puma huwa wanakuja wakiona uchumi mkubwa.

wanatazama je mna mashabiki wa kununua jezi kwa bei zao.
Shabiki mwenye akili zake nyingi hawezi kununua jezi hizi z Sandaland kwa tukio kama hili ambalo ni nadra kwetu. Hakuna mchezaji wa timu pinzani atakubali kubadilishana jezi yake na mchezaji wa taifa stars mwenye jezi isiyofahamika imetoka wapi. Bila shaka wachezaji watakuwa wanalilia jezi za wenzao na kusubiria kwa hamu zoezi la kubadilishana jezi baada ya mechi.
 
We jamaa akili huna tangu lini brandikacheza mpira.
Af kwa akili yako ukivaa sijui nike na adidas hujui kama unamfaidisha mzungu ambaye hana impact kwenye maisha yako. Bora hata sandarland akiuza jezi ananunua sukari analipa kodi anatoa ajira n.k.
Hapo ndio unaonuesha kuwa wewe ni mjinga wa kupindikia. Mpira unachezwa kichwani kule mguuni ni baadae sana. Timu Ina wachezaji international wanahitaji international treatments pia.

Mchezaji umtoe timu ya Liverpool halafu avae jezi ya Sandaland!!! Huna akili, maana hata mwehu anajua kitambaa kizuri Cha suti kinatoka nchi gani na kimetengenezwa na kampuni gani na fundi yupi akishone.
 
Mpira ni mind game with profitable skills .jezi is not cup of tee.
 
Sandaland ndio inayoivalisha timu ya taifa. Wachezaji wetu ni vijana wenye akili timamu wanajua ni Brands zipi duniani zinatengeneza jezi Bora (prestigeous) na zipi zinatengeneza jezi hafifu (inferior) sokoni. Inafahamika kuwa Nike, Puma, adidas, umbro, nk ni kampuni bora kwa vifaa na jezi. Sisi tumewavalisha vijana wetu "matambala" yasiyofahamika yametoka wapi. Vijana wetu wanajiona inferior kuanzia kwenye jezi na mavazi.

Timu yetu itaanza kufungwa kwenye jezi walizovaa kwanza kabla ya kufungwa uwanjani.

Sisi kufika Afcon sio jambo la kawaida, tulipaswa kutafuta jezi Bora ili vijana wetu wajione wako sawa na wenzao kiwanjani na zinazohifadhika kama kumbukumbu.

Kamati ya hamasa hamlioni hili? Hata mjukuu wangu usipomnunulia begi la shule la kampuni inayofahamika kwa ubora analikataa.
Kwamba tukivaa jezi ya puma au addidas tunaweza kumpiga morocco huyu aliefika semis world cup?
 
Back
Top Bottom