Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) yatia aibu Côte d'Ivoire

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) yatia aibu Côte d'Ivoire

Tumechelewa Sana tunafanya maandalizi muda umeshapita

Mfano naona michango ndio inafanyika Sasa hivi kitu ambacho kilijulikana muda mrefu

Wizara ya utamaduni imeshindwankuelewa unapopata nafasi kama hii lazima uandae mwemwbwe za Kila hatari ulkifika kwenye mataifa ya watu mji unasimama na kuanza kujiliza huko TANZANIA KUKOJE?

Tuna Matajiri wa kutosha , tuna fedha za kutosha na kwa mwbwembwe tumebarikiwa

Tuna tamaduni nyingi za kuenda nazo ugenini tofauti na hizo za wamasai tulizokariri au za wasanii wa muziki tulizokariri au za machawa wa tatu wa Taifa tilio kariri au za mbunifu wa Mavazi aliyezaliwa mjini ngowi eti ndio ana buni Mavazi ya nchi

Viongozi wa wizara wao wanakwaza kwenda kuongeza nguvu majukwaani au kusafiri na timu hiyo inasaidia nini? Nini majukumu yako kama msimamizi wa utamaduni wa nchi? Ulifanya mdahalo wa Kitaifa kupitia vyombo vya habari kutuomba maoni ya waandamizi na ma concervative wa utamaduni wa asili ya jamii za Watanzania kabla ya ujio wa waarabu walioletan makanzu na wazungu walioleta masuti? Au tuendelee kuwapokea wageni pale JNA kwa matarumbeta eti ndio ngoma zetu za jadi au wale wa bagamoyo wenye mangoma yaliyochanganywa na utamaduni wa ulaya ya Scandinavia wanaovaa manguo ya rangi ya chui? Nadhani Doctor Mapana unanisikia.

Hii michango tunayochanga Sasa itasaidia nini kama tutatolewa katika hatua za awali? Nani atakuwa Kuna Taifa dume Africa linaitwa Tanzania lililokomboa mataifa mengine?

Tumepoteza fursa kubwa Sana ya KUINGIA na nafasi hiyo ndio ingeteka vichwa Cha habari duniani kote, nafasi hiyo ndio ingefanya kitabu mtu atamani kuja kuotembelea Tanzania, nafasi hiyo ndio ingefanya Kila Mchezaji Bora wa Afrika aje acheze ligi za Tanzania . TUMEINGIE KINYONGE MMO? Kweli Tanzania!!! Tuna midege, tuna machawa yadiyo na kazi mjini yenyewe ajira Yao ni vituko tuu, Yale unayasimamia unayapangia nini Cha kufanya maana bila usimamizi yataharibu tuanze kuonekana tena nchi ya ajabu. Wapo akina utopolo wa YANGA,wapo akina Mzaramo wa Simba, kule costal union Kuna jitu linaloimba mwanzo mwisho kama linatumia jenereta. Mbao ya Mwanza Kuna limtu linabeba moto kichwani ,tuna ngoma za asili origino mikoani zile ambazo za kujipaka majibu,asizi mask za asili na maleba ya kutisha ambao wakiingia tuu uwanjani bila hatamkuimba unaona watu wanashangilia sio hivyo vikundi vya hapo mjini wanakwenda kucheza ngoma na sare zenye ujumbe kabisa kama waimba kwaya?

Tena tusidhani inavutia wakati sisi ndio waandalizi hapana unakwenda kwa mtu unateka Kijiji unaonekana zaidi ya mwenyeji. Taifa lenye furaha linaloongozwa na Raisi Bora mvumilivu na mwenye upendo kwa watu wake, Taifa pekee Afrika lenye demokrasia na kujali uwasa wa binaadamu linaloongozwa na mwanamama pekee katitati ya maraisi zaidi ya 65 Afrika wenye mfumo dume wanaomini bila mwanaume nchi haiendi Sasa najua wanajua ila tungewaonyesha kuwa sisi ndio nchi yenye furaha zaidi Afrika nchi tunaolelewa na mama yetu. TUMEINGIE KINYONGE Sana hii nafasi hatuipatintena. Hata kama machawa wataenda baadaye kupitia mitaani na kwenye majukwaa bado uli uzito haupo tena. TUMEINGIE KINYOOOOONGE SANA
 
Kuna ombwe kubwa sana katika uendeshaji wa timu ya taifa. Nitaishia hapo bila kupoteza muda wangu.
 
All the best Taifa Stars, mavazi hayachezi mpira!
 
Kwanza haya mambo ya kuomba Hela kwenye vibaba na wakati wizara zinabajeti ni tatizo kubwa,kwani wale wabunge Huwa wanafanyaga Nini pale bungeni?huu naona ni aina nyingine ya upigaji.kukitokea majanga utasiki tuwachangie wenzetu? Kwani SI tunalipa Kodi jamani?
 
Back
Top Bottom