Timu za Tanzania na maendeleo ya Mpira Nchini

Timu za Tanzania na maendeleo ya Mpira Nchini

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Timu za Tanzania hasa Yanga, Simba na Azam zimejiimarisha sana kusajili wachezaji nyota kutoka nje ya nchi. Ingawa kwa kufanya hivyo kumeichangamsha sana ligi ya NBC mwaka huu, kinachosikitisha sana ni kwamba hali hiyo pia inadidimiza sana vipaji vya ndani, hivyo kuifanya Taifa Starts ibaki kichwa cha Mwendawazimu.
 
Jiulize , Kabla hata ya hizi timu kuanza kusajili wachezaji wa nje Tanzania ilishawahi kufanya vizuri lini mechi za kimataifa? Je, jina la kichwa cha mwendawazimu lilianza lini?

Acha tufurahie ligi bora. Siku wachezaji wetu wa ndani wakijitambua tutaacha kusajili wachezaji wa nje. Wasipojitambua timu iruhusiwe kusajili hata wachezaji wote wa kigeni ,hakuna namna.
 
Uingereza pamoja na kua na ligi bora duniani lkn timu yao ya taifa ni tia maji tia maji.

Wacha tufurahie ligi yetu, wacha yabga itume utamu.

Napendekeza na timu zingine zisaidiwe kujiimarisha ktka kusajili wachezaji wa nje ili kuondoa ufalme wa yanga na simba kwenye ligi yetu.

Hilo litimu gani sijui mlitaalo kichwa cha tahira wacha liendelee kua bovu tu. Kam boko ndo striker tegemewa unafikiria nn hapo.
 
Shida yetu wsbongo ni waoga,wachezaji,makocha wapambane na wao wasajiliwe huko nje ya mipaka.
Timu ya taifa sio jukumu la Azam,Simba au Yanga.
 
Back
Top Bottom