Timu za Coastal Union na African Lyon zarejea ligi kuu ya Vodacom Bara (VPL) msimu wa 2018/19

Timu za Coastal Union na African Lyon zarejea ligi kuu ya Vodacom Bara (VPL) msimu wa 2018/19

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,957
Timu ya JKT Ruvu ikiongozwa na Kocha Bakari Shime almaarufu Mchawi mweusi leo imerejea kwa kishindo Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania ( VPL) baada ya kuichapa kwa bao 5 -0 timu ya Afrikan Lyon.
Kwa mujibu wa kanuni za Ligi Kuu jumla ya timu 6 zitapanda daraja hadi ligi kuu wakati timu 2 zitashuka daraja.
==================

Timu za soka za Coastal Union ya Tanga na African Lyon ya Dar es Salaam zilizokuwa zinacheza ligi daraja la kwanza zimefanikiwa kupanda daraja na zitacheza ligi kuu bara (VPL) msimu wa mwaka 2018/19.

Pamoja na timu hizo timu nyingine zilizopanda daraja msimu huu ni KMC ya mkoani Dar es Salaam, Alliance ya mkoani Mwanza, Biashara United ya mkoani Mara na JKT Ruvu ya Pwani

Timu za JKT Ruvu na African Lyon zilikuwa kundi A na kumaliza kwa alama 37 na 27. Timu za KMC na Coastal Union zilizokuwa kundi B, zimefuzu kwa alama 28 na 26. Timu za Biashara United na Alliance School zilikuwa kundi C na kumaliza kwa kuwa na point 27 na 25.
 
Nimefurahishwa zaidi na mpango wao wa kujenga kiwanja chao cha kuchezea mechi pale Mbweni
 
Washafata mfumo wa wazungu, hadi kuwa timu 20.
 
Coastal union imerudi ligi kuu kwa kuifunga Mawenzi market goli mbili kwa bila,mechi imechezwa uwanja wa jamhuri morogoro..nimefurahi kwa timu ya nyumbani kurudi ligi kuu..Ushauri wangu.Wache majungu na fitna za kukimbiza wadhamini.
 
Habar wana Jf

Kwanza kabisa namshkuru mungu kwa Timu yangu ya nyumbani Coastal union, wagosi wa kaya kwa ushindi wa leo wa mabao 2 walio yapata kwani ushindi wa leo ndio uliopelekea kupanda ligi kuu.

b64b888a1bf55c52857ffd9109966994.jpg


Hongera kwa wachezaji wote kwa kujituma hadi kushika nafasi ya 2 katika msimamo wa kundi, B na kuweza kujipatia tiketi ya kupanda ligi kuu: Msimu wa 2018--2019

688951304810f7a21a47cccb9f9a0192.jpg


Haikua kazi nyepesi kwani ligi daraja la kwanza lina changamoto nyingi.......

54ba4c01f0574eca808988d2fd5da2c8.jpg


hongera kwa viongozi wote walioipa sapport timu hadi kufikia hatua ya ligi kuuu.


TEAM B-13
 
Tatizo kubwa la wagosi wa kaya (coastal) ni kucheza kwa kuhakikisha kuwa hawafungwi na simba, yanga au azam. Lkn wakija majimaji, toto cjui kipanga fc ruksa kufungwa. Huu ujinga wasipoufuta wa kutumia nguvu kubwa kukamia timu tatu tu hlf inakubali kufungwa na timu 13 zinazobakia lazima warudi daraja la kwanza.
 
Back
Top Bottom