Timu ya Taifa ya wanawake ni tishio

Timu ya Taifa ya wanawake ni tishio

Kilimanjaro queens ni timu iliyokamilika kuliko taifa stars.
Hiyo midfield kuna mkata umeme mmoja ana rasta hivi Amina Ally, mbele yake Mwalala na kuna mkata umeme mwingine aliingia kipindi cha pili game ya Taifa stars na South Sudan anavaa jezi namba tatu hatari sana. Right wing Stumai Abdallah anaudambwi udambwi mwingi Simon Msuva akasome, left wing kuna mwanadada roho ya paka na mapafu ya mbwa Donisia Minja anapita vijiji uwanjani anapiga migoli hatari.
Tuki-invest hawa mabinti watatuwakilisha vyema sana kimataifa shida tupo kwa wale vijeba kwa sababu ya mazoea tu...

D.Minja pekee anauwezo mkubwa wa kufanya maamuzi kuliko strikers wa stars
 
France na USA wametuzidi kila kitu unataka tujilinganishe nao ?
tunawafunga wabovu wenzetu sema kwa afrika mashariki hakuna atakaetufunga ila bado hatuna timu bora ukitaka kujua tuna timu ya kawaida kafatilie ile game ya USA NA FRANCE world cup ya wanawake alafu anagalia game za tanzania
 
Katika michuano inayoendelea sasa hivi ya CECAFA SENIOR WOMEN CHAMPIONSHIP, Kilimanjaro Queen's imekuwa na muunganiko mzuri. Ukiwa unaiangalia timu hii unaona ule muunganiko mzuri.

Pia unaona usahihi wa pasi ambapo mara nyingi timu zetu zimekuwa zinapata shida.

Kuanzia golini mpaka bench la ufundi unaona muunganiko huo.

Mpaka sasa wachezaji waliotia fora ni Donisia, Double Aisha,Amina na kule nyuma ni balaaa. Mwalimu na benchi zima la ufundi wanastahili pongezi.

Pia timu nzima imekuwa ni nzuri sana. Mungu awasaidie wabakishe kombe nyumbani.

Mungu ibariki The Kilimanjaro Queens. Mungu ibariki Tanzania
Nashauri iwakilishe Taifa badala ya Taifa stars
 
Zanzibar leo wamefundishwa mpira na dada zao wakuu
 
hawa dawa yao ni kuwapambanisha na BANYANA BANYANA ya south africa ama wanawake wa NIGERIA na GHANA uone wanavyohemea matakoni[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
hawa dawa yao ni kuwapambanisha na BANYANA BANYANA ya south africa ama wanawake wa NIGERIA na GHANA uone wanavyohemea matakoni[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
[emoji23] [emoji23] [emoji23] Hata hao Banyana Banyana, Nigeria na Ghana wakajipange kwa timu hii ya sasa. Usiichukulie poa.
 
tunawafunga wabovu wenzetu sema kwa afrika mashariki hakuna atakaetufunga ila bado hatuna timu bora ukitaka kujua tuna timu ya kawaida kafatilie ile game ya USA NA FRANCE world cup ya wanawake alafu anagalia game za tanzania
Huko umeenda mbali, jiulize tu kama hata Taifa stars inaziweza hizo timu ulizotaja!
 
Wazuri CECAFA tu wakikutana na magiant Cameroon na Nigeria watapigwa wiki
 
Lakini wanacheza mpira mzuri ambao hata Taifa Stars haichezi. Bado nasema kwa sasa hata Cameroon na Nigeria wajipange.
Mademu wa Nigeria na Cameroon wanacheza Ulaya hatari man
 
Back
Top Bottom