kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,154
- 17,491
Timu nyingi zinasajiri wachezaji kwa kuangali performances zao viwanjani, na hapo ndio neno la usajiri ni kamari linapoanzia.
Timu inayofanikiwa kwenye usajili ni ile inayozingatia uwezo wa mchezaji pamoja na mazingira (supporting background) yake yaliyomsaidia kuonyesha uwezo wake uliosababisha umuone kuwa anafaa kuwa mchezaji wako.
Mazingira ya mchezaji ni pamoja na hali ya hewa ya ligi anayocheza na ile unayotaka akacheze, vyakula, lugha, marafiki, nafasi anayocheza uwanjani, wachezaji anaocheza nao na mfumo anaocheza kwenye timu yake hiyo anayocheza. Mazingira yake hayo lazima yasiwe tofauti sana na mazingira unayompeleka kucheza kwenye hiyo timu mpya.
Kwasababu ya mazingira kuna wakati unaweza kulazimika kusajili wachezaji 2 kutoka timu moja ili mchezaji huyo mpya kumtengenezea mazingira kama yale aliyozoea. na wakati mwingine unaweza kulazimika huyu mchezaji aishi nyumbani badala ya kuishi kambini na wachezaji wenzake ili kumpatia mazingira aliyoyazoea; na upo wakati unaweza kukulazimika msajili na kocha wake pia.
Mfano, kama utamleta mchezaji mzaliwa wa ulaya au Afrika Kusini na kucheza ligi ya Afrika Kusini (baridi) na kumleta kwenye timu ya Yanga au Simba, au Azam (mazingira ya joto) msemo wa usajili ni kamari utatumika.