carnage21
JF-Expert Member
- Jan 24, 2023
- 591
- 1,382
Nakumbuka baada ya mafanikio makubwa 2012/13 viongozi wengi kutoka Halmashauri za Miji tofauti mikubwa na midogo, walisafiri kilomita nyingi kwenda Mbeya kujifunza jinsi gani Halmashauri ya jiji la Mbeya ilivyofanikiwa kuitengeneza @officialmbeyacityfc hadi kupata mafanikio yale!
Namna mashabiki waliokuwa wakijitolea kuiunga mkono timu kwenye michezo ya nyumbani na ile iliyochezwa nje ya dimba la Sokoine hakika ilikuwa jambo la kuvutia sana lililoicha @officialmbeyacityfc kuwa mfano wa kuigwa na mashabiki wa soka mikoa au miji mingine kutamani kuwa na timu kama hii.
Kumbukumbu wanazo wakazi wa Tanga, siku ambayo @officialmbeyacityfc ilikwenda kucheza na @MgamboJKT Mashabiki wa MCC waliliteka jiji lote ilifika mahala mpaka wanajeshi wakalazimika kuungana nao kuishangilia timu hii 😂
Kwenye mchezo wa kihistoria dhidi ya Azam fc uliochezwa Chamazi Complex na kumalizika kwa sare ya 3-3, achana na matokeo na mamba mengine yaliyojiri uwanjani ikiwemo uwanja huo kujaa kwa mara ya kwanza kwa idadi kubwa ya mashabiki hadi wengine kuzuiwa wasiingie ndani, kivutio kilikuwa nje ya uwanja!
Wakati msafara wa mashabiki ukiwa njiani kueleka uwanjani,Waziri wa Sanaa na michezo wakati huo nae alikuwa njiani kuelekea huko lakini alilazimika kupaki gari yake kupisha msafara huo na wakati msafara unapita waziri aliuliza kuna nini na hao ni kina nani? Baada ya kujibiwa ni mashabiki wa Mcc wanakwenda uwanjani kusapoti timu alishuka kwenye gari akaungana nao, hakika zilikuwa nyakati za furaha sana kwa @offficialmbeyacityfc
All the best @officialmbeyacityfc timu ya kwanza Tanzania kumiliki App timu ya kwanza kuuza jezi online kwa zaidi ya Tsh 70K.